Mkuu, mimi mwenyewe naunga mkono kuvunja MOU kwa sababu ya usalama wa nchi yetu lakini sio kweli kwamba kanisa haliwezi kujiendesha sidhani kama hiyo ndio dhamira ya malalamiko ya waislamu. Mimi nadhani hoja hapo ni kwamba MOU imeleta malalamiko na kama ingekuwa na faida hata waislamu wangeomba MOU serikalini ( Rejea hotuba ya Rais KIKWETE siku ya IDD akisema kwa kinywa chake kuwasihi waislamu wapeleke maombi) ingawa hadi sasa taasisi za aghakan zina MOU na serikali.
Kabla ya uhuru na hata kabla ya MOU kanisa lilikuwa na shule na hospitali kama ilivyokuwa kwa waislamu liliendesha kwa fedha za sadaka, zaka, harambee, mavuno, minada, maduka ya kanisa na maegesho ya magari inayofanyika makanisani kwa ajili ya shughuli zote za maendeleo ya kanisa.
Kuhusu posho za madaktari inategemea MOU ilikuwa na makubaliano yapi??? Pengine serikali inalipa madaktari bila kujali dini zao kwani daktari anaweza kuwa wa dini yoyote kama ilivyo kwa mwalimu wa shule ya kanisa. kuwalipa posho madaktari kama lengo ni kupunguza gharama za tiba kwa watu wa dini zote ni jambo jema. Je, wagonjwa wengi ni wa dini ya wakristo?
bado naunga mkono kuvunja MOU.