Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Tuletee wewe taarifa za uthibitisho ambae umeshafanya uchunguzi,hivi kila mtu akichunguza itakuwaje?
Sikonge amka kumekucha sasa,

Fanya uchunguzi utagundua kwamba Dunia nzima inaendeshwa kwa mfumo Katoliki wala si Kristo is just Catholic. Rudi uliza wana sheria watakueleza vyema uwezo wa Canon Law ulivyopenya kote.

Halafu MoU ile is jusy PPP amka cha kulialia wewe
 
Mkuu Sikonge una pointi nzuri sana na zinatufaa sisi watanzania wa leo.

TATIZO LILOPO KWENYE MAADA YAKO.

1. UMEWEKA MBELE SERA YA UDINI (UISLAMA & UKRISTO0
2. UMESHINDWA KUTOA MCHANGANUO WA HOSPITALI ZIPI ZA KIKRISTO ZNAWATOZA WAISLAMI GHARAMA KUBWA ZA MATIBABU.
3. UJUE SERIKALI YETU HAINA DINI KATIKA KUONGOZA NCHI, LAKINI WANANCHI WAKE WANAUHURU WA KUABUDU DHEHEBU LOLOTE.

Nakuomba ndugu yangu mtanzania mwenzangu, sio kila unaloambiwa "USEME NDIO"!! Acha kuwahadaa watanzania wenzako.
 
Last edited by a moderator:
Kutokana na kulalamikiwa saana na Waislaam kuwa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Makanisa (MOU) yanafanya nchi hii iwe na "Mfumo Kristo" na hivyo kuwanyanyasa Waislaam na hata kuwatawala, inabidi ifike wakati Makanisa yaanze kufikiria jinsi ya kuvunja mkataba huo na kurudi kama ilivyokuwa zamani.

Kwa sababu hili swala limeonakana likichochea sana vurugu, mie napendekeza lifuatalo:

- Wavunje mkataba wa MOU na Serikali.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mahospital ya Kanisa.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mashule ya Kanisa nk.

-Makanisa na vitengo vyake, viwe vinalipa kodi kwa kufanya biashara ya Hospitals, Shule nk.

-Gharama kwa walio Wakristo, ziwe zinapunguzwa kwa wingi kwa sababu wao hutoa michango mingi tu ya kuendeleza kanisa na sadaka za kila Jumapili.

-Kwa wasio Wakristo na hapo wanapoishi hakuna hospital ya Serikali au ya dini yao, basi itabidi wailazimishe Serikali MPYA ya Tanzania ambayo haitakuwa na Mfumo Kristo tena ili wawajengee Hospitals za Serikali.

Kama Serikali ikishindwa basi wajiandae kulipa gharama kubwa kwenye huduma hizo za jamii au KUBADILI DINI. Kama siyo hilo basi na wao na dini zao wajenge hizo huduma za jamii ili kushindana na za Makanisa.

Nafikiri muda umefika wa kuonyesha kuwa Viongozi wa Makanisa ni Wasomi wa hali ya juu na siku zote "Akili kubwa hutawala akili ndogo......" Vinginevyo, akili zao zitakuwa kazi bure kama hawawezi kutatua matatizo yaliyowazunguka.

Kama kuna kundi jingine au Serikali litakuja na mbinu mbadala na kuweka huduma hizi za jamii katika bei nafuu zaidi, basi ina maana huduma za jamii kutoka kwenye Makanisa tutakuwa hatuhitaji tena. Maendeleo yanakuja kwa mashindano. Muda umefika Makanisa kutangaza mashindano kwa kutoa huduma za JAMII VS dini nyingine au Serikali.
--
Thubutu waondoe MOU uone kama zitajiendesha wanashindwa hata kufanya baadhi ya surgery sometimes kwasababu tu serikali haijapeleka fungu la MOU kwa ajili ya malipo ya wafanyakazi na ununuaji wa gas.Kama wangekuwa hawafaidiki wala wasingesaini MOU.Kwani kwenye hizo huduma za jamii pamoja na serikali kuwekeza ni wapi umeambiwa makanisa wanatoa huduma hizo bure au kwa bei nafuu?
 
