pole mama,sali nyumbani Mwenyezi MUNGU yupo popote sio kanisani tu,hao Wakatoliki,Walutheri,Waangrikani etc etc ambayo ndio makanisa mama our no 1 anaombewa tena kwa SALA kuu (real!!!) .....utusamehe makosa yetu KAMA SISI tunavyowasamehe WALIOTUKOSEA ,huku ni kumdhihaki Mungu,wakitoka hapo wanatoa amri za ajabu,piga yule,ua yule,weka ndani yule etc etc ,next sunday kanisani tena,....please give me a breakUmetoka nyumbani unaamua kuingia kanisani japo kupunguza stress za ugumu wa maisha na matatizo mbalimbali lakini humo kanisani unakutana na michango isiyoisha tena kwa lazima.
Nijuavyo mimi sadaka ni kile ambacho mtu amejaaliwa kukipata
Sasa eti kuna makanisa mpaka wameweka viwango sadaka isiwe chini ya kiasi flani, bado shukrani, bado fungu la 10, bado sadaka ya utumishi, bado sadaka ya madhabahu, bado sadaka ya malimbuko sijui nini. !
Mbaya zaidi kila mahubiri ni kusisitiza utoaji sadaka na michango tu.
Sio siri makanisa yetu mnakatisha tamaa kabisa ukute mtu ni mama wa nyumbani atapataje pesa yote hiyo kama sio mwanzo wa kugombana na mmewe.
Mungu atusaidie.
Askofu anatembelea v8 na ana mjengo mkali huko mtaani,wewe muumini uko na baiskeli yako mtaani na bado unatamba,hahahKWANI TUNATIBIWA BURE? KWANI SHULE ZAO TUNASOMA BURE? KWA TAARIFA YAKO VITEGA UCHUMI VYAO TUNAJENGA SISI THEN TUNALIPISHWA SISI TENA KWA BEI KUBWA ZAIDI BILA KUJALI MICHANGO YETU. TUMIA KICHWA CHAKO VZURI KUFIKIRI
Au peleka sadaka kwa watu wenye mahitaji maalumu; Wazee, Watoto; Wagonjwa, Wenye baa la njaa etl ; Ukifanya hivi hata bila ya kwenda kanisani au msikitini utapa baraka.Sadaka nitatoa mwenyewe kwa jambo ninaloona mwenyewe linafaa.
Nenda kasali mahali ambapo moyo wako unakuwa na amani...Kulalamika huko inaonesha ulipo si mahala sahihi au tatizo ni wewe mwenyewe!
Si sawa wala sahihi kusema "makanisa ya kiroho" kwa ujumla wake, be specific na mpe Mungu Utukufu!
Be blessed!
kanisa zuri ni lile ambalo liko KITAASISI kama LUTHERAN, MORAVIAN, KATHOLIC, SABATO, MAKANISA YA KIROHO (EAGT,n.k) tatizo ni zile huduma za ''kanisa la fulani'' huku ndo kuna ile inaitwa '' watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa''. huku kwa kweli mnapigwa. yaani sio siri hasa kina mama na kina dada, huku mnpigwa. WAJINGA NDO waliwao.
mimi nna shemeji yangu alikuwa anafanya biashara ya mchele Mwanjelwa, akaacha kahamia kwa mchungagaji, yaani mpaka kapoteza muelekeo wa maisha, ila tunashukuru MUNGU juzi , amerudi kwenye shughuli yake na anaendelea na kusali
Kitu huwa kinanishangaza kuhusu hizi sadaka
Yaani unaenda kabisani unatoa michango ya lazima lakini ukiwa umekaa mahali na watu anakuja maskini ambaye unamuona hali yake ni ngumu, humpi hata 200
Au umekaa unakula hotel unashindwa kumpa maskini aliekaa nje sahani ya wali
Ni uungwana au unafiki wa kijionesha
Halafu isitoshe sijawahi kuona mkiambiwa jamani leo tunaenda kuwapa msaada katika michango yenu vipofu au Yatima
Mungu anawaona wachangishaji wanaojilimbikizia hela zenu na nyie mnaowatajirisha wakati jirani yako analala njaa
Shame
ulivyooandika , kwanza naona wazi hupendi UKWELI, na UNA TATIZO, nina hakika mimi naheshimu kanisa kama TAASISI, naamini MAKANISA YA KIROHO (na nayaheshimu) SABATO , CATHOLIC, Moravian N.K , Sasa wewe kusema yamekufa, tayari naona UNA TATIZO la kujihesabia HAKI, NA KUJIONA UMEFIKA MBINGUNI NA HAO WA MAKANISA NILIYOYATAJA WAMEKUFA. HongeraKaribia yote uliyoyataja hapo ni makanisa yaliokufa,inawezekana hata wewe umeshakufa kiroho ndio maana unapenda vitu vilivyokufa.Mimi niko hai,mimi ni simba napenda vitu vilivyo hai,vitu moto.Hizo dini hapo namwachia babu yangu.
Sifa kuu ya muumini siyo kutoa sadaka bali ni kuzishika Amri za MUNGU na imani ya YESU KRISTO. YESU KRISTO alisema hivi; "enendeni mkajifunze maana ya maneno haya, sitaki sadaka nataka rehema".Sifa Kuu Ya Mshirika/muumini Ni Utoaji Sadaka.