Chakula kinachodaiwa kuwa na sumu chaua watoto 5 wa familia moja

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Watoto watano wa familia moja Kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamekufa baada ya kula chakula kinachohofiwa kuwa na sumu huku mmoja akiwa anaendelea kupatiwa matibabu hospitali teule ya Biharamulo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera Brasius Chatanda amesema kuwa watoto waliopoteza maisha ni Brian Ezekiel (3), Kahindi Samson (9), Happeness Lazaro (12), Melina Lazaro (2) na Melesiana Lazaro (11).

"Mnamo tarehe 13/11/2023 majira ya saa za usiku familia ya Lazaro Sanabanka (61) mkulima wa Kijiji cha Nyakanazi akiwa na familia yake kwa pamoja walikula chakula ambacho ni ugali mboga za majani ya maharage, baba alikula chakula akiwa na watoto watatu na watoto waliobaki walikula chakula hicho wakiwa pamoja na mama yao". Amesema Chatanda.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

"Tumepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za vifo vya watoto watano ambao wanasadikika kula chakula chenye sumu taarifa hizi zimetustua sana lakini kwa dhamana tuliyonayo kazi yetu ni kufanya uchunguzi wa kina na kuna wataalamu wanakuja kutoka nje ya mkoa kwaajili ya uchunguzi wa suala hili," amesema.

Chanzo: EastAfricaTV

=================
Mussa-Chatanda.jpg

UPDATES: WALIOFARIKI KWA CHAKULA KINACHODHANIWA KUWA NA SuMU WAFIKA 6
Idadi ya watu wa familia ya Lazaro Sanabanka mkazi wa kijiji cha Nyakanazi waliofariki dunia baada ya kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu jioni ya November 13 mwaka huu imeongezeka kutoka watu 5 na kufika 6.

Aliyefariki dunia hii leo ni mtoto mdogo ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospital Teule ya Biharamulo.
 
Inauma sana, tena sana. Pole Lazaro na mkeo mama Mele. Pumzikeni salama watoto.

Yaani ukiamka unaona vichuguu vitano. Lazima uhame Kijiji. Ningekuwa na uwezo nampa shamba mnzani. Mama fatuma mwasa... Mbadikishieni mazingira huyo Mzee
 
nawaombeni sana mijusi wa manyumbani wa Rangi ya kaki wauweni wakilamba mwiko kaweka sumu na wengine huangukia kwenye mboga bila kumuona na mkila hiyo mboga huwezi kupiga hatua hata moja unakufa hapo hapo
Wakoje hao mkuu
 
Sio kweli

Mijusi Kafiri haina shida yoyote

Kuua viumbe vya Mungu bila kuvitumia ni dhambi.
 
nawaombeni sana mijusi wa manyumbani wa Rangi ya kaki wauweni wakilamba mwiko kaweka sumu na wengine huangukia kwenye mboga bila kumuona na mkila hiyo mboga huwezi kupiga hatua hata moja unakufa hapo hapo
Story za vijiweni tu hizo hazina uthibitisho wowote, popote!

Mbona watu wazima (wazazi) hawajafa na wamekula chakula kilekile?

Yawezekana hiyo sumu watoto wamekula kabla ya hiyo dinner!

Story za vijiweni tu hizo hazina uthibitisho wowote, popote!

Mbona watu wazima (wazazi) hawajafa na wamekula chakula kilekile?

Yawezekana hiyo sumu watoto wamekula kabla ya hiyo dinner!

asante sana. Tunataka vitu kama ivi hapa JF! Scientific proof...
see extract from the website you have posted

Conclusion
The posts which were shared mentioning that the geckos are deadly venomous or poisonous even than snakes are incorrect. They are just innocent, harmless animals. There can be some harm, but it does not occur because of venom or poison. But food contaminated with their faeces is dangerous and can pervade human salmonellosis.
 
Watoto watano wa familia moja Kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamekufa baada ya kula chakula kinachohofiwa kuwa na sumu huku mmoja akiwa anaendelea kupatiwa matibabu hospitali teule ya Biharamulo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera Brasius Chatanda amesema kuwa watoto waliopoteza maisha ni Brian Ezekiel (3), Kahindi Samson (9), Happeness Lazaro (12), Melina Lazaro (2) na Melesiana Lazaro (11).

"Mnamo tarehe 13/11/2023 majira ya saa za usiku familia ya Lazaro Sanabanka (61) mkulima wa Kijiji cha Nyakanazi akiwa na familia yake kwa pamoja walikula chakula ambacho ni ugali mboga za majani ya maharage, baba alikula chakula akiwa na watoto watatu na watoto waliobaki walikula chakula hicho wakiwa pamoja na mama yao". Amesema Chatanda.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

"Tumepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za vifo vya watoto watano ambao wanasadikika kula chakula chenye sumu taarifa hizi zimetustua sana lakini kwa dhamana tuliyonayo kazi yetu ni kufanya uchunguzi wa kina na kuna wataalamu wanakuja kutoka nje ya mkoa kwaajili ya uchunguzi wa suala hili," amesema.

Chanzo: EastAfricaTV
Mwanaume wa miaka 61 ana watoto wa miaka 3 hadi 12!!!! Msinipopoe please!!!!🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️
 
dah ! ukute hata ni kile ki mjusi kafir kimetumbukia kwenye sufuria la msosi bila wao kujua 😞
 
watoto-pic.png

Muktasari:​

Watoto watano wa familia moja wamefariki dunia katika kijiji cha Nyakanazi Wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera kwa kile kinachosadikika kula chakula chenye sumu.
Biharamlo
. Watoto watano wa familia moja wamefariki dunia katika kijiji cha Nyakanazi Wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera kwa kile kinachosadikika kula chakula chenye sumu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kuwa vimetokea kwa nyakati tofauti baada ya wanafamilia 11 kula chakula cha usiku Novemba 13, 2023.
Chatanda amesema, wanafamilia hao baada ya kula chakula cha usiku walienda kupumzika lakini asubuhi yake watoto watatu Brayan Ezekiel (2), Kahindi Samson (9) ambaye ni mwanafunzi wa awali shule ya msingi Muungano na Happines Razaro (12) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Muungano walianza kujisikia vibaya wakakimbizwa kituo cha afya Nyakanazi wakati wanaendelea na matibabu Novemba 14, 2023 wakapoteza maisha.
Amesema kuwa, baada ya watoto hao kupoteza maisha wengine watatu walianza kujisikia vibaya nao walipelekwa katika hospitali ya rufaa ya wilaya ya Biharamlo wakati wakiendelea na matibabu Novemba 15, 2023 wawili walipoteza maisha na hivyo idadi ya waliofariki kuwa watano.
Wawili waliofariki ni Melisiana Razaro (11) na Melina Razaro (9) huku Josephina Juma (5) akiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
Aidha amesema wanafamilia wengine ambao walishiriki chakula hicho akiwemo mama aliyepika wako salama na uchunguzi wa awali umebaini kuwa chakula kilikuwa na sumu na uchunguzi unaendelea kubaini ilikuwa ni sumu ya namna gani.
Amesema miili ya watoto watatu bado imehifadhiwa katika kituo cha afya Nyakanazi huku miili miwili ikiwa imehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya wilaya ya Biharamlo.
Chatanda amasema wamechukua sampuli kwa ajili ya kuzipeleka kwa mkemia mkuu wa serikali.
Diwani wa kata ya Rusahunga Amos Madebwa amesikitishwa na vifo hivyo na kusema kuwa, alipokwenda hospitali daktari alimwambia watoto walikuwa wanabanwa kifua pamoja na maumivu ya tumbo. chanzo. Watoto wafariki wakidhaniwa kula chakula chenye sumu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom