Makapuku Forum

Asante Madenge. Kuna watu huwa wanadhani kuwa huku Makapuku ni watoto tupu hatuelewi cho chote. Kumbe sivyo. Na sisi huku hata kama ni ishu siriazi tunajadiliana kwa heshima na staha bila kutukanana kama ilivyo huko kwao.

Ni kweli ulivyosema. We have to go back to the drawing board. Tatizo ni kwamba tuliacha misingi ya Kambarage na hatukuweka mingine. Matokeo yake sasa hata falsafa yetu kama jamii haieleweki japo bado tunajifanya tu wajamaa wenye lengo la kujitegemea. Na mimi naamini kuwa hata aje malaika kutuongoza bado tutakuwa tunaangukia pale pale kwenye kisiki na shimo lile lile. Inabidi kabisa kabisa tuamue kwa nia moja kutafuta dhana mpya kuhusu majukumu ya viongozi wetu (pamoja na uadilifu wao), elimu yetu (lengo lake ni nini katika wakati huu?) na hata utajiri (ifike mahali kiongozi aone aibu kutajirika kwa ufisadi, na jamii imkoromee - siyo sasa ambapo ukiiba sana ndiyo unasifiwa na kuitwa mjanja, na ukiwa mwadilifu ukastaafu bila kujilimbikizia mali unachekwa). Na mahali pazuri pa kuanzia ni kuwa na katiba mpya nzuri yenye uwiano na inayotokana na matakwa ya wananchi. Ndiyo maana namdharau sana Kikwete kwa sababu alikuwa ameji-position kuwa mmojawapo wa viongozi bora kabisa tuliowahi kuwa nao kama angetupatia katiba mpya ile ya Warioba. Lakini akaweka matakwa ya chama chake mbele baada ya kuona kuwa pengine kisingeshinda kama uchaguzi uliopita ungefanyika chini ya tume huru. Na kama hiyo haitoshi akatuongezea na sheria ya makosa ya mtandao. Leo hii rais ni kama mungu kwa sababu ana madaraka makubwa mno na watu hawana mahali hata pa kusemea.

Tupiganie kwanza katiba mpya mengine haya ni makelele tu na hakuna kitakachobadilika. Hata the so called wapinzani sijui kama wanalijua hili. Makapuku!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…