CCM [Kilimanjaro] yavuna watoto wa VETA zaidi ya 100 kuwaahidi ajira!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
WhatsApp Image 2024-03-09 at 20.45.48.jpeg

Leo 9-3-2024 Uongozi wa SENETI VYUO NA VYUO VIKUU (M) KILIMANJARO, Umezindua Tawi jipya La Idara ya Vyuo Chuo Cha VETA.

Katika Uzinduzi Huo wa Tawi la Chuo Cha NVTC kwa sasa kinaitwa VETA kilichopo Moshi Mjini, Zaidi ya Wanachama Wapya 120+ Walisajiliwa Kwenye Mfumo wa Kielektroniki na Kupewa kadi Mpya ya CCM na UVCCM.

Aidha, akizindua Tawi Hilo, Mwenyekiti wa SENETI Ndg. Godfrey G. Deho, aliwapongeza Mamia ya Wanafunzi walioridhia na kuamua Kulazimishwa kujiunga la sivyo hakuna connection ya ajira wala mikopo iwapo watataka kwenda vyuo vikuu Kujiunga na CHAMA CHA MAPINDUZI na hata hivyo hawakuonyesha Utayari wa Kukitumikia Chama.

Pia Katibu wa SENETI Ndg. Goodluck N. Bosha, aliwaeleza Wanachama hao Wapya Madhumuni na Malengo Makuu ya Kuwepo Kwa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu na Matawi yake, aliwagusia Wanafunzi hao juu ya Wajibu wa Kila Mwanachama wa CCM katika Kukijenga Chama na Taifa.

Katika Uzinduzi Huo, Katibu Hamasa wa SENETI Mkapa HALOTA, alitumia nafasi yake ya Kujitambulisha kuwaeleza Kwa Uchache Wanachama hao Wapya juu ya Historia ya Chama Cha Mapinduzi tangu TANU na ASP. Aidha Mratibu wa SENETI Bi Shania Minja, aligusia Juu ya Nafasi ya Binti na Mwanamke katika Chama Cha Mapinduzi na Ujenzi wa Taifa Tanzania.
 
Afadhali Mtoto wangu hasomi VETA. Angeingia kwenye anga za Kitapeli za Wana CCM
 
Back
Top Bottom