Makala za Mohamed Said Katika Mwananchi: Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika


Mwanakijiji,

Sitanii hii ni kweli.

Katika hii "critique" yako nakiona kitabu kileeee kinakuja.

Usipuuze ushauri wangu.

Wewe una uwezo wa kuandika hebu tazama ulivyosimama na mimi "toe to toe" kama Waingereza wasemavyo unadhani ni kitu kidogo.

Matani ya nondo zote nilizokushushia hukufa bado unakuja tu.

Hilo si mchezo si unaona rafiki yako Mag3 kakimbia karudi leo anauliza hivi mnakasha bado unaendelea?

Andika kitabu unitoe makosa na dunia nzima ijue Mohamed Said kakutana na saizi yake.

Bila kitabu bado ushindi uko kwangu.

Mohamed
 

Najisikia kuheshimiwa mzee, ila kwa kweli kitabu ambacho nilikuwa nakifiria ni kutumia kitabu chako peke yake kuangalia vile vile ulivyoangalia wewe na kuvipa tafsiri nyingine.
 
Najisikia kuheshimiwa mzee, ila kwa kweli kitabu ambacho nilikuwa nakifiria ni kutumia kitabu chako peke yake kuangalia vile vile ulivyoangalia wewe na kuvipa tafsiri nyingine.

Plagiarism.

Andika chako usitafute pakutokea. Mohamed Said kisha weka msingi, kwa hilo tunamsifu, wewe ubaki kuwa "critique" na kuandika vijarida vya uchochezi, kuandika historia huwezi kabisa. Na Mohamed Said kawa "diplomatic" tu.

Mimi nakupa "open challenge" huwezi kuandika kitabu kikapata hata hata 5% ya "academical response" kama cha Mohamed Said. Uandishi wa vijarida ni tofauti kabisa na uandishi wa historia.

Huwezi, ikiwa hata vitabu vya imani za watu unavi "quote" isivyo na unashindwa hata kuomba msamaha unapostukiwa. Utaweza kuandikia historia? Aahhh, hilo si rahisi.

"Fumbo hufumbiwa mjinga, mwerevu huling'amua" nimeona nikusaidie kwa uliyoambiwa na Mohamed Said kwani nakuona huna uwerevu huo.
 
Walichanga kwa kuwa ni WAISLAMU au mioyo na uwezo wao uliwatuma kufanya hivo? Mohamed, kwako DINI ni gamba la nguvu. Na kwa umri wako kulivua hauwezi.
 
Walichanga kwa kuwa ni WAISLAMU au mioyo na uwezo wao uliwatuma kufanya hivo? Mohamed, kwako DINI ni gamba la nguvu. Na kwa umri wako kulivua hauwezi.

WC,

Kweli hawa watu walichanga kwa NIA moja,UWEZO na MIOYO yao misafi,sasa kinachotufanya sisi tushindwe KUWAPA TUNU nini?? au majina yao hayataleta UTAMU kwenye kuyatamka??? kama yale mingine ambayo juzi tu tumyapa vitivo pale Mlimani
 

Wakati mwingine tunajiburudisha.

1971 Muhammad Ali kafunguliwa kupigana na kamkuta Joe Frazier ndiyo "World Heavy Weight Champion."

Ali katoa changamoto, Frazier kapokea sasa wanakutana Guy Madison Square Garden, New York.

Mpamabano ukapewa jina "Fight of the Century."

Kwenye kitabu chake "The Greatest My Own Story" Ali anamsifia Frazier anasema nimeshusha kila aina ya kipigo kwa Frazier, Frazier anakuja tu yuko na mimi haniachii..."

Frazier akamshinda Ali kwa "points"

Ukiingia Guy Madison Square Garden utakuta bango kubwa sana la mpambano ule wa Ali na Frazier limepamba lango kuu.


Mohamed
 

Sheikh Mohamed,

Nachukulia bandiko hili kama wewe ndiye Muhamad Ali na Mwanakijiji ndiye Frazier!! au sivyo ulikusudia?
 
WC,

Kweli hawa watu walichanga kwa NIA moja,UWEZO na MIOYO yao misafi,sasa kinachotufanya sisi tushindwe KUWAPA TUNU nini?? au majina yao hayataleta UTAMU kwenye kuyatamka??? kama yale mingine ambayo juzi tu tumyapa vitivo pale Mlimani
TUNU wamepewa sana. Mitaa mingi tu hapa Dar ina majina yao. Ukitoa mchango wa harusi wanandoa wakizaa mtoto ni lazima wamwite JINA lako au la mkeo? Watu tunaielewa vibaya dhana ya michango.
 

Hal yangu.
Ulichoongea hapo kitu kizito sana. Kwani kunatofauti kubwa sana katika uadishi wa makala za kiucgunguzi na vijalida.

Hakka mwadishi anayediriki kuthubutu kuandika makala za kiuchunguzi siku zote ni mwandishi makini kwani hapo zinahitajika busara zan atka uuatilia mambo kuahata kufaya mahojiano mengi na watu mbalimbali kisha kuiweka mezani hiyo makala yako.

Mwanakijij hiyo ni chalenge kubwa sana kwako kwani pamoja na kutumia muda mwingi lakini pia unahitaji uwe na pesa za kufuatilia habari husika. Ok all in all tunasubiri makala yako.

Kila lenye kheir
 
Baadae wakakutana Zaire ya Mobutu na Mohamed Ali akashinda mwaka 1973?
 
Jasusi nikuulize,

Historia lazima muikubali nyie ndio iwe historia???? Kwani msikubali tu kuwa mmekosea na hivyo historia iandikwe kwa pande zote hata kama nyie hamuikubali??

Nafikiri ahali yangu hujaelew somo.

Hakuna hata ha kubadiisha historia yaTanganyka hapa bali alichoandika Sheikh Mohamed ni kuandika yale yaiyo sahaulika au kufichwa katika histori a Tanganyika. Kusaahulika huko au kufichwa huko iwe kwa makusudio maalum au bahati mbaya, Bw Mohamed ameamua kufanyika utafiti na kutuwekea makala yake hapa.
 

Shk Mohammed nilikuonya juu ya huyu mtu anayejiita Mwanakijiji. Huyu jamaa ni mbishi sana..utapoteza muda wako bureee! kuna mada humu ya NSSF na Dr Masau au NSSF na Vifo vya watoto Tabora ndipo utakapo mjuwa huyu mtu. Hebu fuatilia mijadala yake na Game Theory ndipo utakapo mjuwa.

Anathubutu kukudhihaki ilihali wasomi wa Ulaya na Marikani wanaafiki kama ulichoandika ni Historia.. mpaka reviews zake zikawekwa kenye ma jono ya historia '' Journal of Africa History''. Huyu jamaa licha ya kumpa rejea zoote na nyashaahid zote yeye bado haelewi, basi ni dhaahir ana ajenda yake huyu.
 

Kilasara,

With due respect... please read my book and you will see that we are of the same mind. There is no place in my work where even by far I hinted that the struggle for independence was a monopoly of Dar es Salaam.

But the chiefs were not forthcoming in supporting, TAA, TANU or the struggle.

If you have any new information contrary to what I have stated ukumbi will be glad to hear you.

But to give you the state of affairs obtabing at that time please go through this:

"Ilikuwa katika kipindi cha uongozi waAbdulwahid ndipo alipomwendea Chifu Kidaha Makwaia na kumuomba achukue uongoziwa chama kama rais. Abdulwahid alimwambia Chifu Kidaha kuwa endapo atachukuauongozi wa TAA, kwa kuchukua kwake uongozi wa Waafrika, angekua amefungua dimbala mageuzi Tanganyika kwa sababu machifu wengine wangemfuata. Kidaha alikuwachifu aliyependwa mno na serikali ya kikoloni, kwa ajili hiyo hakuweza kwawakati ule kuona busara ya kukubali ombi hilo. Pamoja na kauli aliyotoa kuhusuwatumishi Waafrika serikalini waruhusiwe kushiriki katika siasa, kauli ambayohuenda ndiyo iliyofanya uongozi wa TAA kumuomba achukuwe uongozi, Chifu Kidahaaliuamini uchifu na ushirikiano wa karibu na serikali ya Kiingereza kwa kupitiaindirect rule. Chifu Kidaha hakuwa tayari kuweka rehani nafsi yake na namaslahi ya watu wake kwa kukiunga mkono chama kilichokuwa kinapinga ukoloni.Baadaye mambo yalipowiva ndipo alipotanabahi kuwa alikuwa amepoteza nafasi yapekee ambayo ingemwezesha kuwa rais wa chama cha kwanza cha siasa (TANU)na labda kuwaWaziri Mkuu wa kwanza Tanganyika ililopata uhuru mwaka 1961."

Kilasara sasa huyu Nyerere mwaka 1957 yuko Mtaa wa Mvita, Dar es Salaam katika taarab ya TANU anahutubia. Hebu msikilize madongo yake kwa machifu:

"Katikahafla hiyo waheshimiwa, wageni waalikwa walipewa vitafunio, vinywaji baridi nachai. Nyerere katika kutoa shukrani kwa wanachama wa TANU alikamata kikombe chachai na kukionyesha juu kwa wasikilizaji wake. Aliwaambia watu kwamba wasidhanikitendo cha kumpa mtu kikombe cha chaini kitu kidogo. Nyerere aliendelea kusema kuwa watu wameiuza nchi hii kwakupewa kikombe cha chai na wakoloni. Nyerere alikuwa akitoa maneno hayo akiwaanawapigia vijembe watu maalum. Nyerere kwa maneno yake alikuwa akiwakusudia machifu. Baadhi yaowalikuwa pale pale katika meza kuu wakinywa chai na yeye. Wakati huo baadhi ya machifu walikuwa wakishirikianana Gavana Twining na UTP katika hila za kuipiga vita TANU ishindwekuikomboa Tanganyika kutoka makucha yaukoloni. Ilikuwa dhahiri kuwa makombo waliyokuwa wakipata machifu kutoka kwaMwingereza hayakuwa hata na thamani ya kikombe cha chai. Maneno ya Nyererehayakuwa fumbo kwa wale machifu. Yalikuwa maneno ya wazi ambayo waliyaelewa.Machifu walitambua kuwa wao ndiyo walikuwa wakisemwa katika hotuba ile yashukurani."

Karibu kwenye jamvi Bwana Kilasara.

Mohamed


Mohamed
 

Nimekusika Shk Yahya lakini nifanyeje nami nina amana ya Allah? Sheikh Mohamed Ayoub akisema ilm ni amana mwenyewe akija kuitaka ni wajib wako umpatie.

Sasa huyu mtu yarabi ndiyo kama unavyomwelezea mbishi lakini wajibu wa sie kumsomesha hauondoki.

Hivyo hivyo twende nae taratibu.

Mohamed
 
Sheikh Mohamed,

Nachukulia bandiko hili kama wewe ndiye Muhamad Ali na Mwanakijiji ndiye Frazier!! au sivyo ulikusudia?

MM,

Nakupa mji chukua New York kama hujafika nenda Guy Madison Garden tena iwe Jumamosi maana ndiyo kuna mambo hapo.
Umepatia.

Mwanakijiji kiboko bwana usifanye maskhara mie nikimsikia kwa vijana wangu wananieleza khabari zake.
Kataka kuniongeza mvi...huyu mtu.

Mohamed
 
TUNU wamepewa sana. Mitaa mingi tu hapa Dar ina majina yao. Ukitoa mchango wa harusi wanandoa wakizaa mtoto ni lazima wamwite JINA lako au la mkeo? Watu tunaielewa vibaya dhana ya michango.

Ilishindikana nini kuwa -acknowldged UDSM katika sherehe ya miaka 50? majina yao au dini zao? au ndio mfumo kristo at work
 

Mohamed,'
This is another face of Nyerere, no? Kuna mahali umetuambia kuwa Nyerere hakuweza kukabiliana na mtu uso kwa uso, mbona hapa anawamwagia machifu waziwazi bila kumung'unya maneno?
 

Mkandara,

Ndugu yangu tosheka na kwamba wengine tulikosa nafasi kwa sababu ya majina yetu. Kuna mzee wangu moja alipelekwa kusoma shule ya kikatoliki kwasababu ya uhaba wa shule zengine na ikabidi abadilishe jina lake ili aweze kuingia humo ndani. But tuachane na suala hilo pengine kuna sababu zengine zilichangia because I do not like to mourn the past.

Unapoyazungumza haya ya sasa na sheria kuwalinda wenye nazo source ya matatizo haya ni Nyerere. Kwanini mfumo aliouanzisha wa ujamaa ulipelekea jamii ya wateule nchini na wasiokuwa watawala. Tulikuwa tunasikia familia za kiteule tu Kuanzia Nyerere, Rupia, Bomani etc familia zengine za kimaskini zikawa hazisikiki. Mfumo wa utopia uliokuwapo madarakani ulipelekea kila kitu kikawa centralized na hatukuweza kuuliza kwanini imekuwa hivi badala ya vile. Isitoshe idara ya usalama wa taifa ilikuwa haifanyi kazi kwa interest ya taifa bali ikifanya kwa interest ya mfumo wa nchi. Ndio sababu watu kama akina Oscar Kambona, Mtei , Babu na wengineo wengi walikimbia nchi kwasababu waliyaonamapungufu wakaamua kuondoka nchini kuokoa maisha yao. Mfumo huo sasa ukaja ukarithiwa na mabepari wa nchi na wanautumia kulinda maslahi yao. Hivyo kabla hujaulalamikia mfumo pengine tuuliza mfumo huu ulianzia vp hadi ukafikia ulivyo sasa hivi.

HIVYO BASI KABLA HUJAANZA KUZUNGUMZIA MFUMO ULIOPO ULIZIA MFUMO HUO ULIANZIA WAPI? Anyway hiyo sioni jambo la msingi suala la msingi ni kwanini kuna imbalance katika education and social development between Muslims and Christians. Umesema sana kuhusu wakristo kuendeleza shule zao na jamii zao hata hivyo nimekuuliza swali msingi kabisa JE SERIKALI INAWAPA HELA WAISLAMU KAMA INAVYOWAPA WAKRISTO???? Hili swali haulijibu badala yake unakimbilia kujustify kwanini wakristo wanapewa hela. Labda nikuongezee swali jengine hivi unafahamu kuna taasisi na shule za waislamu zilichukuliwa before independence na viwanja vingi vya waislamu vilichukuliwa baada ya kutangazwa kwa azimio la arusha. Je viwanja hivyo wenye navyo walirudishiwa kihalali?

Mkandara usiyaguse ya sasa kwanza kabla hatujamaliza ya zamani ndugu yangu. Sifa moja ya usomi is to know how ask the right question at the right time and place sio vyenginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…