Mkandara, naamini wewe ni msomi na una uelewa mkubwa sana kuliko wenzako walio wengi ambao wanaandamana bila hata kujua ni kwanini wanaandamana. Naamini unajua wazi kabisa kwamba serikali haina uwezo wa kutoa huduma zote za jamii kwa watu wote, pia unajua wazi kabisa kwamba waislam hawajawekeza vya kutosha kwenye suala zima la huduma za jamii. Hivi kama leo hii itatokea MOU ivunjwe, na wakrito wakasema tutatoa huduma kwa watu wetu tu kwa kuwa wao wanachangia sadaka, unafikiri waislamu wataenda wapi? Na niambie umoja wa taifa utajengwa vipi kama huduma za jamii zitatolewa kwa udini? Kumbukeni kwamba sehemu nyingi za vijijini ambako kuna wakristo na waislam huduma nyingi za kijamii kama maji na afya zinatolewa na mashirika ya kidini?
Kule kijijini kwetu kanisa la Anglikana limegawa ng'ombe wa maziwa kwa akina mama wa dini zote waislam na wakristo bila ya ubaguzi wowote, na hivi sasa wakina mama wale wanaweza kusomesha watoto na wanajikwamua kutokana na umaskini. Hivi kanisa lile lingeleta udini, hali ingekuwaje kwa waislam? Hata rais wenu amesoma shule za misheni, kama kusingekuwa na huu utaratibu waislam wangesoma wapi jamani na hali shule hamjengi? Sasa hivi ukienda peramiho au KCMC unapata huduma kama mtanzania na si kama Muislam au Mkristo, na unapata huduma yenye ubora sawasawa, sasa kinachowauma ni nini?
Nakuhakikishia Mkandara wanaoongea maneno ya hovyohovyo namna hii na kuupotosha umma ni watu ambao hawajaenda shule. Na ni fedheha kwako kufuata maneno haya ya wakosaji. Maana mkataba mnaoulalamikia si wa wakristo na serikali tu bali ni wa serikali na mashirika ya dini yakiwemo ya waislamu. Tatizo ni tu kwamba shule zenu wanasoma waislamu tu. Hiyo ndo tabu yenu. Lakini najiuliza kama mikataba hii ya serikali kuchangia gharama za kuendesha huduma za jamii zinazotolewa na mashirika ya kidini itafutwa, ninyi mashirika yenu mtaendeshaje na hivi mnategemea misaada kwa kila kitu?