Ulishaji wa ng'ombe, mbuzi na kondoo kipindi cha ukame

JS Dairy Farm

JF-Expert Member
Feb 13, 2022
305
679
Mwaka 2023 umekua mwaka wa neema kwa wafugaji, mwaka wa maji mengi na malisho mengi tofauti na mwaka 2022 ambapo ng'ombe wengi walikufa.Gazeti la Mwananchi la Jan.16,2022 liliandika kuwa Ng'ombe 5000 walikufa kwa ukame wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro na gazeti hilohilo la Feb.12,2022 liliandika kuwa ng'ombe 25,000 walikufa wilayani Kiteto mkoa wa Manyara kwa sababu ya ukame.Kipindi cha ukame hapa nchini ng'ombe,mbuzi na kondoo wengi huwa wanakufa kwa sababu ya kukosa maji na chakula na wanaobahatika kubaki huwa wanakondeana na hawafai kwa soko.

Lakini mwaka huu 2023 utabaki na kumbukumbu nzuri kwa wafugaji kwani mpaka sasa hakuna habari iliyosikika ya kufa kwa mifugo kutokana na kukosa maji au chakula.
Sasa tukumbushane njia za kuhifadhi chakula cha wanyama wanaokula nyasi(malisho)wakati wa ukame.

1.Hei (Hay)
Hei ni malisho yaliyovunwa,yakakaushwa na kisha kuhifadhiwa bila kufanyiwa utalam mwingine wowote wa ziada.Hei ikikaushwa vizuri,inaweza kuhifadhiwa mahali pakavu pasipofikiwa na mvua au unyevu wowote na kulishwa mifugo wakati wa ukame au kiangazi.Ili kupata kiwango cha juu cha viinilishe,nyasi zitakazotumika kutengeneza hei zivunwe kabla ya kufika umri wa kutoa maua.Baada ya nyasi kuvunwa,zikaushwe juaani huku zikigeuzwa mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa sehemu zote za nyasi hizo zimekauka.Chukua tahadhari kuhakikisha kuwa nyasi hizo haziachwi hadi zikauke mno.Nyasi nyembamba zinaweza kuchukua muda wa siku1-3 kukauka kama inavyotakiwa.Nyasi nene huweza kuchukua zaidi ya siku 2 kukauka vizuri.
Baada ya kukauka,inashauriwa nyasi zifungwe na kuhifadhiwa juu ya chanja ambapo hazitanyeshewa au kuchafuliwa kwa namna yoyote.
Hei inaweza kutengenezwa kwa nyasi za asili au za kupandwa.Nyasi nzuri za kupandwa za kutengeneza hei ni pamoja na Rhodes na Buffel.

Screenshot_20231230-100527_1.jpg


2.Sileji (Silage)

Saileji ni aina ya malisho yaliyohifadhiwa bila kukaushwa kwa mtindo unayoyaruhusu yavunde huku yakiwa katika mazingira yasiyo na hewa ya oksijeni na hivyo kubakia na asilimia kubwa ya viinilishe muhimu kwa mwili wa mnyama atakayeila.

Saileji inaweza kutengenezwa kutokana na ziada ya malisho ambayo kwa kawaida hupatikana wakati wa mvua.Saileji pia inaweza kutengenezwa kutokana na aina nyingi za mazao yanayostawishwa kama mahindi,mtama au aina nyingine nyingi za malisho ya jamii ya mikunde na nyasi.
Mahindi au mtama uliooteshwa kwa ajili ya kutengeneza saileji hufyekwa wakati punje zake zikiwa changa kiasi cha kupasuka kwa urahisi unapozibonyeza na kutoa majimaji yanayofanana na maziwa.
Nyasi nyingine zilizostawishwa kwa ajili ya kutengeneza saileji zikatwe katika kipindi kile zinapoanza kutoa maua.Katika umri huo,mimea inayohusika huwa ina viwango vikubwa vya protini madini na vitamini.

Nyasi nyingine nzuri kwa ajili ya kutengeneza saileji ni Super napier (Pakchong 1)
View attachment 2857302

Mbegu za Super napier zinapatikana kwa sh.5000(elfu tano) kwa kg.Ni nyasi nzuri unazoweza kuvuna hadi tani 200 za majani mabichi kwenye eneo la ukubwa wa eka moja kwa mwaka.Shamba la malisho lipo Ruvu karibu na Mlandizi-Kibaha,Pwani.Karibuni wote.
View attachment 2857305

KUMBUKA:Unapotaka kutengeneza saileji kwa kutumia mtama,utalazimika kuchukua tahadhari zaidi kuhakikisha kuwa mtama huo haukatwi mapema mno kabla haujaanza kutoa maua au wakati wa ukame kwani katika nyakati hizo,aina fulani ya tindikali ijulikanayo kama "Prussic acid"ambayo hupatikana kwenye mmea wa mtama huwa katika kiwango cha juu zaidi kiasi cha kuweza kuwa sumu kwa mifugo.
Njia za kuhifadhi saileji.
Zamani wafugaji wengi walikuwa wanahifadhi kwa kuchimba shimo lakini sasa hivi zinaweza kuhifadhiwa kwa kuwekwa kwenye mapipa au mifuko maalum.