Nadhani amelala huyo! Hajui kwamba KCMC, Bugando ambazo ni hosp kubwa nchini zinatoa msaada tu! Mbona viwanja vipo kwanini sisi Waislam tusifunguke? Tuna Morogoro University, hivi tumefanya nini cha maana tangu Mzee wetu Mkapa atupatie yale majengo bure? HAdi leo hatjawahi kuyakarabati!
Hizo hospitali kubwa zote unazozitaja serikali ndiyo iliyozifikisha hapo zilipo na Mh. Rais Mstaafu Mkapa kutaka kuficha mabaya yake akaamua kuyapatia makanisa na awali zilitaifishwa na Mwalimu na zilipotaifishwa na kuchukuliwa na serikali zilikuwa ktk hali duni serikali ikafanya mabweresho na Mkapa akazirudisha kinyemela kutaka kuficha zile biashara alizokuwa anazifanya ikulu na kawaziba mdomo kina Kitwana Kondo akatoa majengo ya Tanesco kuwapa the so called muslim university!
 
Kanisa limewahi kuendesha mashule na mahospitali yake bila ya MOU ni busara sasa kanisa na hata taasisi za Aghakan foundation zijitoe kwenye mkataba huo kisha kanisa lifanye biashara ya shule na hosptali ambapo wale waliojenga mashule hayo na mahosptali wanaweza kupewa unafuu wa karo za shule na nafuu ya kulipia tiba.

Hofu yangu ni kwamba kwa kuwa nchi imeanza kuvurugika kidini kuna ishara kwamba baada MOU kuvunjika kanisa linaweza kutoa vitambulisho kwa waumini wake ili wasome kwa nafuu na kutibiwa kwa nafuu na wasio waumini wa kanisa watalipa gharama za juu.

Hii inawezekana kutokana na imani kwamba wakati huo fedha za sadaka, zaka, harambee, mavuno na minada ya kanisani itakuwa inaendesha huduma hizo na serikali haitakuwa na mkono wake katika huduma za kidini.
 
أنها وفرت لنا، ونحن نقدم ثيقة من وثائق اتحاد تنجانيقا وزنجبار

طجدفسجبفطجابدسنفطجابدفنس‎..باجطفبسنفطجابس‎..بفنس؟؟‎.‎
 
Wewe unatibiwa kwenye hospital zipi? Alafu mnavyoongea kana kwamba wakristo wao hawalipi kodi, mmepandikizwa chuki kiasi kwamba mnashindwa kujua madhara ya hizo chuki mwisho wake ni nini?

Je wale wapagani nao wadai chuo kama waislamu wakivyopewa majengo morogoro ya kodi za wananchi wote?
Je taasisi kama Aghakhani nazo zieekewe kodi?

Nakwambia ata wakitoa misamaha ya kodi hospital zitaendelea kuwepo na zitakuwa nzuri tu, kwani kuna hospital ngapi binafsi zilizopo na hazijafungwa, zinaendelea kulipa wafanyakazi wake?
Binafsi nafanya kazi hospital binafsi nalipwa mara 2.5 ya mshaara wa serikali na hapa vifaa vyote na madawa uwa hayalipiwi kodi,
 
Chanzo cha MOU ni wakati wa Utawala wa awamu ya pili kushindwa kutoa hudumu za shule na hospitali kwa wananchi wake ambao walikuwa wanaongezeka kwa kasi kuliko kukua kwa huduma za kijamii. Wazo hili lilikuwa jema lakini kama linatugawanya kidini misamaha yote ya kidini inaweza kufutwa na mikataba ya MOU kufutwa.

Hii haitaondoa malalamiko ya waislamu lakini kwa hoja hii moja ya misamaha ya kidini, MOU, Mahakama ya kadhi na OIC serikali itakuwa hailaumiwi. Jambo kubwa hapa ni kwamba baadhi wanatumia mashirikiano hayo kama njia ya kubagua kundi jingine ingawa kiukweli kundi linalolalamika halijanyimwa fursa hiyo ( rejea hotuba ya Rais KIKWETE) aliposema Waislamu hawajanyimwa bali hawajaomba MOU lakini kuna taasisi za kiislamu za Mabohora na Aghakan ziko kwenye MOU.
 
Kanisa limewahi kuendesha mashule na mahospitali yake bila ya MOU ni busara sasa kanisa na hata taasisi za Aghakan foundation zijitoe kwenye mkataba huo kisha kanisa lifanye biashara ya shule na hosptali ambapo wale waliojenga mashule hayo na mahosptali wanaweza kupewa unafuu wa karo za shule na nafuu ya kulipia tiba.

Hofu yangu ni kwamba kwa kuwa nchi imeanza kuvurugika kidini kuna ishara kwamba baada MOU kuvunjika kanisa linaweza kutoa vitambulisho kwa waumini wake ili wasome kwa nafuu na kutibiwa kwa nafuu na wasio waumini wa kanisa watalipa gharama za juu.

Hii inawezekana kutokana na imani kwamba wakati huo fedha za sadaka, zaka, harambee, mavuno na minada ya kanisani itakuwa inaendesha huduma hizo na serikali haitakuwa na mkono wake katika huduma za kidini.


