Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Mkuu,

Hii makala imeanzia mbali, kule kwenye ripoti ya mkutano wa viongozi wa makanisa KKKT.

Pia, Kama mwanao Sikonge ulikuwa hufahamu huandika vitu kwa kutumia kamera ya 3D basi nikupe pole. Chukua miwani ya kuona picha za 3D na ndipo utaweza kumuona vizuri sana Sikonge alikuwa anamaanisha nini.

Zama chini chini chini zaidi na huko ndiyo tutakutana. You are Great Thinker I hope 🙂
Mwanangu Sikonge nilikuwa nikikuheshimu na kukuhusudu bila kujua kuwa kumbe wewe ni bomu! Tukianza kuangalia mambo kwa mboni za udini hawa tulielemika vya kutosha na kutisha tutaonekana mataahira na vihiyo kama ambayo hoja yako imekuweka. Hakuna mfumokristo bali mihangaiko na hisia za mfumo huo. Tukiangalia waislamu wanavyovumiliwa kwenye kutaka kuvunja amani kila mwenye akili anakushangaa. Ondoa hiyo miwani yako ya mbao na kiarabu uuangalie utanzania.
 
Mwanangu Sikonge nilikuwa nikikuheshimu na kukuhusudu bila kujua kuwa kumbe wewe ni bomu! Tukianza kuangalia mambo kwa mboni za udini hawa tulielemika vya kutosha na kutisha tutaonekana mataahira na vihiyo kama ambayo hoja yako imekuweka. Hakuna mfumokristo bali mihangaiko na hisia za mfumo huo. Tukiangalia waislamu wanavyovumiliwa kwenye kutaka kuvunja amani kila mwenye akili anakushangaa. Ondoa hiyo miwani yako ya mbao na kiarabu uuangalie utanzania.

Soma tena na tena alichoandika Sikonge halafu umwombe radhi.
 
Mwanangu Sikonge nilikuwa nikikuheshimu na kukuhusudu bila kujua kuwa kumbe wewe ni bomu! Tukianza kuangalia mambo kwa mboni za udini hawa tulielemika vya kutosha na kutisha tutaonekana mataahira na vihiyo kama ambayo hoja yako imekuweka. Hakuna mfumokristo bali mihangaiko na hisia za mfumo huo. Tukiangalia waislamu wanavyovumiliwa kwenye kutaka kuvunja amani kila mwenye akili anakushangaa. Ondoa hiyo miwani yako ya mbao na kiarabu uuangalie utanzania.
Wakati serikali inatoa misamaha wa kodi hawaangalii hawa ni wakristo au waislamu. Tatizo lipo katika matumizi ya misamaha ya kodi ma vipaumbele vyao.

Wakati wengine wanajenga shule na hospitali kwa wingi,wenyewe wanajenga misikiti, unakuta eneo lina waislamu say 5 wanawajengea msikiti mkubwaa wakati shule na hospitali hakuna.ukianzia DAR kwenda mbeya kuna misikiti zaidi ya 100 wakati shule zao za sekondari zenye ubora hakuna hata moja.

Je, wakristu wakiwa na roho ya kubagua waislamu si wataathirika sana? Jukumu la waislamu ni kuona kuwa haina maana kuendelea kuendelea kuwahubiria waislamu wenzao juu ya uislamu kwani tayari wana fahamu uislamu ni nini. Wanatakiwa sasa waanze kuwafundisha wasio waislamu waujue uislamu kwa kuwashawishi kwa uunguana na siyo kuwachukia wakristo na wasio na dini.
 
makanisa yamenufaika sana na yanaendelea kunufaika na MOU pamoja na misamaha ya kodi.

Ndiomana serekali ilipojaribu kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za dini wakapiga kelele mpaka ikashindikana.

Serekali haijashindwa kujenga hosptali au shule, makanisa yaendeshe shule zake na hospt na yaache kutegemea kodi tunayolipa watanzania wote inufaishe watu wachache.

Tuangalie chanzo cha malalamiko ya waislam na tukitibu na sio kujaribu kutibu matokeo kama lilivyofanya tamko la maaskofu leo.

Kuishia kulaumu waislam sio suluhisho, makanisa yajitoe kwenye MOU na yasiingilie mambo ya waislam kama walivyofanya kwenye tamko lao la leo walipozungumzia suala la mwinyi kupigwa kofi au kugomea sensa.
Unajua na taasisi ya kiislamu ya Agha Khan wana MOU na serikali ya kutolipa kodi yoyote. Mbona nao hujawataja wajitoe? Kwanini hujasema chuo kikuu cha kiislamu Morogoro kirudishe majengo ya msaada kutoka serikalini?
 
jmushi1 MOU si kwa wakristo tukuna hosp iko pale dar na arusha inataka kufungua tawi jina nimelisa ni mwislam nayoinapewa fungu kubwa ni ile hospital ambao zitt alilazwa miezi michache akiwa na maralia 150..
 