Kwenye shimo

Mara nyingi Saileji inayoharibika husababishwa na makosa katika utengenezaji.Masharti yanayotakiwa kufuatwa wakati wa kutengeneza Saileji ni kama ifuatavyo:

i) Mazao au nyasi zinazotumika zipangwe na kushindiliwa vizuri kwenye shimo ili hewa isiweze kubaki ndani yake;maji kutokana na mvua au kutoka kwenye ardhi yasiruhusiwe kwa namna yoyote kuingia kwenye shimo la kutengenezea saileji.

ii)Saileji inaweza kutengenezwa kwenye shimo au mtaro.Mtaro/shimo lazima lichimbwe kwenye ardhi isiyosimamisha maji kama vile kwenye kilima au mwinuko.Ukubwa wa mtaro au shimo hilo utategemea kiasi cha saileji kinachohitajika au kiasi cha malisho ya ziada kilichopo ambacho ndicho kitakachotumiwa kutengeneza saileji.Ili kupunguza uharibifu wa saileji unaoweza kusababishwa na udongo au unyevu unaotoka kwenye udongo,sakafu na kuta za shimo ni sharti zifunikwe kwa nailoni.Mfereji uchimbwe upande wa juu wa mwinuko wa mahali shimo lilipo ili kuzuia maji yanayotiririka yasiweze kupitia kwenye mdomo wa shimo wakati wowote.

Ili kazi ya kushindilia iweze kufanywa kwa ufanisi na hewa yote iweze kutoka kwenye shimo,ni vyema malisho yakakatwakatwa vipande vidogo vidogo kabla ya kutiwa kwenye shimo.Iwapo hewa haikutolewa vizuri kutoka kwenye malisho yaliyowekwa kwenye shimo,basi saileji itaoza na haitafaa tena kwa matumizi kama chakula cha mifugo.Iwapo hutataka kutakata malisho katika vipande vidogovidogo,basi unaweza kuyalaza kwa uangalifu kwenye shimo katika uelekeo mmoja na kuyashindilia mara kwa mara hadi shimo litakapojaa.
Baada ya kuanza kuweka malisho kwenye shimo,endelea kufanya hivyo na kuhakikisha kuwa shimo limejaa katika muda mfupi kadri itakavyowezekana.Wakati ukiendelea kujaza shimo,tembeatembea juu ya malisho uliyoweka kwenye shimo ili kuyashindilia.Ikiwa utaweza kupata molasi (molasses)basi inyunyuzie kwenye malisho wakati ukiendelea kulijaza shimo.Molasi itasaidia kuharakisha tendo la kuvunda na vilevile kukuhakikishia saileji yenye thamani kubwa kilishe.

iii)Shimo likishajaa,lifunike kwa nailoni na kisha ongeza udongo juu yake ili kuhakikisha kuwa hewa haitaweza kupenya na kuingia ndani.Muda mfupi baada ya kufunika shimo,majimaji yanaweza kuanza kuchuruzika kutoka shimoni.Hali hii ni ya kawaida kabisa.Saileji itakuwa tayari baada ya kipindi cha kati ya mwezi mmoja hadi miezi miwili.Hata hivyo saileji hiyo inaweza kubakia kwenye shimo bila kuguswa kwa kipindi cha muda mrefu.

Saileji nzuri inatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

Mara utakapofungua shimo,utasikia harufu kama ya ndizi mbivu.
Ina rangi ya unjano na ukijani.
Haina majimaji mengi.
Ni safi,bila kuwa na mchanganyiko na udongo au takataka nyingine.

Saileji mbaya itakuwa na sifa zifuatazo:

Harufu mbaya ya uozo.
Itakuwa na rangi ya weusi au weupe.
Itakuwa na majimaji mengi.
Itakuwa na uchafu.

KUMBUKA
Pembeni ya shimo kutakuwa na saileji iliyooza.
Kwa siku za mwanzo za ulishaji, ng'ombe hawataipenda sana na hivyo watakula kiasi kidogo tu.Inashauriwa kwa siku hizo za mwanzo za ulishaji,saileji ichanganywe pamoja na malisho mengine yanayopendwa na ng'ombe na kulishwa mara kwa mara.Saileji inaweza kusaidia kuongeza kiasi cha maziwa kinachotolewa na ng'ombe na haswa wakati wa uhaba wa malisho. Pia inafaa kulisha ng'ombe wa nyama hasa katika unenepeshaji.

Mapipa
Saileji inaweza kuhifadhiwa kwenye mapipa,kinachotakiwa ni kushindilia na kuliziba pipa ili hewa isiingie.

Mifuko maalum
Saileji pia inaweza kuhifadhiwa kwa kutumia mifuko maalum.










View attachment 2857298.


Maelezo haya yametokana na kitabu cha Mwongzo wa ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa
View attachment 2857299.

Ukikihitaji: 0756625286.
Soft copy/e-book.
Bei.Tsh 5000.

Heri ya mwaka mpya 2024.
 
Back
Top Bottom