HAPA TUTAJAZA WEZI MTAANI NA UCHOMAJI WA MASHULE UTARUDI TENA PALE PALE... tUWAPENDE TU JIRANI ZETU KAMA nAFSI ZETU...... WAONDOE mou YAO SIYE TUTAENDESHA HUDUMA ZETU KWA HELA ZETU NA PIA WAJE TU KUSOMA NA KUTIBIWA HUKU NDIKO TUTAKAKO VUA SAMAKI WENGI... NA KONDOO WA BWANA WATAONGEZEKA...
 
Napenda kuuunga mkono ila nashidwa kusema ndiyo,ila sijui umetazama kwa kigezo kipi hasa..sijui ulikwisha fika baadhi za wilaya au vijiji au mikoa,Serikali yako haina Hosp.zaidi ya Dispensary?na kuna sehemu nyingine kuna Dispensary za Makanisa kwenye vijiji kutokona na serekali yako kushidwa kupeleka hizo huduma za jamii?

Kwa ufupi kuna Hosp.Kama ya Bugando-Mwanza ,serikali iliichukua lakini ilishidwa kuiendesha na kuirudisha tena kwa Wakatoriki?Kodi zifutwe ndiyo ulikwisha fikiria juu ya Hizi hosp au hizi huduma wanazitoa wapi hizo pesa za kuendesha?kasome habari za Non-profit organization.Hosp.za rufaa wanatibu wagojwa wakristo tu au na waumini waimani nyingine?mbona hauzungumzi juu ya Agakhan Hosp.

Vyuo vinavyopata ruzuku vinafundisha wakistro pekee?mfano.St.Agustine,Tumaini,n.k?kuna waislam wangapi wamefanikiwa kupitia vyuo hivi?

Ngoja nikwambie kitu kuwekewa kodi au kufuta mikataba si solution ya matatizo ya waislam Tanzania..waislam wanamatatizo yao mengi..na wengi wanaolalamika elimu dunia hawana mbona sijawai kusikia Prof au DK. wa kiislam analalamika?kwani hawapo maprof.wakislam Tanzania?nenda UDSM au UDOM,kwani wao ndiyo hawana machungu na imani ya Kiislam?

Wikimaliza kupigana na makanisa watagundua adui yao ni ukristo bali adui yao ni wao wenyewe kisha wataanza kuchina wao kwa wao..
 
nani kasema nhif ni hosptl?
Nimesema watibiwe kwenye hosptl yoyote iwe binafsi au ya kanisa kwa kutumia bima kakini baada ya serekali kuvunja mou na kanisa.

Ni % ya watz wana uduma za bima ya afya? Tena ujue uduma za bima zinategemewa sana na watu walio kwenye ajira so% ngapi ni watu wenye ajira wanaoweza kuafford hiyo kitu? Pls usijibu tu kwasababu hauwapendi wakristo, ujue utaumiza wengi sana
 
kuendelea kung'ang'a MOU ni kama ukristo hauwezi kusonga mbele au kuwa na huduma bila MOU. Siamini kwamba bila MOU kila kitu kitasimama kwenye huduma za kanisa bali gharama zitapanda. Hofu yangu ni mashule na mahospitali kuwakataa watu wa dini nyingine kwa sababu ya mbegu ya ubaguzi inayopandwa sasa. Kwa mfano, mashule na mahospitali ya dini yatahusika na waumini wao tu.

Kwa upande wa shule waislamu wanaweza kudai kuwa shule za kanisa zina wanafunzi wengi wakristo lakini na wao kwa kuwa wana shule za waislamu wangeweza kuomba nafuu hiyo.

Kwa upande wa hospitali za kanisa sijui wagongwa wengi ni wa dini ya kikristo au kiislamu kwani ugonjwa ni majariwa ya Mungu, labda nako ugonjwa unawapendelea wakristo lakini kama Waislamu hawataki kuomba nafuu hii kwenye mahosptali yao na pia wanalalamika hosptali za kanisa zinazotibu watanzania wote kuondolewa nafuu hii hakuna budi kufuta MOU.
 
Mkuu Sikonge, ni kama vile ulikuwa kwenye mawazo yangu. Lakini je na makanisa hayo yatazizuia taasisi zake kutoa huduma za afya na elimu kwa watu wasiokuwa wa madhehebu yao?

Ni ukweli kabisa hilo litaondoa mzizi wa fitina, ila pia kutakuwepo na madhara yake mengi tu. Especially kama kuna watu wasiokuwa wa madhehebu hayo ambao bado walikuwa wakipata unafuu wa huduma hizo kutokana na msaada mmoja wa serikali kwenye uchangiaji wa kuendesha huduma hizo.