Last edited by a moderator:
Mbona matajiri wa Kiislam hawajengi mashule na vituo vya afya? Wao wako busy na kujenga misikiti na kufadhili fujo na vurugu. Badilikeni
 
Misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini ni kwa dini zote, pamoja na uislamu, vinginevyo mtoa hoja aseme uislamuu si dini bali ni chanzo na mfumo wa vurugu tu duniani. Historia inaonesha kuwa hata rais kikwete kasoma shule za wakristo siza waislam kwani hazikuwapo. Pia katibiwa kwa masangoma ambao ni viongozi wa dini za jadi na pia kwenye hospitali za kikristo.

Serikali ilipotaifisha mali za taasisi mbalimbali wakati wa azimio la arusha,ni makanisa yaliyonyang'anywa majumba, shule, hospitali na miradi kadhaa, mfano ni chuo kikuu cha mkwawa ambacho hadileo serikali yetu inayoendeshwa kiislamu haijarudisha kwa kanisa.

Hospitali za bugando na kcmc ni kubwa na hutoa huduma kwa wote hadi sasatangu kabla ya kutaifishwa na kisha kurudishwa kwa makanisa zikiwa kama magofu ya kufugia panya.

Wakati makanisa yakinyang'anywa, waislamu wakapewa chuo cha tanesco kilichojengwa kwa kodi za wote kuwa chuo chao kikuu ambapo usajili wake huwapendelea waislamu kwa wazi huku serikali inayoendeshwa kiislamu ikijua yote.

Kama hiyo haitoshi, serikali inayojitapa haina dini, imewaruhusu waislamu kuvaa nguo zao za kidini(hijabu) shueni na sehemu za kazi wakati watu wadini zingine wakuzuiwa. Machinjio ya serikali nayo yamesilimishwa na kusaliwa na mashehe wakati nyama hailiwi na waislamu tu.

Kuna mifano mingi ya upendeleo kwa waislamu na hivy mtoa mada asipotoshe umma eti wakristo wanapendelewa wakati wao ndio wanaopendelewa na serikali inaendeshwa kiislamu zaidi wakati wote kuliko kisekula wavyojidai.

Asalaam aleykum.
 
Waislamu wa TZ acheni ubaguzi wa kidini mtaifikisha nchi pabaya!
Rais wetu Muislamu makamu wake Muislamu wizara zote nyeti Waislamu hata wizara ya Afya unayolalamikia iko chini ya Hussein Mwinyi.
Kama tatizo ni MOU je nyie mmezuiliwa na nani msijiunge nayo?
Acheni mawazo mgando tuache udini tuiendeleze nhi yetu pamoja.
 
JERUSALEMU

Wakristo kwa mtazamo wako wewe wamesoma na wanamaendeleo sana, inakuwaje wanahubiriwa kwenye makanisa yao wanayoyaita ya kiroho kuwachukia waislam? Kudharau waislamu, hilo nalo utalirekebisha vipi? Mimi ni mkristo sio mlokole.
 
Last edited by a moderator:
kwa kifupi sana waislam kila wanachofundishwa/ kuelezwa huwa hawafikiri sana kwa undani maana leo hii hata jambo nilakijinga wenzetu wanasema ndio. kufuta MOU sio suluhisho maana serikali ina depend sana kwenye makanisa angalieni shule, hospital kubwa zinahudumiwa na makanisa na wapa tu mifano michache (paramiho hospital, bugando hospital, etc.) na kuna shule nyingi tu ambazo zinaubora wa hali ya juu sana kuliko hata za serikali na ndio zinaiweka tanzania mahali pazuri kielimu na hata kimataifa kwenye nyaja za elimu
 
Mgonjwa hatibiwi kwa kunyongwa bali kudungwa sindano kwa dawa stahiki. Hawa wafanya fujo wanatakiwa wakubane na mkono wa sheria bila huruma.

Waisamu walipewa Majengo ya Tanesco bure waanzishe chuo kikuu yaani hawawezi chochote zaidi ya kelele lakini hakuna hata Kanisa moja hapa bongo limepewa na serikali jengo hata moja. Hawa hata ukiwapa LIBUGANDO lote wataliua shule ndogo kelele nyingi.

Sasa hivi viongozi wa juu wote Bongo Waislamu bado wanaona mfumo kiristo hahahhaaaa wagonjwa wapewe dawa mkuu
 
Concrete

Hivi unajua ni asilimia ngapi ya madaktari unaowaona wewe katika hizo hospitali ni madaktari wa serekali na si wakanisa..au unaropoka tu....fanya utafiti wa kina.

Haiwezekani madaktari bingwa wa serikali wapelekwe Ifakara, Bugando na kwingineko then unasema kanisa linajitegemea wakati wanatumia watumishi wa umma.

Acheni maneno ya kijiweni. Mchnagia mada yupo sahii ila hakunyambulisha katika swala la Afya ndhani anadhania hospitali ni jengo tu. Na hajui kuna maelewano gani kati ya serekari kupitia wizara ya afya na makanisa katika upatikanaji wa watumishi wa uma kwenye makanisa hayo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Sikonge hawa mashehe wanaoipigia MOU kelele wanaishi mjini ama sehem za pwani ambapo waislam wapo kibao na hospital zimejaa tele. Ila kama wangekuwa wanaishi vijijini ambapo kuna hospital za wakatoliki tu wasingethubutu kuropoka ropka na kulalama kuhusu MOU.
 
