Propaganda za Bolleni Ngeti na ukweli juu ya suala la umeme nchini

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Na Mwl Udadis, Dsm CBD

Moja ya sifa kuu ya kiongozi bora wa nchi ni kutatua matatizo kwa kuleta suluhu ya kudumu, wazungu wanaita "sustainable solutions", kwa bahati mbaya akili ndogo huhitaji muda mrefu kung'amua tija ya SULUHU za namna hii.

Mdogo wangu Bolleni Ngeti kwa makusudi ameamua kuhadaa umma juu ya tatizo la umeme nchini akiamini watu wengi si wadadisi. Tuwekane sawa hapa, tatizo la umeme nchini ni kweli limekuwepo na athari zake ni dhahiri, nitakupa chanzo cha tatizo na hatua zipi zimechukuliwa ambazo kwa hakika zinakwenda kutoa SULUHU YA KUDUMU.

Chanzo cha tatizo? Mto Ruaha Mkuu ni chanzo muhimu cha maji katika mabwawa ya Mtera na Kidatu ambayo kwa pamoja huzalisha hadi megawati 280. Mwishoni mwa mwaka 2022, serikali ilibaini uharibifu uliofanywa katika bonde la Ihefu na Usangu ambayo ndio chanzo cha mto Ruaha Mkuu, na tayari serikali ilianza kuchukua hatua kwa haraka japo athari za uharibifu uliofanywa ndio hizi tunazo ziona, ni uharibifu huu ulipelekea Ruaha Mkuu kuonyesha dalili za kuanza kukauka.

Sanjari na uharibifu huo, shughuli za kilimo na ufugaji ziliathiri vyanzo vya mto Ruvu, Ruvuma na Malagarasi. Ikumbukwe, umeme unaotokana na vyanzo vya maji umekuwa ukichangia kiasi kikubwa katika gridi ya Taifa. Iko hivi Bwawa la mtera linapokuwa na ujazo wa maji kuanzia Mita 450, huweza kuzalisha hadi megawati 200, lakini maji yakipungua, ujazo mdogo hulazimisha kuzimwa kwa baadhi ya mitambo na kufikia uzalishaji wa hadi megawati 30.

Ikumbukwe kabla ya uharibifu huu, Mtera ililazimika kufunguliwa ili kupunguza maji mnamo mwezi March 2020. (Najua unayo maswali mengi juu ya hili lakini huo ndio ukweli, na jambo hili kabla ya hapo liliwahi kufanywa mwaka 1997/98 wakati wa Mvua ya El nino)

SULUHU ya kudumu ni ipi? Kama kuna eneo ambalo busara za Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake zimeonekana ni katika kuandaa mkakati madhubuti wa kuondoa kabisa tatizo la umeme nchini kwa vitendo. Nitaeleza hapa.

Mosi, ili kuleta suluhu ya kudumu Rais Samia amechagua njia ya kitaalum tunayoweza kuiita "Energy Mix" yaani kuwa na vyanzo vya aina mbalimbali vinavyochangia katika gridi ya Taifa. Baada tu ya kuingia madarakani aliamua kufanya yafuatayo;

1. Kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa JNHPP (2115MW) kwa kuhakikisha fedha za mradi zinatolewa kwa wakati na usimamizi thabiti. Mpaka hivi sasa ninapo andika makala hii tayari serikali imetoa kiasi cha Trilioni 5.67 kati ya Trilioni 6.5 ambayo ndio fedha anayodai mkandarasi, hii ni zaidi ya 87%. Ni kwa kasi hii, leo hii tayari mashine zenye uwezo wa kuzalisha megawati 470 tayari zimefungwa, ambazo hizo tu zitazalisha umeme mwingi kuliko unaoweza kuzalishwa na Kidatu na mtera kwa pamoja.

2. Kutoa fedha za ukarabati na uboreshaji wa mitambo na miundombinu katika mabwawa yote muhimu. Huwezi kuendesha mitambo zaidi ya miaka 5 bila kufanya maboresho, mpaka hivi sasa tayari serikali imetoa fedha kiasi cha Bilioni 8 (Mtera), Bilioni 8 (Kihansi) na Bilioni 4 (Kidatu). Hii ndio maana ya "sustainable solution", sio kumkamua Ng'ombe bila kumpa marisho.

3. Hatua kali kwa watu wote waliochukua maeneo ambayo ni vyanzo muhimu vya mto Ruaha Mkuu na mito mingine kama vile Malagarasi, Ruvu, Ruvuma ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa umeme hapa nchini.

