Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

Umetoka nyumbani unaamua kuingia kanisani japo kupunguza stress za ugumu wa maisha na matatizo mbalimbali lakini humo kanisani unakutana na michango isiyoisha tena kwa lazima.
Nijuavyo mimi sadaka ni kile ambacho mtu amejaaliwa kukipata
Sasa eti kuna makanisa mpaka wameweka viwango sadaka isiwe chini ya kiasi flani, bado shukrani, bado fungu la 10, bado sadaka ya utumishi, bado sadaka ya madhabahu, bado sadaka ya malimbuko sijui nini. !
Mbaya zaidi kila mahubiri ni kusisitiza utoaji sadaka na michango tu.
Sio siri makanisa yetu mnakatisha tamaa kabisa ukute mtu ni mama wa nyumbani atapataje pesa yote hiyo kama sio mwanzo wa kugombana na mmewe.
Mungu atusaidie.
Ha ha ha haaa! Kuna kanisa moja hapa Mbeya siku moja wakati ibada inaendelea mchungaji akasema "kila muumini mwenye shilingi 10,000 mfukoni asimame" wakasimama (si mnajua tena ukikauka mchungaji anadai hiyo elf 10 Mungu anaiona, ha ha ha). Basi wasijue hili wala lile wakiwa wamesimama wakaambiwa waende mbele. Kikapu kikasogezwa ili waweke hiyo 10,000 walipoweka wakaambiwa waende kwa amani Mungu arawaongezea! Sasa je huo sio wizi? Yaani watu waliharibiwa bajeti zao vibaya mno. Nasikia walishaanza kulihama kanisa hilo.
 
Umetoka nyumbani unaamua kuingia kanisani japo kupunguza stress za ugumu wa maisha na matatizo mbalimbali lakini humo kanisani unakutana na michango isiyoisha tena kwa lazima.
Nijuavyo mimi sadaka ni kile ambacho mtu amejaaliwa kukipata
Sasa eti kuna makanisa mpaka wameweka viwango sadaka isiwe chini ya kiasi flani, bado shukrani, bado fungu la 10, bado sadaka ya utumishi, bado sadaka ya madhabahu, bado sadaka ya malimbuko sijui nini. !
Mbaya zaidi kila mahubiri ni kusisitiza utoaji sadaka na michango tu.
Sio siri makanisa yetu mnakatisha tamaa kabisa ukute mtu ni mama wa nyumbani atapataje pesa yote hiyo kama sio mwanzo wa kugombana na mmewe.
Mungu atusaidie.
Mbona Kwa waganga mnapeleka mbuzi, kuku na vitu vingine. Lazima mmpeleke
 
Hayo makanisa ni miradi ya watu inayowaingizia pesa mingi sana... Ukiachana huo mlolongo wa sadaka hakuna Huduma inatolewa bure
Mi nashangaa unakuta mnachangishwa hela kibao kujenga hospital. And then after that hakuna hata ahueni kwa mliochanga. Mnapigwa vilevile tu kwa gharama kubwa sasa si bora zile hela zangu ningeweka zinisaidie baadae
 
Mbona kwa waganga kienyeji mnatoa sadaka why kanisani iwe shida. Nina mashaka na imani yako
 
Wewe sio mkatoliki ndo maana sitokujibu swali lako
ACHA UPIMBI WEWE, WEWE UNAJIONA MKATOLIIIKI? HAKUNA MKATOLIKI ZAIDI YA PAPA NA BADO ANAENDELEA KUKOSOA BAADHI YA MAMBO SO UKATOLIKI UTAENDELEA KUKOSOLEWA TUU
 
Mbona kwa waganga kienyeji mnatoa sadaka why kanisani iwe shida. Nina mashaka na imani yako

Wapuuzi hawa,mimi nitatoa kwa Mungu kwa nguvu zangu zote,nikikaa na mchungaji kama haongei mabo ya kumtolea Mungu naondoka.

Kutoa kwa Mungu inalipa sana
 
Hamna neno la Mungu hapo,umechukua maandiko na kutafsiri kutokana na akili yako isiyo na nuru na kuliita eti NENO la Mungu,kawadanganye wengine huko,nyie ndio manabii wa uwongo.popote pale ukisikia au kusoma kuhusu nabii wa uongo ujue ni wewe,hivyo unabidi utubu ili uweze kuondokana na hizo roho zidanganyazo.
Hebu wewe ambaye ni Nabii wa kweli nifafanulie haya maandiko ambayo niliandika kwenye comment yangu; MATHAYO 25:31-40, YAKOBO 1:27, MATHAYO 9:13.
Na kisha uniambie dhambi yangu ni nini hata useme nitubu, nikiijua dhambi yangu hakika nitatubu. Nasubiri ufafanuzi wa hayo maandiko. Na ukishindwa kunifafanulia basi wewe ndiye Shetani Ibilisi unayewadanganya watu, wewe ndiwe utapaswa kutubu ikiwa utashindwa kuniambia maana ya maneno hayo.
 
Acha yani kama wakiendaga kwenye semina wanafundshwa mbinu za kutufanya tutoe jamani khaaa!
 
Kumbe siku hizi bado kuna sadaka!? Nijuavyo mimi huwa hatutoi sadaka bali tunatoa michango.
 
Mimi nilishaachana na hizo habari kitambo sana tu.

Sadaka nitatoa mwenyewe kwa jambo ninaloona mwenyewe linafaa.

Nilikuwa nasikiliza BBC World Service kama kawaida yangu, wakawa wanaongelea habari mpya nilikuwa sijawahi kuisikia.

