Maisha yamenishinda, vita imenishinda

Maisha yamenishinda, vita imenishinda

Mkuu pole sana na changamoto za maisha
Hayo ndio maisha yenyewe inabidi ukubaliane na ukweli kwanza, Ni heri ndugu yangu utafute njia mbadala ya kuishi
 
Nimepambana kwenye nyanja nyingi za kimaisha ila bado, nimeitafuta furaha kwa muda mrefu ila siku zangu za kuishi hapa duniani zimekuwa za mateso na maumivu,

Matatizo yako ni yako binadamu hawajali na hata hawatawaza hicho ndio kitu kikubwa nimekutana nacho, nimehangaika kwa kila namna kufanikiwa kimaisha, ila ukweli destiny yangu nimeishaijua niliandikiwa kufeli toka nazaliwa, hilo nimejua,

Sioni haja ya kuendelea kuhangaika kwenye dunia hii ambayo imeshanihukumu kwamba mimi nitakuwa mtu wa kufeli maisha yangu yote, siku za kukosa furaha na maumivu zinatosha sasa, mimi moja kati ya wanadamu ambao furaha tumegombana nayo,

Naishia hapa na hii ndio point ambayo sina budi kurudi kwa yule aliyeniumba

Ukiona kiza kimetanda sana na huoni mbele, huo ni mwanzo wa pambazuko.

Maisha bila kuamini ni bure! Sababu ktk imani tunapata tumaini na uzima.

Wale tunao amini ktk KITABU CHEUSI tunaamini kukata tamaa, kukatisha UHAI ni dhambi(Uhasi wa sheria ya Mungu).

Lakini pia Mungu alisema hatokupa jaribu ambalo hutoliweza, na akasema jaribu lolote kwetu huwa na mlango wa kutokea.

Kwa hivo muhimu kwako sasa ni kuomba usaidizi wake Atakusaidia.
 
Kitu cha kwanza katika kutafuta solution ni kutafuta na kugundua chanzo cha tatizo
Na hilo neno destiny ndio chanzo cha kwanza cha wewe kufikia hapo
Kwanza futa hilo neno destiny kwenye mindset yako.

wewe ndio kiongozi na muamuzi wa maisha yako so ukishaweka mindset ya destiny trust me utaishia kubweteka na utabaki hapohapo.

So solution ya kwanza ni F Destiny.
 
Ila maisha Yana fumbo kubwa Sana ,muda mwingine unajiuliza why wengine kila wanachogusa wanafanikiwa fasta tu ,gusa mwingine Ni majanga tu.

Mimi naamin Kuna maisha ya aina mbil ,haya ya kawaida na yapo mengine nje ya haya tunayoishi.

Mungu katufumba Sana hili fumbo ,siku ukija lifumbua utajicheka Sana na kujiuliza nilikuwa nakwama wapi?
So usikate tamaa milango yako inakaribia kufunguka ,pale unapowaza kukata tamaa kabisa na pale shida zinapozid kiwango basi jua umetanganishwa na utepe mdogo Sana wa mafanikio ,kwa lugha nyepes unakaribia mafanikio.

Ila usisahau kuomba kwa mungu .
Siku hizi ni kuloga tu
 
Wakati wewe unalalamikia maisha haya,kuna watu hawawezi hata kununua simu kama uliyonayo na kujiunga humu cha msingi ,endelea kupambana maisha hayana fomulara na wala hayana umri wa kupata,kuna wengine hupata wakiwa wadogo sana,wengine umri wa kati,wengine hata uzeeni,hujawahi ona mtu mzima kaoa kabinti na anaitwa baby🐂🙆🙆🙆🙆!mambo ya mapene hayo!
 
