chibuga mugeta
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 1,176
- 1,055
maandiko yameshawasema watu kama nyie,mwenyezi Mungu kupitia manabii na mitume alisema watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa na kutokusoma maandiko,magazeti ya udaku na umbea mnasoma sana ila kuchukua muda kujisomea neno la Mungu hampati huo muda mnasubiri kusomewa na wachungaji feki wenye kuchambua mafungu ktk biblia yenye kuwanaufaisha na kuwasononesha na kuwafurahisha ila ukweli hawausemi na mtaangamia kweli,na mtawanaufaisha kweli nami nasema acha wawapige,acha wawafilisi na hasa wanawake amabao wao wanaenda kusali sbb ya kupata miujiza,muda unapotea wakizinduka hawana kitu,umri umeenda na hakuna walichopata.Mjini shule,vijana wengi wasomi kwa sasa hawana kazi hvy kimbilio ni kufungua makanisa,kutafuta miujiza basiUmetoka nyumbani unaamua kuingia kanisani japo kupunguza stress za ugumu wa maisha na matatizo mbalimbali lakini humo kanisani unakutana na michango isiyoisha tena kwa lazima.
Nijuavyo mimi sadaka ni kile ambacho mtu amejaaliwa kukipata
Sasa eti kuna makanisa mpaka wameweka viwango sadaka isiwe chini ya kiasi flani, bado shukrani, bado fungu la 10, bado sadaka ya utumishi, bado sadaka ya madhabahu, bado sadaka ya malimbuko sijui nini. !
Mbaya zaidi kila mahubiri ni kusisitiza utoaji sadaka na michango tu.
Sio siri makanisa yetu mnakatisha tamaa kabisa ukute mtu ni mama wa nyumbani atapataje pesa yote hiyo kama sio mwanzo wa kugombana na mmewe.
Mungu atusaidie.
