-Kwa wasio Wakristo na hapo wanapoishi hakuna hospital ya Serikali au ya dini yao, basi itabidi wailazimishe Serikali MPYA ya Tanzania ambayo haitakuwa na Mfumo Kristo tena ili wawajengee Hospitals za Serikali.
Kama Serikali ikishindwa basi wajiandae kulipa gharama kubwa kwenye huduma hizo za jamii au KUBADILI DINI. Kama siyo hilo basi na wao na dini zao wajenge hizo huduma za jamii ili kushindana na za Makanisa.
Nafikiri muda umefika wa kuonyesha kuwa Viongozi wa Makanisa ni Wasomi wa hali ya juu na siku zote "Akili kubwa hutawala akili ndogo......" Vinginevyo, akili zao zitakuwa kazi bure kama hawawezi kutatua matatizo yaliyowazunguka.
Lengo la Ukristo si nani mwenzetu, bali ukristo unajukumu kubwa la kulinda uhai wa kila mwanadamu katika dunia hii bila kujali imani yake, dini, elimu rangi, jinsia wala taifa.
And hence, hayapo tayari kuona utu wa mtu ukidharirishwa kwa kukosa elimu, maarifa, huduma za afya n.k na hapo ndipo ulipo msingi wa huduma za kiroho kwa jamii.
Kwa namna ulivyoyaanika hayo mawazo yako umepita picha ni kipi kitatokea pale Sikonge? Mazinge Hospital (District Hospital) imeshamalizwa kujengwa na kuanza kazi lakini inasuasua, hakuna hata huduma moja ya upasuaji inayofanyika pale wa ya kulaza wagonjwa kuna ward lakini ni makazi ya vumbi, koboko na ndege. Huduma za kulaza wagonjwa na upasuaji zote zinafanyika Sikonge District Designated Hospital(DDH) now CDH (Council Designated Hospital).
Na hospital hiyo ya Mission kila mwaka huleta flying Doctors kwa ajili ya kuendesha upasuaji mdogo kwa wananchi wa pale ambao hutangaziwa in Advancea, Ndala Hospita iliyopo Wilayani Nzega nayo I hope unaielewa vizuri coverage yake, Pia kuna Nkinga Hospital iliyopo Wilayani Igunga ambayo kwa sasa ni Referal Hospital pekee katika mikoa ya kanda ile. Sina wasiwasi na Hospitals za Makanisa yaliyopo Tukuyu na mkoani Mbeya kwa ujumla sababu majority wata qualify kwa huduma hizo...lakini hiyo minority bado ni pigo kubwa sana tunapoongelea uhai wa mwanadamu.
Think again....do you real mean Bugando ikate huduma kwa wakazi wa Mwanza kwa kigezo cha Imani? Unadhani kanisa limejipa mamlaka na uwezo wa kutambua ni yupo muumini wa kweli and who is faking? Hilo ni jukumu la Mungu pekee, wajibu wa kanisa ni kustawisha maisha ya mwanadamu popote alipo, kuhakikisha utu wa mtu unaheshimiwa.
And hence, kanisa halipo tayari kuona utu wa mtu unadharirishwa kwa kukosa elimu, maarifa, huduma za afya n.k.