Makamu wa Rais Mpango, mvua zinazonyesha zisije kuwasahaulisha utekelezaji wa makubaliano na Wahariri ili kusalimisha uharibifu kwenye Mto Ruaha Mkuu

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Saalamu,
Siku chache zilizopita tulishuhudia mjadala makini ulioitishwa na wanahabari huku mgeni rasmi alikiwa makamo wa raisi huko mkoani Iringa.

Dhina ya mkutano ule ilikuwa ni kumpatia mh mpango taarifa za kiuchunguzi juu ya chanzo cha mto ruaha mkuu kukauka kwani mpaka siku wanafanya kile kikakao mto ulikuwa umefikisha siku 120 hautiririshi maji kabisa.

Uchunguzi wa wahariri ulibaini zipo familia 12 za vigogo ndio waharibifu wakubwa wa mto ruaha mkuu,mto ambao ndio chanzo cha maji kwenye bwawa la mtera ambalo limekauka lakini pia mto huu unachangia 25% ya maji tunayoyatarijia kwenye bwawa la Mwl Nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea.

Lengo langu ni kumkumbusha mh Makamo wa raisi kwani sasa neema ya mvua inaonekana kila kona ya nchii hii jambo ambalo ninamashaka huwenda maadhimio ya ule mkutano ndio ikawa bye bye kwani mara nyingi nchi yetu ni wazuri wakucheza na matukio.

Tafadhali japo mto utaanza kutiririsha maji kutokana na hizi mvua zinazoanza kunyesha,tekelezeni maadhimio ya mlichokubaliana na wahiriri kule iringa ili kesho haya mambo yasije yakajirudia tena.

Thnx.
 
Naona bahasha zimeisha kwenye Sikukuu ya Christmas Sasa mnaanza kukumbuka viporo. Tajeni izo familia 12 kama kweli mpo serious na maisha ya Watanzania.
 
Miongoni mwa Makamu wa Rais asiye na 'meno' toka tupate uhuru ni huyu...vinginevyo tubadili katiba hiki cheo kifutwe kinatutia gharama pasipo sababu!.
 
Back
Top Bottom