Nataka ujifunze kwa story yangu ndogo tu kwa uchache,
Mimi hapa ni mtu ambaye nimedhulumiwa sana katika kila kazi ninayoifanya licha ya kuwa na vipaji lukuki, ufundi umeme, ufundi finishingi za rangi, ujuzi wa computer mpaka kuzirekebisha zilizoshindikana, uchoraji, n.k,

Katika kila kazi nimejaribu kuajiriwa kwenye kampuni tofauti tofauti laki kote huko nimekuwa sipati haki yangu hata kama ingekuwa ni kazi za nyumba binafsi najikuta boss akinilipa ni pesa ndogo zingine nadhulumiwa,

Mbona sikuwahi kata tamaa kiasi hicho, yako mapito mengi na magumu ambayo sijataka kuyaandika ila nabaki kumshukuru Mungu,

Tafadhali usikate tamaa ni jambo la kusubiri muda tu, kila kitu kitakuwa sawa
 
Mtesi wa watu aliekuwa chanzo cha taabu zote hizi kafa mkuu, tuko na mama ni jembe kinoooma mambo yatanyooka soon, so jipe mda kdg usiharakishe kuuondoa uhai.
 
Watu wengi hawaelewi kuwa tumetofautiana katika uwezo wa kuhimili matatizo kutokana na experiences mtu ulizopitia katika maisha..

Unachokiona kidogo kwako kinaweza kumtoa roho mwingine na unachokiona kwako kikubwa kinaweza kuwa cha kitoto kwa mwingine

Na hii ndio sababu kubwa ya watu kujimaliza kwa sababu mtu anaona akikiri udhaifu, watu watamtoa thamani au kumzingua badala ya kumsaidia hata kama ni kwa njia ngumu ila anayoweza kuendana nayo...
Tujifunze kuelewana na kusaidiana pasipo kujilinganisha wakuu
 
Nimeandika na kufuta Mara nyingi zaidi. Nakosa lugha nyepesi ya kukushauri na kukutia moyo katika hili. Umasikini unaumiza, unachoma Sana moyo. Wakati mwingine Kila njia huziba. Tunawapoteza watu wa karibu Sana kwa kukosa namna ya kuwasaidia kifedha na kupata matibabu stahiki. Wazo langu ni hili: Usikate tamaa! Usiwe m-binafsi kiasi Cha kujiua. Kuna mtu mwingine anakuwa inspired Sana na struggles zako na Kuna mwingine pia anakuombea ufanikiwe. Jipe muda na matumaini ya kushinda. Ni wengi tunaosafiri katika barabara hii lakini ujasiri wa kuendelea huku tukiamini Kila siku inayokuja inaweza kuwa ya tofauti ndo imebaki slaha pekee. Usikate tamaa mwana,,,,one love, let's keep the fight. Kila kitu kitakuwa sawa!!!
 
Mkuu unapoona akutana na ugumu wa kiwango cha kutaka kuondoka duniani ni wakati wa kumkabidhi Mungu maisha yako naye atakuonyesha njia iliyo sahihi.

Yawezekana mapambano yako hayalandani na mazingira uliyopo. Ikiwezekana hama hapo ulipo nenda eneo jingine uangalie fursa. Watu wanaweza wasikujali, ila sio wote
 
Nimepambana kwenye nyanja nyingi za kimaisha ila bado, nimeitafuta furaha kwa muda mrefu ila siku zangu za kuishi hapa duniani zimekuwa za mateso na maumivu,

Matatizo yako ni yako binadamu hawajali na hata hawatawaza hicho ndio kitu kikubwa nimekutana nacho, nimehangaika kwa kila namna kufanikiwa kimaisha, ila ukweli destiny yangu nimeishaijua niliandikiwa kufeli toka nazaliwa, hilo nimejua,

Sioni haja ya kuendelea kuhangaika kwenye dunia hii ambayo imeshanihukumu kwamba mimi nitakuwa mtu wa kufeli maisha yangu yote, siku za kukosa furaha na maumivu zinatosha sasa, mimi moja kati ya wanadamu ambao furaha tumegombana nayo,

Naishia hapa na hii ndio point ambayo sina budi kurudi kwa yule aliyeniumba
Mods. Mtafuteni huyu jamaa apewe msaada.

Atakiua huyu kimzaha mzaha
 
Hauko peke yako man life lina songombingo zake aseeeh kaza ugoko dimbani, kuna watu wanashida zaidi yako and still they believe better days are coming, funga mgwiji ankal lets fight until the last breath
 
Wa Tz badala wasaidie utaskia wanasema
"wewe huna shida sisi tuna shida zaidi yako ila tumenyamaza tu usituone tuna furaha hapa tuna zuga tu"

Utafikiri kama vile shida ni mashindano
"Shida zako cha mtoto hujaziona zangu"
 
Back
Top Bottom