Mkalimani wa taifa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2020
- 753
- 1,290
Mkuu usijiue, usipime mafanikio ya kimaisha na umri ulionao, Mungu akitaka kukupa hakuandikii barua
Naweza kukusaidia?Nimepambana kwenye nyanja nyingi za kimaisha ila bado, nimeitafuta furaha kwa muda mrefu ila siku zangu za kuishi hapa duniani zimekuwa za mateso na maumivu,
Matatizo yako ni yako binadamu hawajali na hata hawatawaza hicho ndio kitu kikubwa nimekutana nacho, nimehangaika kwa kila namna kufanikiwa kimaisha, ila ukweli destiny yangu nimeishaijua niliandikiwa kufeli toka nazaliwa, hilo nimejua,
Sioni haja ya kuendelea kuhangaika kwenye dunia hii ambayo imeshanihukumu kwamba mimi nitakuwa mtu wa kufeli maisha yangu yote, siku za kukosa furaha na maumivu zinatosha sasa, mimi moja kati ya wanadamu ambao furaha tumegombana nayo,
Naishia hapa na hii ndio point ambayo sina budi kurudi kwa yule aliyeniumba
Hata mimi nimeshangaaDuuh huyu memba toka 2010 hadi leo anapost moja tu ambayo ndio hii
Kuna jamaa ameni quote kua jamaa alikua bize, sijamuelewa kwakweliHata mimi nimeshangaa
Nashukuru sana mkuuPole mkuu
Mkuu usijichukulie kuwa wewe ni wa kufeli kwa sababu utakapofeli tena hata kidogo tu, utaiaminisha akili yako kuwa umefeli kwa sababu wewe ni wa kufeli pasipo kuangalia zile siku unazofanikisha chochote hata kiwe kidogo namna gani ila hurudhiki nacho sababu unajilinganisha na wengine..HUTORIDHIKA KAMWEEE..
naelewa sio rahisi, ni ngumu kupita kiasi na inavunja moyo sana
ila unakufuru kwa kudhani kuwa pumzi yako haina thamani au upo peke yako unaepitia hali hiyo
usishangae wengi tu tunafeli sometimes, lakini tunajikokota hivyo hivyo hata kama moyo unavuja damu na nguvu zimeisha mwilini..
tunatoka hivyo hivyo na tunapita mitaa ile ile tunaonyooshewa vidole na kuwasiliana na watu wanaoona hatuna thamani yoyote japo ni ndugu, marafiki au hata wazazi.. Yes IPO HIVYO
kiubinadamu inauma lakini tukijiwazisha na kujiumiza kwani itasaidia kitu!!!..
HAPANA, ndio maana tunaamka daily tukijua haya maisha ni jukumu letu tu pasipo kutegemea kutiwa moyo, kujaliwa au kusherehekewa na watu wengine..ikitokea tunashukuru na isipotokea bado tunaendelea.. KUBALI HILO TU
Mungu akusaidie Mkuu upate nguvu ya kutokata tamaa na kuamka tena. naamini utaweza tena