4. Uzalishaji wa umeme katika vyanzo vingine vya nishati endelevu vya joto la ardhini, jua na upepo. Tayari maeneo kama Kiejo-Mbaka na Ngozi yako tayari kwa uzalishaji wa nishati ya joto la ardhini ikiwa ni sehemu ya maeneo takribani 52 yaliyotambuliwa kuwa na uwezekano wa kuzalisha nishati hiyo. Upo uwezekano wa kuzalisha hadi megawati 1100 ifikapo 2025 kupitia vyanzo mbadala ili kukamilisha adhma ya Rais Samia ya kuwa na vyanzo vingi vya nishati "Energy Mix"

Tunapoongelea hii "Energy Mix" sio hadithi, tayari katika mwaka wa fedha huu tumeona mpango wa kuanza ujenzi wa mradi wa Kuzalisha Umeme Jua wa Shinyanga wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150 unaogharimu jumla ya Shilingi Bilioni 9.55. Mambo ni mengi mno, ningetamani kueleza hata kurasa 10 ila itoshe kusema kwamba njia ya kutafuta SULUHU ya kudumu ndio njia sahihi na ya kitaalum na si janja janja ya kutafuta sifa za kisiasa.

Baadhi ya watu kujaribu kuhadaa umma kutoona kazi hii kubwa ambayo inakwenda kuacha historia katika nchi yetu katu kusiwakatishe tamaa wasaidizi wa Rais na Mhe. Rais mwenyewe kwani muda si mrefu watanzania wote tutashuhudia matunda ya kazi hii iliyotukuka.
 
Mwambie apunguze chai,nchi ngumu hii,kama serikali ina nia ya kumaliza tatizo la umeme,ayo yangeshafanyika miaka mingi sana. TANESCO ni kichaka cha Wanasiasa na Wafanyabiashara uchwara kujitajirisha!
 
Mwambie apunguze chai,nchi ngumu hii,kama serikali ina nia ya kumaliza tatizo la umeme,ayo yangeshafanyika miaka mingi sana.
TANESCO ni kichaka cha Wanasiasa na Wafanyabiashara uchwara kujitajirisha!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
TANESCO WANAPEWAJE PESA NA SERIKALI WAKATI UMEME WANATUUZIA TENA KWA MGAO??

HAYA NDO YALELE YA TTCL, MBONA VODACOM HAWAPEWI HELA NA SERIKALI??

CCM MMECHOKA NA MMECHOKWA!!
 
Na Mwl Udadis, Dsm CBD

Moja ya sifa kuu ya kiongozi bora wa nchi ni kutatua matatizo kwa kuleta suluhu ya kudumu, wazungu wanaita "sustainable solutions", kwa bahati mbaya akili ndogo huhitaji muda mrefu kung'amua tija ya SULUHU za namna hii.

Mdogo wangu Bolleni Ngeti kwa makusudi ameamua kuhadaa umma juu ya tatizo la umeme nchini akiamini watu wengi si wadadisi. Tuwekane sawa hapa, tatizo la umeme nchini ni kweli limekuwepo na athari zake ni dhahiri, nitakupa chanzo cha tatizo na hatua zipi zimechukuliwa ambazo kwa hakika zinakwenda kutoa SULUHU YA KUDUMU.

Chanzo cha tatizo?
Mto Ruaha Mkuu ni chanzo muhimu cha maji katika mabwawa ya Mtera na Kidatu ambayo kwa pamoja huzalisha hadi megawati 280. Mwishoni mwa mwaka 2022, serikali ilibaini uharibifu uliofanywa katika bonde la Ihefu na Usangu ambayo ndio chanzo cha mto Ruaha Mkuu, na tayari serikali ilianza kuchukua hatua kwa haraka japo athari za uharibifu uliofanywa ndio hizi tunazo ziona, ni uharibifu huu ulipelekea Ruaha Mkuu kuonyesha dalili za kuanza kukauka.

Sanjari na uharibifu huo, shughuli za kilimo na ufugaji ziliathiri vyanzo vya mto Ruvu, Ruvuma na Malagarasi. Ikumbukwe, umeme unaotokana na vyanzo vya maji umekuwa ukichangia kiasi kikubwa katika gridi ya Taifa. Iko hivi Bwawa la mtera linapokuwa na ujazo wa maji kuanzia Mita 450, huweza kuzalisha hadi megawati 200, lakini maji yakipungua, ujazo mdogo hulazimisha kuzimwa kwa baadhi ya mitambo na kufikia uzalishaji wa hadi megawati 30.

Ikumbukwe kabla ya uharibifu huu, Mtera ililazimika kufunguliwa ili kupunguza maji mnamo mwezi March 2020. (Najua unayo maswali mengi juu ya hili lakini huo ndio ukweli, na jambo hili kabla ya hapo liliwahi kufanywa mwaka 1997/98 wakati wa Mvua ya El nino)

SULUHU ya kudumu ni ipi? Kama kuna eneo ambalo busara za Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake zimeonekana ni katika kuandaa mkakati madhubuti wa kuondoa kabisa tatizo la umeme nchini kwa vitendo. Nitaeleza hapa.

Mosi, ili kuleta suluhu ya kudumu Rais Samia amechagua njia ya kitaalum tunayoweza kuiita "Energy Mix" yaani kuwa na vyanzo vya aina mbalimbali vinavyochangia katika gridi ya Taifa. Baada tu ya kuingia madarakani aliamua kufanya yafuatayo;

1. Kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa JNHPP (2115MW) kwa kuhakikisha fedha za mradi zinatolewa kwa wakati na usimamizi thabiti. Mpaka hivi sasa ninapo andika makala hii tayari serikali imetoa kiasi cha Trilioni 5.67 kati ya Trilioni 6.5 ambayo ndio fedha anayodai mkandarasi, hii ni zaidi ya 87%. Ni kwa kasi hii, leo hii tayari mashine zenye uwezo wa kuzalisha megawati 470 tayari zimefungwa, ambazo hizo tu zitazalisha umeme mwingi kuliko unaoweza kuzalishwa na Kidatu na mtera kwa pamoja.

2. Kutoa fedha za ukarabati na uboreshaji wa mitambo na miundombinu katika mabwawa yote muhimu. Huwezi kuendesha mitambo zaidi ya miaka 5 bila kufanya maboresho, mpaka hivi sasa tayari serikali imetoa fedha kiasi cha Bilioni 8 (Mtera), Bilioni 8 (Kihansi) na Bilioni 4 (Kidatu). Hii ndio maana ya "sustainable solution", sio kumkamua Ng'ombe bila kumpa marisho.

3. Hatua kali kwa watu wote waliochukua maeneo ambayo ni vyanzo muhimu vya mto Ruaha Mkuu na mito mingine kama vile Malagarasi, Ruvu, Ruvuma ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa umeme hapa nchini.

4. Uzalishaji wa umeme katika vyanzo vingine vya nishati endelevu vya joto la ardhini, jua na upepo. Tayari maeneo kama Kiejo-Mbaka na Ngozi yako tayari kwa uzalishaji wa nishati ya joto la ardhini ikiwa ni sehemu ya maeneo takribani 52 yaliyotambuliwa kuwa na uwezekano wa kuzalisha nishati hiyo. Upo uwezekano wa kuzalisha hadi megawati 1100 ifikapo 2025 kupitia vyanzo mbadala ili kukamilisha adhma ya Rais Samia ya kuwa na vyanzo vingi vya nishati "Energy Mix"

Tunapoongelea hii "Energy Mix" sio hadithi, tayari katika mwaka wa fedha huu tumeona mpango wa kuanza ujenzi wa mradi wa Kuzalisha Umeme Jua wa Shinyanga wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150 unaogharimu jumla ya Shilingi Bilioni 9.55. Mambo ni mengi mno, ningetamani kueleza hata kurasa 10 ila itoshe kusema kwamba njia ya kutafuta SULUHU ya kudumu ndio njia sahihi na ya kitaalum na si janja janja ya kutafuta sifa za kisiasa.

Baadhi ya watu kujaribu kuhadaa umma kutoona kazi hii kubwa ambayo inakwenda kuacha historia katika nchi yetu katu kusiwakatishe tamaa wasaidizi wa Rais na Mhe. Rais mwenyewe kwani muda si mrefu watanzania wote tutashuhudia matunda ya kazi hii iliyotukuka.
Hii taariifa rasmi ya Tanesco au ni porojo kama kawaida yenu?
Chawa kama chawa wengine, hamna jipya hapo.

Hizi hadithi za kutafuta suluhisho la kudumu zilisikika tangu enzi za Kikwete alipokuwa anazindua mradi wa gas na kusema, "Sasa mgao wa umeme utakuwa historia"....yako wapi!!
 
Chawa unampigia mama chapuo tu. Eti tayari mama katoa hela sijui bilioni ngapi pale kwa uzalishaji na pale eti katoa mabioni kwa jsnusri kukarabati miundombinu. Maelezo kama hayo tuliwahi kusikia. Msitake watu wawe na matumaini kwa hela vigogo wanapeana kula na kazi ni ubabaishaji hakuna matokeo hela wanakula. Mama anachofanya ni kile walaji wenzake wanatarajia. Kutoa hela ya umma ya kodi na ya kukopa nje wale. Wananchi wanachotaka ni kuona wana umeme wa kutosha na wa ubora. Sio hadithi za kalumekenge alikataa kwenda shule na blah blah kama kawaida.
 
Back
Top Bottom