Kawaida huwa kuna watu wanapenda kuwa dominated katika mahusiano, wanapenda kuna na ma "dominatrix", usually it is about the use of force and humiliation.

Sasa siku hizi kuna mpaka ma "financial dominatrix", kwa mfano mwanamke ana m control mwanamme anam dominate mpaka kwenye mambo ya fedha, mwanamme anampa pesa zake zote mwanamke (wengine mtasema mganga wake mzuri huyo mwanamke, lakini hamna uganga hapo)

Ulivyosema hiyo habari, nikakumbuka hawa "dominatrix", hao Wachungaji nao wanaweza kuwa katika kundi moja na ma"financial dominatrix".

The Wwashington Post did an article on this.

- The Washington Post

Meet the dominatrixes who control men where it really hurts: Their wallets

In a pastel-colored French patisserie in Beverly Hills, Mistress Harley sips on a Bellini topped with raspberries and scrolls through surveillance monitors on her Android. “Oh, look, there’s Ben!” she says, tapping on the screen with her long magenta nails. “He’s naked.”

Speaking into the microphone on the app Nest, which is usually used for things like home security and pet monitoring, Mistress Harley instructs the man to kneel on the floor and bow down to her. He obeys. “You can see that I’ve made him sell all his stuff and even his bed, so he sleeps on the floor,” Mistress Harley explains. “He lives in Sacramento. I’ve actually been considering buying a house in Sacramento and making him rent it from me.”

Mistress Harley — who, like many in this article, refuses to reveal her legal name citing privacy and safety concerns — isn’t forcing Ben to do anything he doesn’t want to do. He is paying her a weekly salary to monitor him throughout the day. Sometimes she likes to cackle at him in the middle of the night via speakers installed in his bedroom. Other times, she’ll demand that he eat only meals that resemble dog food and send her photos as proof.

Read more here - - The Washington Post

Kumbe uliisikiliza ile makala? Kwamba mtu anaweza kufanyia ukandamizaji au unyanyasaji (nimekosa neno zuri la kiswahili) hadi huyo anaefanyiwa ukatili anampenda mtesi wake.
 
niliacha kwenda makanisa ya kifedha mwaka 2010 baada ya kuchangia kama million moja hivi ndani ya mwezi mmoja na kubwa zaidi mwezi unaofuata tukaambiwa tuchangie fedha kununua gari la mchungaji na ujenzi wa nyumba yake nikaona isiwe shida, nikajivua ulokole mpaka leo, kanisa lipo morogoro kwa mchungaji john lukindo, ibada tulikuwa tunafanyia pale bene kwenye ukumbi wa kukodi, kanisa hakuna et tuanze kununua gari ya mchungaji badala ya uwanja wa kanisa, nikahisi humu hakuna MUNGU
Hizo ni changizo hata usipotoa si dhambi wala huendi Motoni. Ila ukiona Kanisa linakwambia halina habari ya zaka au sadaka achana nao hawana nia nzuri na wewe. Zaka na sadaka ni utaratibu wa Mungu.
 
Kumbe uliisikiliza ile makala? Kwamba mtu anaweza kufanyia ukandamizaji au unyanyasaji (nimekosa neno zuri la kiswahili) hati huyo anaefanyiwa ukatili anampenda mtesi wake.
Hayo ni mambo yapo siku nyingi.

Nilichokuwa sijui ni hii asoectvya "financial dominatrix".

Mwanamke anakufunga kamba, anakuchapa fimbo, anakutukana, halafu anakwambia umoe hela zako zote zilizo benki. Unampa.

Kukudhalilisha hivyo ndiyo furaha yako.

Utajiri nao una matatizo yake tofauti na ya umasikini.
 
Kwani unasachiwa ukiamua kutotoa kabisa utafukuzwa kwenye ibada?
 
Hebu wewe ambaye ni Nabii wa kweli nifafanulie haya maandiko ambayo niliandika kwenye comment yangu; MATHAYO 25:31-40, YAKOBO 1:27, MATHAYO 9:13.
Na kisha uniambie dhambi yangu ni nini hata useme nitubu, nikiijua dhambi yangu hakika nitatubu. Nasubiri ufafanuzi wa hayo maandiko. Na ukishindwa kunifafanulia basi wewe ndiye Shetani Ibilisi unayewadanganya watu, wewe ndiwe utapaswa kutubu ikiwa utashindwa kuniambia maana ya maneno hayo.

Mathayo 12:39 "Yesu akajibu ,akawaambia,kizazi kiovu na cha zinaa,chatafuta ishara wala hakitapewa ishara,ila ishara ya Yona"

Sitakujibu kwasababu wewe ni kizazi kiovu na cha zinana! Unayesema hakuna haja ya watu kumtolea Mungu wala kwa kazi ya Mungu.Tubu upesi.

Mathayo 3:7... Enyi wazao wa nyoka,ni nani aliyewaonya kuikimbia hasira inayokuja?Basi zaeni matunda yapasayo toba.Wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba tunaye baba ....

Na shoka limekwisha kuwekwa penye mti,basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

Kazi kwako kama utaendelea kukumbalia hizo roho zidanganyazo au utaamua kutubu,nakushauri utubu na uanze kumtolea Mungu na kusimama na kazi yake.
 
Mi nashangaa unakuta mnachangishwa hela kibao kujenga hospital. And then after that hakuna hata ahueni kwa mliochanga. Mnapigwa vilevile tu kwa gharama kubwa sasa si bora zile hela zangu ningeweka zinisaidie baadae
.
Screenshot_20180723-143439.jpg
 
Back
Top Bottom