Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,431
Kwetu hakuna bahari, ila kuna ziwa kubwa sana. Mara ya kwanza kufika mikoa ya Pwani nilishanga sana kuona bahari ikiwa kavu na maji yake yameondoka.
Ndipo nilipoikumbuka stori ya moja wa mshujaa wetu aitwaye Ng'wana Malunde. Huyu mwamba baada ya kuwasumbua sana wakoloni, walimua kumkamata na kwenda kumfunga Unguja, aliyeyuka huko gerezani na kuonekana maeneo mbalimbali akirandaranda na ndipo aliposimulia habari za bahari kwenda kuchunga.
Sasa nyie watu wenye bahari yenu, naomba mnijuze kwa kina, bahari ikipwa huenda wapi?