Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

Ila Sadaka ndio kanisa lenyewe na kanisa bila sadaka sio kanisa,cha muhimu kujua ni je ile sadaka unapoitoa inafanya nini pale kanisani,ukishajua madhumuni ya ile sadaka utatoa tu..
 
Mtoa mada ulikwenda kanisani kupunguza stress!!! Yaan kanisani unaenda kupunguza stress!!! Asee ndo nmesikia leo huo msemo, anyway ngoja nije kwnye mada! Sadaka ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mwamini huwezi kuinuliwa na Mungu pasipo sadaka, wewe unalalamika sadaka ni nyingi lakni ukwl ni kwmba kwa makanisa ya kiroho hakuna kiwango cha sadaka ila wakat mwngne kanisa huwa linaazimia kufanya jambo flan hapo ndipo waumini hushirikishwa na kuombwa mawazo ndo unakuta washirika hujadili na kiwango kupendekezwa sasa mtu kama ww uliienda kutoa stress ulipofika ukakutana na kiwango flan ukahisi ndo mchungaji kapanga kumbe wenzio walishajadili siku nyingi na kupitisha.... Lakini kwa mtu kama wewe ukienda kwa mganga wa kienyeji ukaambiwa lete hiki,lete kile mara hiki kamwe huwezi kuja na uzi kama huu hapa....

NOTE:
MIMI HUWA NATOA SANA SADAKA NA HATA ZAKA BILA KUJALI INAENDA WAPI MIMI IMANI YANGU HUWA NINATII MAAGIZO YAKE MUNGU KWA ZAKA NA DHABIHU LAKINI NINACHOKIAMINI HUWA SITOI SADAKA KWA MWANADAMU MWNYE PUA ZILIZOANGALIA CHINI KAMWE! MIE HUWA NATOA NKIAMINI NATOA KWA MUNGU ILI HATA SIKU NKIFIKA HUKO NTAKUWA NA LA KUJIBU LAKINI UKIWAZA KWMBA UKITOA UNAMPA MWANADAMU NI HELI USITOE TU,ENDELEA KUTOA KWENYE MAHARUSI,MASHEREHE NA KUZUNGUSHA BAR HAKUNA ATAKAEKUPANGIA
 
Hilo La Kupangia Waumini Kiwango Cha Kutoa Sadaka Liko Nje Ya Maandiko Matakatifu. Hao Watumishi Wanaofanya Hivyo Ni Utashi Wao Tu Na Hawako Kwenye Makanisa Ya Kiroho Tu Hata Makinisa Mengine Wapo, Tena Hawataki Fedha Za Sarafu Zina Thamani Ndogo. Wapo Watumishi Wa Ibilisi Waliovamia Makundi Ya Wana Wa Mungu Wakiwararua Watakavyo Wakiwa Wamevaa Ngozi Za Kondoo Kumbe Ni Mbwa Mwitu. Watu Wa Mungu Wanaangamia Kwa Kukosa Maarifa. Ni Neema Ya Mungu Tu Itawaokoa
 
Acha tu n back Catholic japo na uko
Michango haioungui lkn afadhali
Maana unatoa ulichonacho Ila
Baadh ya parish wamekataza mtu mzma kutoa coin's
 
Watapata Tabu Sana, Msemo Uliogeuka Dili La Kupata Fedha Kwa Wajasirimali Wa Kuandika (fine Art). Wenye Bodaboda, Bajaj Na Magari Ya Mizigo Wameupenda Sana Msemo Huu. Wanaandikiwa Kwa Nyuma Kama Swaga Tu
 
Tatizo ni hao wanaoliongoza kanisa.
Je wamehitimu miongozo ya Kanisa ?
Wakati huu kuna baadhi ya watu wanaanzisha kanisa wakiwa na Sera yao binafsi ya kujipatia kipato toka kwa waumini.
Kanisa linageuzwa kama kampuni ya kuingiza pesa na sio kuhubiri habari njema ya Kristo.
Mtu akiona hana mwelekeo wa kiuchumi basi anaenda Serikalini na anasajiri kanisa.
Vigezo vilivyowekwa na Serikali ili kumruhusu mtu kuanzisha kanisa ni tofauti kabisa na vigezo alivyoviweka Yesu Kristo.
Ndio maana tunaona baadhi ya makanisa waumini wanalishwa nyoka, mhubiri anasimama juu ya watu, wanawake wanavuliwa nguo, wanabakwa, wanazalishwa, nk. na baadhi ya viongozi wa baadhi ya makanisa ya zama hizi.
Mtu anaanzisha kanisa wakati hajasoma hata mstari mmoja wa Biblia na inawezekana hajawahi kuiona na kuishika.
Ndio maana Bwana Yesu alitahadharisha kuwa

" hapo baadae kutatokea manabii wengi wa uwongo, watakaowadanganya wengi na hata waumini kwa mbembwe zao hivyo kabla ya kuwaamini wapimeni maneno yao na matendo yao kama yanalingana na maagizo niliyowaachia "

Leo hii watu wakisikia tu flani kaanzisha kanisa bila kuangalia kushoto na kulia wanajiunga mojakwamoja kwenye ibada zake athari zake ndio hizo.

Nabii Tito alipata waumini haraka haraka na isingekuwa kukatazwa na Serikali leo hii kanisa lake linge jaa waumini.
Wakati muunini anaenda kanisani huku hajui lolote la kwenye Biblia, anakutana na Nabii ambaye naye hajui lolote la kwenye Biblia kama (Nabii Tito)
Hapo mchezo ndipo unapoanza kupendeza.
Kanisa lililo timiza vigezo kamwe haliwezi kuumiza waumini wake.

Kanisa kama la Mchungaji Mwakasege ni mojawapo ya Kanisa lenye vigezo vya Kristo mwenyewe.

Waumini mjihadhari.
 
Mnaopeleka pesa za jasho lenu katika dini iliyoletwa na dhalimu mnyonyaji akili zenu haziko sawasawa. Pale waafrika tutakapojua kuwa ujinga wetu ni fursa kwa wazungu tutapiga hatua.
 
Wanaboaaaaa sana unauziwa maji kwa sh 50000
 
Kwahiyo ndo tupangiane kiwango cha kutoa!!!? Umejaribu kukwepakwepa lkn ukweli ni kuwa sadaka inayozungumziwa hapa ni pesa tu na siyo kila muumini ana uwezo wa kutoa "sadaka pesa" kwa kiwango kile kilichopangwa, kwahiyo huyo naye asusiwe shughuri zake kisa siyo mtoaji!!!? Ile amri kuu ya Upendo tuliyoagizwa iko wapi!!? Wakristo wa siku hizi tumekuwa kama misukule.
Wewe FACT uliyezungumzwa hapa kwa mamlaka niliyopewa na Baba mtakatifu ninakubatiza kuwa PRINCIPLE.
 
Back
Top Bottom