Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Mkuu, tuweke rekodi sawa.

urudishaji wa shule za dini na mahospitali ya dini ulianza awamu ya Ally Hassan Mwinyi sababu kubwa alipotambua kwamba huduma haziwafikii wananchi waliokuwa wanaongezeka kwa kasi lakini pia taasisi za dini zilimpa sharti kwamba kama serikali inaomba dini ziwekeze kwenye shule na hosptali basi alizotaifisha Nyerere zirudi kwanza. mkataba wa MOU ulitengenezwa mwaka 1992, Mwinyi amekuwa Rais 1985 - 1995.
Rekodi yako si ya kweli Hizo KCMC na Bugando zote zimerudishwa wakati wa Mheshimiwa Rais Mstaafu Mkapa,Pili MOU wala si moja baina ya serikali na Mashirika ya dini zipo MOU kwa mashirika tofauti ya dini na zimesainiwa muda tofauti na zimeanza toka mwishoni mwa utawala wa awamu ya kwanza kwa designated Hospitals kwa upande wa huduma za afya.
 
kwa kifupi sana waislam kila wanachofundishwa/ kuelezwa huwa hawafikiri sana kwa undani maana leo hii hata jambo nilakijinga wenzetu wanasema ndio. kufuta MOU sio suluhisho maana serikali ina depend sana kwenye makanisa angalieni shule, hospital kubwa zinahudumiwa na makanisa na wapa tu mifano michache (paramiho hospital, bugando hospital, etc.) na kuna shule nyingi tu ambazo zinaubora wa hali ya juu sana kuliko hata za serikali na ndio zinaiweka tanzania mahali pazuri kielimu na hata kimataifa kwenye nyaja za elimu
kcmc,st.francis,vyuo vikuu;saut,st.john,st.joseph,tumaini ,teku,arusha university na matawi yake lukuki kila kona ya nchi...udini ni kitu mbaya tukianza kubaguana ni hatari....inabidi taasisi hizi zitoe huduma kwa wote sawa bila kujali dini kwa ustawi wa taifa
 
Sikonge.
Mimi kama mchumi nakubaliana kabisa na wewe.

Kwani kama Serikali kwa dhati kabisa ingeamua kuachana na hiyo MoU na kutumia pesa hizo nafikiri tanganyika saa hizi mngekuwa mnazungumza mengine.

Kumbuka 1.3 Billion ni sawa na kujenga hospital za level ya wilaya na kuweka Vifaa vyote kabsa 4 na Chuo kimoja kikubwa sana cha Ufundi 1.

Kumbuka toka 1992 mpaka sasa 2012 ambapo ni 20 Yrs mngekuwa na Hospital za wilaya 80 na vyuo 20. Nafikiri ingakuwa kila wilaya na hata baadhi ya kata zingekuwa na hospital kubwa.

Suala la kujiuliza Hivi wale wachumi wenye uchungu na nchi yao wapo wapi? au hawalioni hili? au ndio wale wale wenye kunufaika na hili?
 
Mkuu Sikonge hawa mashehe wanaoipigia MOU kelele wanaishi mjini ama sehem za pwani ambapo waislam wapo kibao na hospital zimejaa tele. Ila kama wangekuwa wanaishi vijijini ambapo kuna hospital za wakatoliki tu wasingethubutu kuropoka ropka na kulalama kuhusu MOU.
Tatizo si MOU,tatizo hawa wenze2 ni wavivu kwenye kujishughulisha,michango mingi wakristo wanahimizana kufanya vi2 vya maendeleo,naamin kusitisha MOU kwa wakristo si tatizo kwan maendeleo ya wakristo hayachangiwi na MOU,kabla ya MOU tasis za kikristo zilijiendesha vizuri,serekal ilijipendekeza yenyewe..serekali pia itakiwa irudishe hospital zote za wakristo KCMC,BUGANDO,MUHIMBILI(anglican) atc.,alafu mkatibiwe MOU ya serekal.
 
Last edited by a moderator:
Kutokana na kulalamikiwa saana na Waislaam kuwa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Makanisa (MOU) yanafanya nchi hii iwe na "Mfumo Kristo" na hivyo kuwanyanyasa Waislaam na hata kuwatawala, inabidi ifike wakati Makanisa yaanze kufikiria jinsi ya kuvunja mkataba huo na kurudi kama ilivyokuwa zamani.

Kwa sababu hili swala limeonakana likichochea sana vurugu, mie napendekeza lifuatalo:

- Wavunje mkataba wa MOU na Serikali.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mahospital ya Kanisa.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mashule ya Kanisa nk.

-Makanisa na vitengo vyake, viwe vinalipa kodi kwa kufanya biashara ya Hospitals, Shule nk.

-Gharama kwa walio Wakristo, ziwe zinapunguzwa kwa wingi kwa sababu wao hutoa michango mingi tu ya kuendeleza kanisa na sadaka za kila Jumapili.

-Kwa wasio Wakristo na hapo wanapoishi hakuna hospital ya Serikali au ya dini yao, basi itabidi wailazimishe Serikali MPYA ya Tanzania ambayo haitakuwa na Mfumo Kristo tena ili wawajengee Hospitals za Serikali.

Kama Serikali ikishindwa basi wajiandae kulipa gharama kubwa kwenye huduma hizo za jamii au KUBADILI DINI. Kama siyo hilo basi na wao na dini zao wajenge hizo huduma za jamii ili kushindana na za Makanisa.

Nafikiri muda umefika wa kuonyesha kuwa Viongozi wa Makanisa ni Wasomi wa hali ya juu na siku zote "Akili kubwa hutawala akili ndogo......" Vinginevyo, akili zao zitakuwa kazi bure kama hawawezi kutatua matatizo yaliyowazunguka.

Kama kuna kundi jingine au Serikali litakuja na mbinu mbadala na kuweka huduma hizi za jamii katika bei nafuu zaidi, basi ina maana huduma za jamii kutoka kwenye Makanisa tutakuwa hatuhitaji tena. Maendeleo yanakuja kwa mashindano. Muda umefika Makanisa kutangaza mashindano kwa kutoa huduma za JAMII VS dini nyingine au Serikali.
--
NECTA nayo ifanyweje?
Wakristo walio wengi maofisini hujasema wafukuzwe kazi nafasi zao zizibwe na waislam ili iwe pasu kwa pasu
 
Mkuu Nitonye, nafikiri unamfahamu Mkandara wa JF ambaye ni mtu anaishi nje ya Tanzania hadi sasa kama sikosei. Ni msomi mzuri tu na mtu mwenye heshima yake kubwa sana hapa JF. Mie pia nimejifunza mengi sana kwa makala zake.

Ila nakuomba uende ukurasa huu: https://www.jamiiforums.com/habari-...ofu-lakutana-mbagala-latoa-tamko-zito-11.html

Na ukishasoma Maelezo yake, nafikiri utanielewa kwa nini nilianzisha hii thread. Ukiona Wasomi wa Kiislaam wanaandika hivi, basi huko kijijini hesabu maumivu. Labda wakiona Waislaam vijijini wanabadili dini kwa wingi ili wapate huduma (Makanisa yanaweza hilo kabisa kulifanya ingawa mie SILIPENDI na ningelipenda ni SERIKALI ilifanye, ila ndiyo Serikali yenyewe hiyo tunayo) basi Wasomi hawa na hao wadhamini wao wataanza kufunguka macho.

Ni njia moja KALI sana ila nisingelipendelea kufika huko. Kama alivyosema Jasusi ni kuwa hata MOU ikivunjwa, baso watu watalialia. Ila ukweli unabaki kuwa sasa watajilaumu wenyewe.

Ni Kama Zanzibar ambavyo wanalilia kuvunja Muungano. Unawapa wajitawale kwa miaka 5 na baada ya hapo ndipo mnakutana tena mezani kama "vipi muungano uvunjwe sasa au mnarudi kuwa mkoa wa Tanzania?"

Ni kujaribu tu kuangalia kipi kifanyike ili kumaliza hizi kelele za kila siku kuhusu Mfumo Kristo ambazo hata Wasomi wazuri kama wale waliopo NSSF ila kwa kuwa wapo dini nyingine basi wamekuwa vipofu.
Sikonge naomba unijibu haya maswali:

Je, ulishawahi kuusoma huo mkataba kati ya serikali na MOU?

Na jibu kama ni ndiyo je kuna kipengele kinachozuia taasisi nyinyine za kidini kama za kiislam nazo kuingia mkataba na serikali kwa shughul za kijamii?
 
Last edited by a moderator:
Nakwambia ata wakitoa misamaha ya kodi hospital

with your comment, You made my day.......
 
Mkuu Nitonye, nafikiri unamfahamu Mkandara wa JF ambaye ni mtu anaishi nje ya Tanzania hadi sasa kama sikosei. Ni msomi mzuri tu na mtu mwenye heshima yake kubwa sana hapa JF. Mie pia nimejifunza mengi sana kwa makala zake.

Ila nakuomba uende ukurasa huu: https://www.jamiiforums.com/habari-...ofu-lakutana-mbagala-latoa-tamko-zito-11.html

Na ukishasoma Maelezo yake, nafikiri utanielewa kwa nini nilianzisha hii thread. Ukiona Wasomi wa Kiislaam wanaandika hivi, basi huko kijijini hesabu maumivu. Labda wakiona Waislaam vijijini wanabadili dini kwa wingi ili wapate huduma (Makanisa yanaweza hilo kabisa kulifanya ingawa mie SILIPENDI na ningelipenda ni SERIKALI ilifanye, ila ndiyo Serikali yenyewe hiyo tunayo) basi Wasomi hawa na hao wadhamini wao wataanza kufunguka macho.

Ni njia moja KALI sana ila nisingelipendelea kufika huko. Kama alivyosema Jasusi ni kuwa hata MOU ikivunjwa, baso watu watalialia. Ila ukweli unabaki kuwa sasa watajilaumu wenyewe.

Ni Kama Zanzibar ambavyo wanalilia kuvunja Muungano. Unawapa wajitawale kwa miaka 5 na baada ya hapo ndipo mnakutana tena mezani kama "vipi muungano uvunjwe sasa au mnarudi kuwa mkoa wa Tanzania?"

Ni kujaribu tu kuangalia kipi kifanyike ili kumaliza hizi kelele za kila siku kuhusu Mfumo Kristo ambazo hata Wasomi wazuri kama wale waliopo NSSF ila kwa kuwa wapo dini nyingine basi wamekuwa vipofu.
Kama Kuna mtanzania anafikiri Mashirika ya Kidini yaliyo na MOU na serikali yataamua kujitoa kwasababu watu fulani wanalalamika hilo wasahau kwasababu wao wanafaidika na wanawachuna Tax Payers wote kama mafisadi na wabinafsi wanaofikiria kujinufaisha wao tu.Ila tofauti ya mafisadi na haya mashirika ya dini ni kwamba mafisadi wanaiba na mashirika ya dini wametumia udhaifu wa viongozi mafisadi kujinufaisha na wao.
 
wewe ni mpuuzi wa kwanza na wa mwisho!!!hao waislam wako wameshindwa kuanzisha hata zahanati ili mpate hiyo ruzuku!!what kind of people are you?hamna shukrani kabisa,nenda hospitali za misheni utakuta wapemba kibao na hijab za kutosha,if you tell this in their faces they will definitely spit at you moron.

Unaongea kwa kutumia mdomo wa nyuma thats the ****.....
Hizo misheni unazosema zilijengwa na nani kama si mkoroni kwa kutumia rasilimali za Tanzania. Unless muanze kusema sasa hata madini ni ya kwenu wakristo peke yenu...
Your insane you know that...don't you
 
Barubaru,

Ukipata nafasi likizo moja, njoo Sikonge Hospital ya Moravian Church ambayo hutibu hata ndugu zako wengi tu akina Chapa, Hemmed Nasoro, Koronzo, nk ambao wamejaa Sikonge, Tutuo na Chabutwa.

Hii hospital tangu mwaka 2006, pesa wanazotakiwa kulipwa zilipunguzwa na sasa hawapati kabisa. Wao wanatibu ndugu zako wa pale Sikonge BURE kwa misaada kutoka nchi za Mashoga kama Uholanzi, Ugeruman, nk na hawawabagui kama ni Waislaam, Wapagani, Waarabu, Wahindi nk nk.

Tafadhali sana Barubaru, ukiweza kuitisha HARAMBEE, basi kusanya PESA na uje SIKONGE Hospital kwanza, uone kama kweli WAMETAJIRIKA kwa MOU au WANAFILISIKA kwa MOU. Ukishapata jibu basi hizo pesa wapatie au rudi zako QATAR. Njoo Sikonge tafadhali siku moja na ndiyo utaona ukweli maana hiyo ndiyo Hospital ya Wilaya pekee kwa SIKONGE.

Kama kweli wewe ni Mchumi na moyoni mwako ni Mcha Mungu (Allah) basi njoo huku na wewe utufungulie na Serikali hospital yako na Moravian Church watabaki kuhudumia wafanyakazi wao tu bila kuchukua pesa za MOU.

ANGALIZO: Kama Muhimbili hawana Pesa, madawa, vitendea kazi..... kweli hospitals na mashule ya Makanisa ndiyo wanaokusanya pesa za Serikali? Wengine wanasema ndiyo. Wewe kama Mchumi unaamini kweli kwamba "Tanzania inafilisika kwa sababu ya MOU?"

Sikonge.
Mimi kama mchumi nakubaliana kabisa na wewe.

Kwani kama Serikali kwa dhati kabisa ingeamua kuachana na hiyo MoU na kutumia pesa hizo nafikiri tanganyika saa hizi mngekuwa mnazungumza mengine.

Kumbuka 1.3 Billion ni sawa na kujenga hospital za level ya wilaya na kuweka Vifaa vyote kabsa 4 na Chuo kimoja kikubwa sana cha Ufundi 1.

Kumbuka toka 1992 mpaka sasa 2012 ambapo ni 20 Yrs mngekuwa na Hospital za wilaya 80 na vyuo 20. Nafikiri ingakuwa kila wilaya na hata baadhi ya kata zingekuwa na hospital kubwa.

Suala la kujiuliza Hivi wale wachumi wenye uchungu na nchi yao wapo wapi? au hawalioni hili? au ndio wale wale wenye kunufaika na hili?
 
Nyongeza ya hayo:

Kuna pia hospital za taasisi za Kiislam japo si nyingi kwa sababu hawana umoja wa kuzichangia ili zijengwe na zipate MOU pia. Kwa nini Miskiti kama yalivyo makanisa kwa Parokia na Usharika yanavyochangishana kujenga, na Miskitiki kimitaa wasichangishane kujenga Hospital na kuomba MOU pia.

Pia kuna shule nyingi za Kiislam lakini matokeo yake ya mitihani yanajulikana kwa sababu hawatafuti walimu walio na qualification, pia walimu wao wana motisha ya mishahara mizuri, na pia wanafunzi wanaochaguliwa kwenye shule zile za Kiislam haijalishi matokeo yao ya darasa la saba yalikuwaje, na waislam walio wengi hawawatii watoto kusoma elimu dunia zaidi ya elimu ya madrasa na kuchangia kutofanya vizuri kwenye mitihani yao.

Shule za Kikristo either zinafundishwa na mapadre au wachungaji au masista kwa hiyo nidhamu ni msingi wa kwanza ili uweze kuendelea na shule hiyo. Pia juhudi za darasani vinginevyo unatimuliwa. Ebu Waislam wajaribu njia hiyo tuone kama hawatafanikiwa.
Pia Juhudi binafsi na ubunifu uwepo wa kuchangishana misikitini kujenga shule na hospital za taasisi hizo na serikali inapenda kitu hicho na mara wakishajenga serikali iko tayari kuingia MOU kama ilivyo kwa taasisi za kikrito.

Na hata hivyo hizo shule chache na hospital walizo nazo nazo ziko mbona kwenye MOU na serikali?

Haya ni mawazo mgando kwani yanaonyesha udini hasa, hivi kwa mawazo yako kwa nini hao waislamu wasianze kutoa huduma hizo za bei nafuu ili watu wengine waende huko na ama wao kuwa na MOU na serikali kwani nani kawakataza au kuna faida gani kwa muislamu kung'ang'ania huduma za gharama kubwa anazojua zinafuja kodi yake kama hanufaiki nazo?

Hata hivyo hujalazimishwa kutumia huduma za kanisa kama unaona kutumia huduma hizo ni mfumo kristo tumia za kiislamu maana una uhuru huo wala hulazimishwi. Hiyo misamaha na hata hiyo MOU unayosema haijazuiwa kwa waislamu na sijaona ukishauri kuwa waislamu wawe na MOU na serikali maana misamaha ya kodi tayari tunanufaika nayo.

Si waislamu wote wana mawazo ya udini kama haya kwani wanaelewa athari zake.
 
Tatizo si MOU,tatizo hawa wenze2 ni wavivu kwenye kujishughulisha,michango mingi wakristo wanahimizana kufanya vi2 vya maendeleo,naamin kusitisha MOU kwa wakristo si tatizo kwan maendeleo ya wakristo hayachangiwi na MOU,kabla ya MOU tasis za kikristo zilijiendesha vizuri,serekal ilijipendekeza yenyewe..serekali pia itakiwa irudishe hospital zote za wakristo KCMC,BUGANDO,MUHIMBILI(anglican) atc.,alafu mkatibiwe MOU ya serekal.
Sasa Ukienda kusali Jumapili si uwashauri wajitoe kama wana jeuri hiyo!wananufaika na hawawezi kujitoa na usifikiri kwamba serikali inajipendekeza bali viongozi wa mashirika hayo ya dini waliwapiga mkwara viongozi dhaifu wa serikali na ndiyo wakafikia DEAL.na ndiyo maana wamefungwa midomo hawakemei maovu ya Viongozi wetu na wanawaita kwa majina yenye sifa nzuri!
 
Mama Porojo,

Nilikuwa nazikimbia habari zako siku zote nikijua kuwa wewe ni Mchemshaji. Wewe kweli ni ACTOR mzuri sana, hongera.

Nafikiri huu ujumbe wako inabidi ausome Mchumi wetu Dr. Barubaru
Kanisa limewahi kuendesha mashule na mahospitali yake bila ya MOU ni busara sasa kanisa na hata taasisi za Aghakan foundation zijitoe kwenye mkataba huo kisha kanisa lifanye biashara ya shule na hosptali ambapo wale waliojenga mashule hayo na mahosptali wanaweza kupewa unafuu wa karo za shule na nafuu ya kulipia tiba.

Hofu yangu ni kwamba kwa kuwa nchi imeanza kuvurugika kidini kuna ishara kwamba baada MOU kuvunjika kanisa linaweza kutoa vitambulisho kwa waumini wake ili wasome kwa nafuu na kutibiwa kwa nafuu na wasio waumini wa kanisa watalipa gharama za juu.

Hii inawezekana kutokana na imani kwamba wakati huo fedha za sadaka, zaka, harambee, mavuno na minada ya kanisani itakuwa inaendesha huduma hizo na serikali haitakuwa na mkono wake katika huduma za kidini.
 
Last edited by a moderator:
Lunyungu,

Amka ndugu yangu. Naona hadi leo hujamfahamu Sikonge na aina yake ya Uandishi.

Wakati mwingine napenda kuchokoza. Ukatoliki naufahamu sana na kwa taarifa yako nguvu yake imepungua sana kwa sasa. Pana wakati walikuwa juu mno hadi Tudor Family na Wageruman walipoanza kuwapinga. Niendelee...????
Sikonge amka kumekucha sasa,

Fanya uchunguzi utagundua kwamba Dunia nzima inaendeshwa kwa mfumo Katoliki wala si Kristo is just Catholic. Rudi uliza wana sheria watakueleza vyema uwezo wa Canon Law ulivyopenya kote.

Halafu MoU ile is jusy PPP amka cha kulialia wewe
 
Last edited by a moderator:
Unakumbuka J.K alivyowajibu kwenye baraza la Idd? Sijui wamefikia wapi. Ogopa mtu mwenye wivu halafu hataki kujishughulisha.
 
Ni kweli mkuu Waislamu waende shule waache kulalamika kuwa wanabaguliwa. Hakuna anayewabagua bali wanajibagua wenyewe kwa kutoenda shule. Matokeo yake wanabaki na chuki dhidi ya wakristo na kuendeleza ugaidi kama sheikhe Ponda anavyofanya kwa kuhamasisha uchomaji wa makanisa.
Tatizo la waislamu lipo karibu kwa watu wote, WALIOSOMA NA WASIOSOMA. Wakati unategemea waliosoma wawasaidie ambao hawajasoma unakuta na wao wakiwa kwenye vikao vyao wote wanawaza vilevile. Mapendekezo ya mtoa mada siyo tu ni ya kitoto bali pia yanaonesha ni ya mtu aliye soma lakini ameamua kufikiri kama wasio soma.

NI KAMA ANAPENDEKEZA KUWAWALIO ENDELEA WAWASUBIRI WALIO NYUMA KIMAENDELEO.

Waislamu walio wengi elimu kwao ni kama anasa. Ukiangalia maeneo yaliyo na waislamu wengi mahudhurio ya watoto wao shuleni yako chini ya asilimia 50. Ukienda BAGAMOYO, CHALINZE, LINDI YOTE, MTWARA YOTE KASORO MASASI, siku mvua ikinyesha tu asubuhi mahudhurio yanashuka hadi asilimia 25!! Hali kama hiyo huwezi kuikuta Kilimanjaro, Mbeya, Shinyanga, Iringa, Ruvuma, na maeneo yote ya wakristo wengi.

Kama wakitambua kuwa elimu ni ufunguo wa maisha basi ungetegemea kuona wanajenga shule nyingi zenye ubora wa hali ya juu na kuimarisha uongozi wa shule zao sambamba na kutafuta walimu wenye sifa nzuri kitaaluma na siyo kiroho tu. Shule zao siyo tu zinatia huruma lakini pia nyingi zinaendeshwa kimagumashi. Karibu zote wastani wa kufaulisha watoto kwenda kidato cha tano ni asilimia kati ya 2 hadi 5 tu.

USHARI WANGU NI wajitathini wenyewe kwanza.
 
Hayo si mulimuuliza sheikh J.K kwenye baraza la idd? Tuambie aliwajibu nini acha kuchanganya watu hapa.
Wengi wanazunguzia hili bila kulijua.

Kwa ufafanuzi kidogo ni kuwa MOU ya Kanisa na Serikali ilifungwa mwaka 1992 na Edoward Lowasa. Kila mwaka makanisa yenu yanapata Billioni 60 (sasa hivi yanapata Billioni 91) .

Toka 1992- 2011 ni miaka 19= 60,000,000,000 x 18 + 91,000,000,000 x 2= Trilioni 1.29 or Trilioni 1.3. Kutoka katika kodi za WATANZANIA.

Na pesa hizo ni Admin cost. Vile vile Serikali yenu inagharamia Pesa za Uendeshaji (Op Cost) za hospital hizo ikiwemo pamoja na kutoa misamaha ya kodi kwa vifaa vinavyoingizwa na makanisa hayo.

MoU at work,

Somalia, Misri, Libya, Nigeria, Syria, etc...

Tatizo kuna Waislamu wachache Humu duniani wanatamani Dunia nzima iwe ya Kiislam kitu ambacho itakaa itokee. Ukishakuwa na mawazo kandamifu kama hao waislamu wachache lazima uwe mkorofi.

Tatizo vijana wetu wengi hawaelewi wanatumiwa na hao wachache kwa malengo yao binafsi nao wanakubali tu kutumika. Unawezaje kusema Nchi ina Mfumo Kristo wakati zaidi ya 60% ya watawala wa Nchi ni Islams?

Chukulia mfano hizo hospitali: Hapa Dar Hospitali kubwa wamiliki ni nani? TMJ, Regency, Aghakhan, Burhan e.t.c zote hizo za ukristo!? Mfumo Kristo ungewaachia mjenge Magorofa Karikakoo nzima!? Tatizo lenu kubwa ni ubinafsi kwa mwenye nacho na wasio nacho wamejaa chuki na fitna. Badilikeni ndugu zangu.
 
Barubaru,

Ukipata nafasi likizo moja, njoo Sikonge Hospital ya Moravian Church ambayo hutibu hata ndugu zako wengi tu akina Chapa, Hemmed Nasoro, Koronzo, nk ambao wamejaa Sikonge, Tutuo na Chabutwa.

Hii hospital tangu mwaka 2006, pesa wanazotakiwa kulipwa zilipunguzwa na sasa hawapati kabisa. Wao wanatibu ndugu zako wa pale Sikonge BURE kwa misaada kutoka nchi za Mashoga kama Uholanzi, Ugeruman, nk na hawawabagui kama ni Waislaam, Wapagani, Waarabu, Wahindi nk nk.

Tafadhali sana Barubaru, ukiweza kuitisha HARAMBEE, basi kusanya PESA na uje SIKONGE Hospital kwanza, uone kama kweli WAMETAJIRIKA kwa MOU au WANAFILISIKA kwa MOU. Ukishapata jibu basi hizo pesa wapatie au rudi zako QATAR. Njoo Sikonge tafadhali siku moja na ndiyo utaona ukweli maana hiyo ndiyo Hospital ya Wilaya pekee kwa SIKONGE.

Kama kweli wewe ni Mchumi na moyoni mwako ni Mcha Mungu (Allah) basi njoo huku na wewe utufungulie na Serikali hospital yako na Moravian Church watabaki kuhudumia wafanyakazi wao tu bila kuchukua pesa za MOU.

ANGALIZO: Kama Muhimbili hawana Pesa, madawa, vitendea kazi..... kweli hospitals na mashule ya Makanisa ndiyo wanaokusanya pesa za Serikali? Wengine wanasema ndiyo. Wewe kama Mchumi unaamini kweli kwamba "Tanzania inafilisika kwa sababu ya MOU?"

Sikonge,

Awali ya yote nimefurahi sana kumtaja Cousin wangu Hemed Nassor. nakuomba sana mpe salam sana.
Kifupi naifahamu sana Sikonge na hata mwaka huu July nilipokuja nilifika mpaka huko.

Sasa katika mas'ala yako yana sehemu mbili.
1. Kuhusu Kutoa misaada sehemu hiyo. Hilo nitakujibu kuwa moja ya maeneo tuliokuwa tunazungumza na Dr Abdallah Kigoda ni kuhusu mkoa wa Tabora. Tumeichambua kwa kina sana Tabora ikiwemo na kuonyesha mapunguvu yenu katika Sera za Uwekezaji na vile vile urasimu ndani yya TIC. Lakin all in all kwa tabora tumeainisha mambo makuu matatu. Kwanza Serikali ihakikisha inatengeneza barabara zote za tabora na vile vile kuwe na ufafiri wa uhakika wa Reli. Lakin vile suala la nishati ya umeme ni muhimu sana kuwepo kwani KUNA WENGI WANATAKA KUJA HUKO KUFUNGUA VIWANDA VYA KULINA NA KUFUNGASHA ASALI. Pitia taarifa ya Dr Kigoda na wafanyabiashara wa Oman.

Lakin suala la pili. Mimi naamini uwekezaji mkubwa ni kuwa na rasilimali watu ambao wamesheheni ilmu na kuwa na vitendea kazi bora. UNAJUA KANISA halijawekeza katika HOSPITAL bali limewekeza katika majengo ya hospital. Kwani wataalamu takriban wote wanalipwa na ni waajiriwa wa Serikali na wanalipwa na Serikali. vifaa vya hospital na madawa yote yanatoka MSD ambayo ni ya Serikali. Ukiondoa Admin ya hospital.

ndio maana nikafafanua kuwa kama mngetumia Pesa mnazolipa katika MoU yenu saa hizi mngekuwa na Mahospital mengi sana kwa level kama ya Mwananyamala au Amana na WANGECHUKULIWA WALE MADAKTARI NA KUINGIA KWENYE HOSPITAL HIZO NA HILO PASI NA SHAKA YOYOTE HOSPITAL HIZO ZA KANIS ZINGEKUFA KIFO CHA MENDE. Kwani sifikirii kama zingeweza kujiendesha kibiashara kama ilvyo Agha Khan au Ibrahim hadji.

Kumbuka Hospital sio majengo bali ni wataalamu, vifaa na madawa.

Back
Top Bottom