Last edited by a moderator:
Kama mtakumbuka hotuba ya Raisi JK kwenye baraza kuu la Idd lililofanyika kule Dodoma kwenye msikiti wa Gadafi, Raisi alijibu malalamiko ya waislamu kuhusu MOU kama ifuatavyo: "tulitoa fursa hii kwa watu wa dini zote, lakini waislamu hamkutaka kuitumia fursa hii, badala yake mnazuia wenzenu kuitumia fursa hii..."

Je ni wivu, roho mbaya au ni nini? Kama serikali ilitoa fursa hiyo kwa dini zote kwa nini waislamu hamkiutaka kuichangamkia na badala yake mnazuia wenzenu wasiitumie?
 
Nimejaribu kupitia mijadala mbalimbali humu jamvini nimegundua kuwa kuna kundi kubwa la member wamejaribu ujinga baada ya kuona elimu ni ghari ama kwa kuambiwa au kwa kujaribu na kushindwa.

Kuna watu wanazungumzia MOU na Makanisa lakini sijawahi kusikia MOU na Taasisi za Kislam kama AGHAKAN na Ahamadia iwe Hospitali au mashule waliongia mikataba na serikali hata siku moja wanaowatuma hawaambii kuwa nao katika taasisi zao nao wana MOU jiulize kwa nini???? Ni ujinga

Vijana wengi ama hawajaenda shule kwa walio wengi au shule kwao imekuwa ngumu kwa hari ya kawaida sio rahisi kwa mfanyakazi anae jua umuhimu wa kazi afunge biashara yake au aache kwenda kazini akachome au akaandamane kwa ujinga ujinga.
 
Sikonge naomba unijibu haya maswali:

Je, ulishawahi kuusoma huo mkataba kati ya serikali na MOU?

Na jibu kama ni ndiyo je kuna kipengele kinachozuia taasisi nyinyine za kidini kama za kiislam nazo kuingia mkataba na serikali kwa shughul za kijamii?

Please naomba unijibu with facts
 
Last edited by a moderator:
Africa_Spring

Serikali inapeleka madaktari na kuwalipa ili kupunguza gharama za matibabu watanzania wote waweze kutibiwa, wakiacha tutaongeza gharama za matibabu kama Aga Khan halafu tuone utatibiwa wapi
 
Last edited by a moderator:
Waisamu walipewa Majengo ya Tanesco bure waanzishe chuo kikuu yaani hawawezi chochote zaidi ya kelele lakini hakuna hata Kanisa moja hapa bongo limepewa na serikali jengo hata moja.
Usiende huko!
Mahospitali,Makanisa,Shule vilivyojengwa na Mkoloni kwa hela ya Watanganyika wa dini zote viliachiwa Wakristo waendelee kuvimiliki baada ya Uhuru, Nyerere aliona mbali kuwa baadaye watu watakuja kuhoji hili hivyo akaleta ubabaishaji wa kujifanya kuvitaifisha baadaye kumuachia mwingine avirudishe!

MoU, Necta, Muungano ni vitu ambavyo Wakristo hawatokubali kwa gharama yoyote ile viingiliwe kwa sababu ndiyo mihimili yenyewe ya Mfumo Kristo

Kulijuwa hili ninalolisema angalia mtaharuki uliowapata wachangiaji hapa kuhusu hoja ya Kanisa kuvunja MoU na Serikali.
 
Kwani MOU ni nini? Na kama ushajua ni nini, Je, Waislam wanakatazwa kuwa na MOU na serikari kwa vitu kama Hospitals na vitu vingine wanavyoweza kuvifanya kwa ubia na serikali?

Maana ya PPP ni nini? Ina maana hiyo PPP inaruhusiwa kwa watu wengine na si Makanisa? Hospital zilipe kodi? Tangu lini vifaa vya hospital vikalipiwa kodi?
 
Wakristo kwa mtazamo wako wewe wamesoma na wanamaendeleo sana, inakuwaje wanahubiriwa kwenye makanisa yao wanayoyaita ya kiroho kuwachukia waislam? Kudharau waislamu, hilo nalo utalirekebisha vipi? Mimi ni mkristo sio mlokole.
Kama una ushahidi wa kanisa lolote la kikikristo linalo hubiri chuki dhidi ya waislamu au liliwahi kuhubiri chuki dhidi ya waislamu ulete hapa na pengine wapeleke kabisa mahakamani.

Nijuavyo mimi wakristo wanaamini siyo tu kupendana wao kwa wao bali pia kuwapenda watu wengine kama waislamu na wasio na dini; kwani wakipendana wao kwa wao hawatakuwa tofauti na wezi, majambazi na watenda dhambi wengine kwani wao hupendana wenyewe kwa wenyewe.

MUNGU WETU NI YULEYULE ALIYE UMBA MBINGU NA DUNIA.
 
Back
Top Bottom