Ameeleza vizuri sana, kwa ufupi. Nadhani ambacho kinaweza kuleta utata kwa baadhi ni namna ambavyo mwezi unaweza kuyavuta maji.
Fikiria mwezi kama sumaku, then dunia na kila kitu (na maji pia) ni sumaku. Kwa hiyo vinavutana. Sasa maji kwa vile hayashikamani, yanavutwa na kuhama kulingana na uelekeo wa mwezi na jua angani.
Ikumbukwe kwamba mwezi (na jua) huwa sehemu tofauti tofauti angani, na hii huamua ni wapi kwenye uso wa dunia kuna kani yake ya uvutano mkubwa zaidi.
Palipo na kani kubwa ya uvutano, maji huvutwa zaidi na hivyo hujaa (high tide). Palipo na kani ndogo ya uvutano, maji hupwa (low tide).