Maisha yanaenda kasi sana. Ali Choki ndo yupo kule!

Mafahari wawili hawawezi ishi zizi moja. Si wakumbuka walianzishaga bendi choki,banza na muumini ila ilisambaratika vibaya mno
na ilisambaratika baada ya muda mfupi sana. nilishangaa kweli kwa wakongwe kama wale kushindwa kuelewana kiasi kile. nafikiri ndo hivyo kila mmoja alitaka kuwa juu ya wenzie
 
Mapedeshee wengi waliokuwa wanaziwezisha hizi bendi wamepigwa pini na huu utawala wa jpm.unaweza kuhusisha na kufulia kwa wanamziki hawa


Sent from my iPhone using JamiiForums
Dooh
 
wameyachezea maisha walipokua juu kimafanikio
Deo mwanambilimbi ni muanzilishi wa Twanga pepeta,lakini kwa sasa ana bendi yake na analima,anapata ugali wake vizuri tu
 
amtumikiae shetani huchakaa mwishowe.
bali amtumikiae Mungu huhuishwa roho na mwili kila iitwapo leo!

Sio kweli hakuna uhusiano, hata waimba kwaya wanachakaa hata mapadri wangechakaa pia bila sadaka za watu ishu ni kuwekeza kinachopatikana kuna viongozi wengi tu mafisadi na wanakufa na mali so acha kujipa moyo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
amtumikiae shetani huchakaa mwishowe.
bali amtumikiae Mungu huhuishwa roho na mwili kila iitwapo leo!
Wakati mwingine shetani tunamsingizia sana, upate pesa usijiwekee msingi mzuri ule bata mpaka shilingi ya mwisho ukichoka umsingizie shetani hapana! Kuna wakati hata yeye huwa anatushangaa wanadamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu wana JF, anayopitia Ali Choki, na wengine ndio mfumo mzima wa Maisha ya watanzania. Wao wanajulikana na ndio maana tunawaona kirahisi walivyokuwa sasa tofauti na zamani

Tusiwabeze ndio mfumo ulivyo. Wazazi wetu sisi wengine walikuwa wakubwa serikalini lakini leo tunachangishana watoto kuwakatia Bima za Afya hawana uwezo tena na Maisha yamewapiga wanatutegemea sisi watoto wao. Tusipojipanga vyema na sisi tutakuwa hivyo hivyo tegemezi kwa watoto wetu. Wakati ni ukuta huwezi kubaki juu milele tecnolojia inabadilika na dunia inabadilika vizazi vinabadilika.

Kuna wengi upande wa wafanyakazi na wakulima, Mapedeshee ukiwaona wamefulia tofauti na kipindi cha nyuma

SOMO MUHIMU: Ukiwa juu jitahidi kuwekeza na kujijenga ili wakati unapobadilika ubaki kuwa juu au usitetereke sana
Noma sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom