Makamu wa Rais, Dkt. Mpango: Changamoto hazimaanishi Muungano sio imara au hauna manufaa kwa wananchi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,034
2,000
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema changamoto ambazo zimekuwa zilijitokeza mara kadhaa hazimaanishi Muungano sio imara au hauna manufaa kwa Wananchi.

Amesema, "Serikali zetu zimekuwa zikibainisha changamoto hizo na kufanya jitihada za dhati kwa pamoja kuzipatia ufumbuzi kwa wakati na kwa manufaa ya pande zote mbili".

Ameongeza, "Serikali ya JMT na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa pamoja zimefanikiwa kutatua changamoto 15 kati ya 25 zilizokuwa zinaukabili Muungano wetu, na jitihada zinaendelea kufanyika".
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom