Maji ni huduma ambayo Serikali inafeli vibaya mno, uhaba na mgao karibu kila mkoa japo mabilioni yanatumika. Rais Samia anashindwa wapi?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Nilitegemea kwamba serikali inayosema inapigana na kupambana sana kuhudumia watu wake ingefanikiwa sana katika suala la kutoa maji kwa watu wake. Lakini inasikitisha sana kwamba hadi leo Tanzania inafeli sana katika kutoa huduma hii kwa wananchi. Na kinachosikitisha hata zaidi ni kwamba hii ni huduma muhimu sana hasa kwa wananwake na watoto, na ina athari katika mambo mengi.

Huduma mbovu za maji zina athari nyingi sana, kwa mfano;
  • Wanawake wanapoteze muda mwingi katika kufuata maji
  • Matatizo ya kijamii kama kubaka watoto na wanawake wanapokuwa wakifuata maji
  • Hatari za afya za wananchi kutokana na kutokunywa maji safi na kutokuwa na usafi wa mwili
  • Ugomvi katika familia na jamii kutokana na uhaba wa maji
Matarajio yangu yalikuwa kwamba kuwa na raisi mwanamke kungekuwa ni chachu ya tatizo hili kukomeshwa nchini, lakini hali bado ni mbaya leo kama ilivyokuwa jana. Tunachoona ni matumizi makubwa ya fedha kwenye miradi ya maji bila kuona matukio ya miradi huo. Ufisadi umezidi mno kwenye miradi ya maji na hatusikii watu kuchukuliwa hatua.

Jambo la aibu hata zaidi ni kwamba hata sehemu zenye rasilimali ya maji kubwa sana zinakuwa na matatizo ya maji. Mikoa kama Mbeya, KIlimanjaro, Iringa, Morogoro, nk, yenye mito na vyanzo vya maji tele kwa nini iwe na matatizo ya maji?

Kichekesho kwa mfano, ni mwanzoni mwa mwaka huu nilitembelea mji wa Tukuyu huko Mbeya, na kukuta kuna uhaba mkubwa wa maji, ambapo sehemu za mji huu zina mgawo wa maji wa siku mbili au tatu kwa wiki. Niliuliza viongozi wa mji, chanzo cha maji katika mji huu ni wapi? Nikaambiwa ni pembezoni mwa Mlima Rungwe. Nikasema ikiwa chanzo ni huko mlimani, ina maana mnaweza kugawa maji kwa kutumia gravity tu, na kinachihitajika ni mambomba na matenki makubwa labda matatu tu. Sasa kwa nini mji una shida ya maji muda wote huu ikiwa gharama za kusambaza maji ya gravity ni za nchini kiasi hiki? Hakuna aliyenipa jibu la kitaalamu zaidi ya majibu ya kitoto ya kisiasa.

Nina uhakika mikoa kama KIlimanjaro, Arusha, ziko katika mazingira kama haya ya kupata maji kwa gravity lakini hakuna chochote kinachoendelea.

Mama Samia, watu wako wanashindwa wapi katika hili? Huenda ni jambo linahitaji liangaliwe upya na sio kutumia njia za zamani ambazo zimefeli kwa muda mrefu sana. Tunaweza kuelewa matatizo ya umeme na kuyavumilia, lakini sio maji. Ikibidi dedicate tozo za mwaka mzima ziende kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji. Kama raisi wa kwanza Tanzania mwananke, ukimaliza muda wako bila kuhakikisha access ya maji nchini ni 100% nitakushangaa sana. Utakuwa umewaangusha na hata kuwasaliti mno wanawake wenzio.

Reference: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/mgawo-wa-maji-watikisa-mijini-vijijini-3974394
 
Wana JF mnaoishi sehemu zenye uhaba wa maji, hebu tuelezeni basi sehemu zenu ni zipi na hampati maji kkwa ukawaida
 
Wana JF mnaoishi sehemu zenye uhaba wa maji, hebu tuelezeni basi sehemu zenu ni zipi na hampati maji kkwa ukawaida
Dar hii hii mbezi malamba mawili,king'azi maji ni shida,cha kushangaza eneo hili liko chini ya kata ya kwembe ambapo hapo kwembe kuna mradi mkubwa wa maji ulizinduliwa na magufuli sambamba na ule wa wilaya ya kisarawe,sio mbunge wa ubungo wala diwani anaejali ukosefu wa maji,na si maji tu barabara pia ni shida!
 
Bongo ni nyoso kila mara unasikia kuna bilion kazaaa zimetengwa kwa ajili ya maji ila sasa hata hazionekani ziko wapi km huku kigamboni kuna mavisima yamechimbwa yana miaka yanajengwa hata bomba hawajaanza kusambaza naona watakuja kuyatumia wajukuu zangu.Viongozi tunaomba kigamboni mtupe na sie maji maana km vyanzo mlisha chimba ni kusambaza na kuweka pump tu hapo kisarawe 2 biashara inaisha.
 
Maji na umeme ni huduma zisizo na kikomo yaani kuna wamasai na wahadzabe ukiwapelekea maji na umeme wanahama wanaenda mbali kuanzisha makazi mapya huko sasa tatizo haliwezi kuisha kwa style hyo
Mkuu, Tanzania kuna miji mingapi ya Wamasai na Wahdzabe? Hicho ndio kisingizio? Kwanza tangu Wamasai wahamia Vigwaza njia ya Morogoro sijaona kama wamehama, miaka zaidi ya ishirini sasa
 
Dar hii hii mbezi malamba mawili,king'azi maji ni shida,cha kushangaza eneo hili liko chini ya kata ya kwembe ambapo hapo kwembe kuna mradi mkubwa wa maji ulizinduliwa na magufuli sambamba na ule wa wilaya ya kisarawe,sio mbunge wa ubungo wala diwani anaejali ukosefu wa maji,na si maji tu barabara pia ni shida!
POleni sana Mkuu. Unakuta ni hatua ndogo sana za kuchukuliwa kurekebisha, lakini ni nyimbo tu za siasa zinatolewa
 
Bongo ni nyoso kila mara unasikia kuna bilion kazaaa zimetengwa kwa ajili ya maji ila sasa hata hazionekani ziko wapi km huku kigamboni kuna mavisima yamechimbwa yana miaka yanajengwa hata bomba hawajaanza kusambaza naona watakuja kuyatumia wajukuu zangu.Viongozi tunaomba kigamboni mtupe na sie maji maana km vyanzo mlisha chimba ni kusambaza na kuweka pump tu hapo kisarawe 2 biashara inaisha.
Kigamboni nina kiwanja siku nyingi na mojawapo ya vikwazo vyangu kwenye kujenga ni maji!
 
Bongo ni nyoso kila mara unasikia kuna bilion kazaaa zimetengwa kwa ajili ya maji ila sasa hata hazionekani ziko wapi km huku kigamboni kuna mavisima yamechimbwa yana miaka yanajengwa hata bomba hawajaanza kusambaza naona watakuja kuyatumia wajukuu zangu.Viongozi tunaomba kigamboni mtupe na sie maji maana km vyanzo mlisha chimba ni kusambaza na kuweka pump tu hapo kisarawe 2 biashara inaisha.
Kweli wewe ni ngosha Acha ushamba .

Dar kuna mgao WA maji na huku wanaishi wamasai ?
 
POleni sana Mkuu. Unakuta ni hatua ndogo sana za kuchukuliwa kurekebisha, lakini ni nyimbo tu za siasa zinatolewa
Rushwa mzee,wenye vilori vya kuuza maji wanacheza na dawasa mzee,hizo miundo ya maji ipo shida hawataki kuunga maji wakiunga biashara ya maji inakufa
 
Sehemu kubwa ya umeme wa Tanzania tunategemea vyanzo vya maji (H.E.P)

Na maji kwa matumizi ya nyumbani na viwandani chanzo ni hii mito yetu na mabwawa.

Kabla ya kulaumu ni nani ana takwimu za vyanzo vya maji viko katika hali gani ndani ya miaka hii miwili?

Ninauliza hivi kwa sababu wote ni mashuhuda mwaka jana na mwaka huu mvua zimenyesha kidogo.

Sasa ikiwa umeme na maji hapa Tanzania vinategemea vyanzo vya maji je, mamlaka husika zifanye nini ili angalau wananchi wapate kidogo tulicho nacho?

NB: Na tutegemee pia kupanda kwa bei za vyakula miezi ijayo
 
Muheza mwaka karibu wa ishirini sasa maji toka milima ya magoroto hayafiki mjini
Huo ni mfano halisi wa maeneo ambayo maji hayahitaji pampu wala umeme kuyatoa milimani na kuyafikisha kwa watumiaji. Yanapaswa kutumia gravity kama yatachukuliwa kule milimani, na kinachohitajika ni mabomba na kujenga tanki. Taki linajengwa ili kusaidia pia kupunguza pressure, ukigagawa moja kwa moja pressure itakuwa kubwa mno yatapasua mabomba
 
Halafu hii ya mara mbili kwa wiki sijui walikubaliana huko wizarani, iko sehemu nyingi sana. Hivi jamii zitaishije na mgao wa maji wa mara mbili kwa wiki?
Acha kabisa Yaani Ila Kwao uzunguni yanatoka ka Siku
Huku Kwa wapiga kura ndo taabu ilipo mfano huku nkuhungu yanatoka j4 na Ijumaa Ila Leo hayajatoka Yaani ni balaa,mmejiulza Hii nchi ina viongozi?
Mbona wabinafsi sana afu Wana roho mbaya
 
Sehemu kubwa ya umeme wa Tanzania tunategemea vyanzo vya maji (H.E.P)

Na maji kwa matumizi ya nyumbani na viwandani chanzo ni hii mito yetu na mabwawa.

Kabla ya kulaumu ni nani ana takwimu za vyanzo vya maji viko katika hali gani ndani ya miaka hii miwili?

Ninauliza hivi kwa sababu wote ni mashuhuda mwaka jana na mwaka huu mvua zimenyesha kidogo.

Sasa ikiwa umeme na maji hapa Tanzania vinategemea vyanzo vya maji je, mamlaka husika zifanye nini ili angalau wananchi wapate kidogo tulicho nacho?

NB: Na tutegemee pia kupanda kwa bei za vyakula miezi ijayo
Mkuu, unajua ni kiasi gani cha maji yanakwenda kuishia baharini na kwenye maziwa? Na pia, kuwa na miradi ya Hydo hakuzuii kusambaza maji kwa matumizi, kwa kuwa bado unaweza kutumia maji downstream ya HEP. Hydo hazi-consume maji, zinayapitisha tu kwenye turbines na infact yanapotoka kwenye turbine yanakuwa na pressure kubwa tu. Kwa hiyo kitu kimoja hii serikali ingekuwa ni ya mainjinia wangefanya kila mradi wa HEP unakuwa chanzo cha kusambaza maji, downstream the turbines

Angalia picha hii ya Mtera

1665137417354.png
 
Back
Top Bottom