Maisha ya ubachela ni vituko

Maisha ya ubachela ni vituko

Huo sio ubachela ni uchafu ubachela na uchafu ni vitu viwili tofauti!
 
Mimi situmii chandarua wala dawa ya mbu lakini sijawahi hata kuumwa na malaria. Huyo mbu ndani anaingia kutafuta nini wakati kutwa mlango umefungwa na akikaa lazima afe mwenyewe kwa njaa.
Sikutaka kusema haya usemayo kwasababu utaambiwa unajidai.
 
Kuna ishu ya kutandika kitanda
Uwaga asubuhi unakurupuka unaacha kitanda ivyo ivyo, ukirudi kutoka kwenye mishemishe zako ndio unatandika au wakati wa kulala
 
Swala la kufanya Tishet kua taulo nalifanya sana mkuu


Ukweli mtupu,
ubachela nikuskia njaa ndo kuanza kupika ni ngumu sana kwanza kwangu haijawahi kutokea napika sina njaa au unapika mchele kilo mbili ili uwe unapasha tu kila unaposkia njaa mboga nayo kama sio mchemsho wa nyama basi ni mayai yamekaangwa wengine maharage tunanunua yaliopikwa jero tu afu unayaunga nyumbani.

Viombo vinaoshwa wakati wa kupika tu siku ukibaki home ndo unaosha viwe visafi.

Demu mpya akija ghetto linakua mbingu ya saba clean as f*

Taulo likichafuka ndo story yake imeisha linakua dekio au kutupwa. Hapo tshirt na mashati yanageuzwa taulo

Wanawake ni muhimu sana tuacheni masihara. Tena ka ulikua unakaa na dem ushazoea anarekebisha kila kitu akiondoka tu wiki ya kwanza utamaintain ya pili aah wapi hamna kitu unarudi kule kule.
 
ubachela unapika ugali mara mbichi
Huko ni kutojua kupika wala si ubachela,...
Hii inatokana na malezi ya nyumbani kwani.... mlizoea kufanyiwa na wafanyakazi au wanawake tuu sasa mnateseka,,.,,,
 
Haya maisha ni shida sana siku moja me nilienda kabisa kununua unga wangu na dagaa mchele wangu nakasema leo sili kwa mama ntilie, niwasha jiko langu la mafuta ya taa nikaweka sufuria kabisa aisee, kuja kukumbuka hivi kumbe sina mwiko wa kusongea ugali aisee, nilichofanya nikaenda tu kununua mkate nikala na dagaa mchele wangu yale maji nikayageuza chai tuu, yaan ni vituko juu ya vituko tuu
 
Wanaosema ni uchafu nakataa inategemeana na kazi gan unafanya kuna kazi unarudi home upo hoi.

Siku unajikaza unafua kama nguo za wiki 2 halafu kamba inakatika.

Kutupa mwiko ni jambo la kawaida kuna mtu alinipa mbinu imenisaidia sana baada ya kusonga ugali tu osha mwiko ukiacha ukaukie umetupwa huo.

Kwenye soksi hapa kurudiwa ni jambo la kawaida unafukua tenga la nguo chafu tu na kukagua soksi ipi inanafuu inarudiwa hiyo.

Kunasiku nimebandika mboga inayotembea nyama kujiegesha kidogo nimelala kuamka nyumba nzima inanuka moshi wa nyama..hahaa
 
Kuna siku maji yamekatika ndani kumbe nimefungua maji nikaacha tap wazi maji kurudi Karo limeziba nimeweka sufuria hapo kurudi nyumba imegeuka bahari ya shamu aloo nlipita juu ya maji nikachukua begi nikaondoka kwanza kwenda mkoa mwingine kurudi ndo nikaanza kuchota yale maji ndani.

Wali kuliwa wiki sio jambo la ajabu.

Vimfuko vyeusi vya chips kujaa ndani sio jambo la ajabu.

Ila kupika saa 6 kawaida sana natabia ya kutoka kazini nikifika nalala kuja kuamka saa 4 usiku ndo nafikiria ntakula nn.

Kujifanya unakula mchemsho kila siku kumbe uvivu wa kupika

Ubachela hatari
 
*Fahamu maisha ya ubachela*
Maisha ya ubachela unaweza kuloweka sufuria ulopikia ugali likakaa na maji wiki nzima yakianza kunuka unamwaga halafu unaweka tena maji mengine..



Sasa wewe wa unga kuishia kati, kwani wakati wa kupika hupimi unga na maji kuona kama vitatoshana, haki nyie watu...lol!

Hahahha Mara unapika wali unatoa kitu bokoooo.au ugali unapika Mara unga unaisha .inakua haielewek ni uji au ugali
 
?0
Hahahah karoti za kuunga mafuta ilikuwa mboga kuu . wiki nzima ugali na karoti. Samaki ni marufuku Kununua wale wa kubwa.

Kuna tule tudogodogo unakuta fungu LA samak 10 kwa jero...hahahahaha. Mtaa wa kiboloroni raha sana. Mchele ni robo na hauna mboga. Unapika na nyanya kabisaaa huo wali. Unatoka unanukia nyaya...ni balaa.

Siku moja nililetewa maziwa ya mgando ila yalikuwa na maji.
Nikatoa yale maji nkapikia ugali ili nisave mboga.....hahahahah ilishindikana nikamwaga.....

Lazima macho yako mazuri sana, cos sio kwa kula mboga na carrot kiasi hiki!


Acha uzembe wewe, tafuna mboga na ratiba nyingine zifuate


unamshauri kabsa!

Poleni sana kapelas!
 
Back
Top Bottom