Asante Rais Samia kwa Maendeleo Sekta ya Maji Wilaya ya Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

ASANTE RAIS DKT. SAMIA KWA MAENDELEO YA SEKTA YA MAJI WILAYA YA LUDEWA

Kamati ya Kudumu ya Bunge- ya Maji na Mazingira; ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati- Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga(MB) sambamba na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Anna Richard Lupembe (MB)- wamefika Mkoani Njombe, Wilayani Ludewa kwenye Ukaguzi wa Mradi wa Maji wa Luvuyo.
Kamati hii iliambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Maji- Mhe Eng. Maryprisca Mahundi.

Wilaya ya Ludewa inashukuru na kuthamini sana ugeni huu wa Kitaifa- kwani umekagua mradi wa Luvuyo ambao una Gharama za Mradi Jumla ya kiasi cha:- 1,523,922,255.46
Mradi huu unatajia kunufaisha wananchi wapatao: 2,268

Kazi zilizopangwa kutekelezwa kwenye mradi huu;
i. Ujenzi wa chanzo cha maji(Intake)
ii. Uchimbaji mtaro, ulazaji wa bomba na ufukiaji bomba kwenye njia kuu na njia za usambazaji (14.262km)
iii. Ujenzi wa tenki la maji (150M3) juu ya mnara wa mita 4
iv. Ujenzi wa vituo 6 vya kuchotea maji na ukarabati wa vituo 22
v. Ujenzi wa Ofisi ya CBWSO

Mradi umetekelezwa kwa asilimia 75% hadi sasa.

Utekelezaji wa mradi huu unalenga kuboresha huduma ya maji kwa wakazi 2,268 wa Kijiji cha Luvuyo. Mradi huu utawezesha kuruhusu utumiaji wa chanzo namba 3 eneo la Igongwi kinachotumika kuhudumia wakazi wa Luvuyo kwa sasa kiweze kuwa miongoni mwa vyanzo vitakavyotumika kwenye mradi wa Igongwi unaojengwa ili kuhudumia vijiji vya wakazi wa Wilaya ya Njombe.

Changamoto ya chanzo cha maji imetatuliwa rasmi na Kamati ya Kudumu ya Bunge- Maji na Mazingira kwenye ziara yao ya Kimkakati.

Wana-Ludewa Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania- Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Fedha za mradi huu wa maji- na kwa maendeleo yote Sekta ya Maji Wilayani Ludewa-
Tunamshukuru Waziri wa Maji- Mheshimiwa Jumaa Aweso kwa kazi kubwa kwenye Sekta ya Maji.
Sambamba na Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mheshimiwa Joseph Kamonga kwa kuzidi kutetea wana-Ludewa kwenye kazi zake zote.

Tunashukuru uongozi wa RUWASA Mkoa wa Njombe- Engineer Sadick Chakka- na Engineer RUWASA wa Wilaya ya Ludewa Engineer Jeremiah Maduhu kwa ushirikiano mkubwa, usimamizi bora wa Sekta ya Maji.

Katika Ziara hii- Wilaya ya Ludewa ilishiriki kikamilifu- Kamati ya Usalama ya Wilaya- Kamati ya Siasa ya Wilaya na viongozi wa Kata, Kijiji na wananchi wa Luvuyo.

Tupo pamoja katika utendaji na kuhakikisha Wana-Ludewa wanapata huduma ya Maji Bora, Safi, Salama na Yenye Kutosheleza.
Tunasema Asante na Mwenyezi Mungu awabariki.

Victoria Mwanziva
DC Ludewa
15/03/2024
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.38(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.38(1).jpeg
    123.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.36(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.36(2).jpeg
    110.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.36(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.36(1).jpeg
    119.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.37.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.37.jpeg
    92.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.37(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.37(1).jpeg
    144.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.38.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-17 at 14.59.38.jpeg
    116.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom