Cde. Shemsa Mohamed: CCM Yapokea Wanachama Wapya 100 Busega

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

Cde. Shemsa Mohamed: CCM Yapokea Wanachama Wapya 100 Busega

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea Wananchama wapya 100 kutoka kata ya Nyaruhande wilayani Busega Mkoani Simiyu baada ya kuridhisha na Utekelezaji wa Miradi ya maendeleo unaofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Wakizungumza jana mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Uanachama kwenye Maadhimisho miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika katika kata hiyo, wanachama hao wapya wamemshukuru Dk. Samia pamoja na wasaidizi wake kwa kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Umeme na Barabara.

Akizungumza mara baada ya kupokea wanachama hao wapya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed alisema Chama Cha Mapinduzi kimefanya mambo makubwa katika nchi hii ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa huduma kijamii.

Aliwataka wanachama hao kuendelea kuunga mkono juhudi za Dk. Samia Suluhu Hassan huku akiwata Mabalozi kuhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba ili CCM ishinde katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Shemsa pia aliwasisitiza kulipa ada za Uanachama ili waendelee kuwa hai na wanufaike na CCM ikiwemo kugombea nafasi za uongozi huku akisisitiza kuwa CCM imeimarisha mfumo wa utoaji kadi za uanachama ambapo kwa sasa kila mwanachama anapata kadi ya kielektroniki.

"Dkt. Samia ameelekeza wasaidizi wake tushuke kwa mabalozi na kuwatambua, nanyi ngazi ya wilaya waiteni Mabalozi, shirikianeni nao na tusipange wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu bali tupitishe kiongozi anayekubalika kwa wananchi" - Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed
 

Attachments

  • DSC_4290.JPG
    DSC_4290.JPG
    59.3 KB · Views: 3
  • DSC_4304.JPG
    DSC_4304.JPG
    64.1 KB · Views: 3
  • DSC_4309.JPG
    DSC_4309.JPG
    50.5 KB · Views: 2
  • DSC_4311.JPG
    DSC_4311.JPG
    55.7 KB · Views: 2
  • DSC_4241.JPG
    DSC_4241.JPG
    58.7 KB · Views: 2
  • DSC_4248.JPG
    DSC_4248.JPG
    56.3 KB · Views: 2
  • DSC_4268.JPG
    DSC_4268.JPG
    43.5 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom