JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Ng’ombe 15 wamekufa katika kijiji cha Losirwa wilayani Monduli Mkoa wa Arusha wakidaiwa kuwa wamekula majani yenye sumu yaliyoota maeneo mbalimbali kijijini hapo.
Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya ya Monduli, Fank Mwaisumbe amesema hadi jana zaidi ya ng'ombe 15 wamekufa kwa kula majani hayo.
"Nimepata taarifa za mifugo kufa kutokana na majani hayo na sasa tumeagiza ifukiwe ili watu wasile mizoga yake kwani ni sumu," amesema akibainisha kuwa uzikaji wa mifugo hiyo unasimamiwa na polisi ili kuhakikisha hakuna watu watakaokula mizoga.
Mmoja wa wafugaji, Lememo Mollel amesema,”hii sio mara ya kwanza mifugo kufa kila baada ya ukame kutokea, mvua zikianza kunyesha majani yenye sumu huota na mifugo wakila hayo majani wanakufa.”
Hata hivyo, aliomba Serikali kusaidia upatikanaji wa malisho ya mifugo hasa kipindi hiki cha ukame.
Daktari wa Mifugo wa shirika la kilimo na chakula la umoja wa mataifa (FAO), Moses Ole-Neselle amesema kufa mifugo kunatokana na kula majani mabichi yenye sumu kutokana na kutokamaa.
"Mifugo inakufa pia kwa sababu bado utumbo haujazoea kula majani mabichi ambayo hayajakomaa baada ya kiangazi kwanza huwa wanaharisha na wengine kufa kabisa," amesema.
Chanzo: Mwananchi