Hatahivyo bottomline nakubaliana na wewe.

Mkuu hawa watu hiyo MOU ni kisingizio tu... kifupi hawajui hata kwa nini wanalalamika, Most of them are looking for shortcuts in life.. Angalia wanaoleta fujo ni wapuuzi fulani tu wanaoshinda vijiweni na kufikiria dini zingine ndio zinawafanya waishi kwenye mbavu za mbwa na kula mlo mmoja kwa siku.. Wanafikiri MOU ndio inajenga makanisa,shule,vyuo na mahospitali.. they are very stupid ukienda msikiti wa sinza pale sadaka wanayotoa sidhani hata kama inazidi 50k kwa week lakini ukienda kanisa la RC sinza au KKKT sadaka utakuata ni more than 5m kwa week, halafu bado wanafikiri MOU inasaidia kanisa, Kwa Taarifa yao ni kwamba kanisa linaweza kuendelea maradufu hata zaidi ya sasa bila hiyo "MOU" Ukimuuliza Muislamu anayekaa kule Kiteto au Bumbuli umuhimu wa MOU atakwambia iboreshwe zaidi na ziadi ila ukiuliza hawa wacheza bao na zuna wa magomeni, tandika na Ilala watakwambia inakandamiza uislam as if wao wanakatazwa kuitumia hiyo MOU...
 
Mada hii nzuri sana lakini kwa leo nawasikiliza nyinyi wakubwa. Jadilini yote. Kama ni elimu basi napenda mfananishe elimu ya vyuo vikuu kati ya Oman nchi tajiri au Kuwait na Norway au sweden. Kwa sababu hizi zote ni nchi tajiri na pia nyingine za waislamu na nyingine za Wakristo,Na kama mtapata nchi ambazo ziko nyuma mjadili pia sababu ya nchi hizo kuwa nyuma kama ni mou au la.Tukitoka hapo tujadili elimu kati ya somalia na Namibia au zambia.Hiyo iwe comparative analysis. Chonde chonde msiniingize katika mjadala huo, Naogopa sana Bokoharamu, MRC,alqaeda,Hamas na Alshabab.Mimi simo nimejitoa kabisa.
 
Wapo wanaoamini kwamba Islamic Banking account ziondolewe kwenye benki za wateja wa dini zote kwa sababu benki hizo sio za dini moja kama kule NBC, Stanmbic na Standard chartered ( hii huduma pia ni mkataba (MOU) kati ya waislamu na bank hizo). wengi tunasahau kwamba huduma ya benki sio ya kidini kama ilivyo MOU ya kanisa na serikali.

Kuna wanaoona kwamba shule na hospitali za dini zibaki kutoa elimu na tiba kwa waumini wake kwa kuwa fedha za kuendesha mashule na mahospitali zitakuwa za waumini wa dini moja.

Serikali ni chombo cha wote (haina dini) kama kuna wenzio hataki taasisi za dini zote kupata nafuu ya kodi wala hataki kuomba nafuu ya MOU ni jambo jema kwani tumesema serikali haina dini.

Hapa haijalishi MOU ina faida au haina faida wananchi wanapolalamika na kutaka kuingia vitani kwa hoja inayoepukika ni kukosa busara.
 
MoU kati ya kanisa katoiki na serikali ni utekelezwaji wa dhana ya public-private partnership(ppp) ambayo inafanyika duniani kote kwa sasa. dhana ya ppp inaruhusu sector binafsi (kanisa na misikiti vikiwamo) kutoa huduma za kijamii, na serikali husika kusaidia taasisi hizo binafsi kutekeleza azma zake(kutoa huduma).kwa mfano serikali ya tz inazisaidia baadhi ya hospitali binafsi kama CCRBT,KCMC,(zinazomilikiwa na taasisi za kidini na taasisi zisizo za kidini). changamoto iliyopo kwa waislam ni kujenga hospitali na shule zao na kuiomba serikali iwasaidie kwa kiwango fulani kuziendesha, kama wakristo walivyofaya. kulalamika au kutaka serikali ijitoe kusaidia taasisi hizi si suluhisho, isipokua ni kuwaumiza raia wa dini zote kwa kua serikali pekeyake haiwezi kutoa huduma hizo.
 
Kanisa haliwezi, na halitaweza kujiendesha bila kubebwa na serikali, Just for your information, sasa hivi hadi posho za madaktari serikali inagharamia tofauti na zamani ambapo posho zilitoka mahospitalini.
 
Back
Top Bottom