Makamba aingizwa mjini

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,131
0
Makamba aingizwa mjini CCM Tanga

Na Maingwa Mohamedi, Tanga

WAASISI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini hapa wameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha Katibu Mkuu Yusuph Makamba kuwapokea na kuwaapisha wanachama hewa alipofanya ziara mkoani wa Tanga hivi karibuni.

Wamesema wamegundua kuwa viongozi wa chama hicho kutoka wilaya mbalimbali walilazimika kutumia mbinu za udanganyifu ili kumridhisha Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Idd Amme ambaye aliwaagiza kuleta wanachama wapya.

Wazee hao walitoa madai hayo jana walipokuwa wakizungumza na mwaandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mkutano na ziara ya Katibu Mkuu wa CCM mkoani hapa.

Wazee hao walidai kuwa wanachama waliyopokelewa na Makamba katika uwanja wa Tangamano jijini hapa kuwa kwanatoka upinzani ni hewa.

Wanasiasa hao walisema hayo wakati wakiichambua taarifa iliyotolewa kwamba wanachama 12,000 kutoka vyama vya upinzani wamejiunga na CCM na kumtaka Makamba kuwapokea na kuwakabidhi kadi mpya za uanachama.

Walisema kitendo alichofanyiwa Makamba ni utapeli wa kisiasa kutokana na ukweli kwamba hakuna kazi ya siasa iliyofanywa na viongozi hao na kuwawezesha kupata wananchama wapya 12,000 waliojiunga kutoka vyama vya upinzani kujiunga na Chama hicho.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,307
2,000
Mgosi ! Kupenda sifa za mtindo wa kizamani zamani kunamshushia heshima sana. Hivi sasa anaonekana mwigizaji kama PWAGU.
 

Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,776
1,195
Nashangaa kwamba ndo wanastuka leo??
Mbona hii biashra ya kupokea wanachama hewa ipo siku zote??, tukianzia kule kigoma, tuli ijadili sana hapa, hata hii ya Jk aliyo lishwa kasa kwamba kapokea wanachama 40 wakiwakilisha wenzao 1000?

Lakini yote haya ni malezi na makuzi mazuri ya CCM ya kupika taarifa!
 

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
1,195
Hii ni kasumba mbaya sana- wanaanza na wanachama hewa then ukifika wakati wa uchaguzi watakuja na wapiga kura hewa na matokeo yake tunayaona Kenya sasa.
 

binti_bin

Member
Jan 1, 2008
5
0
It’s time Tanzanians we come to terms with harsh reality triggered by opposition parties. What made them fool their team leaders? I bet it’s kinda enforcement to get a little something!
 

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
7,059
2,000
This is terrible, wanachama hewa, wapiga kura hewa, kura hewa, matokeo hewa, ahadi hewa, utendaji hewa, every thing is hewa. Hii hewa itatuacha pabaya kama ilivyo kenya, msijefikiria hili linaishia kwenye wanachama tu, is a long thread.
 

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
14,995
2,000
This is terrible, wanachama hewa, wapiga kura hewa, kura hewa, matokeo hewa, ahadi hewa, utendaji hewa, every thing is hewa. Hii hewa itatuacha pabaya kama ilivyo kenya, msijefikiria hili linaishia kwenye wanachama tu, is a long thread.
Waliucheza mchezo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom