Maisha ya ubachela ni vituko

*Fahamu maisha ya ubachela*

Maisha ya ubachelor unaweza kujishaua kufululiza kupika msosi hata mwezi mzima ila vyombo visafi vikiisha ndani unarudi kwenye utaratibu ule ule wa kula chipsi na paja la bukujero.Maisha ya ubachela kila siku tunapoteza vijiko kidogo kidogo kwa kumwaga maji ya ukoko wa ugali.

Maisha ya ubachela unaweza kuloweka sufuria ulopikia ugali likakaa na maji wiki nzima yakianza kunuka unamwaga halafu unaweka tena maji mengine.

Maisha ya ubachela mara nyingine neti hugeuka kuwa hema.Ikichomekwa haichomolewi mpaka siku utakapopata mgeni.

Maisha ya ubachela hufika kipindi mtu unageuka mbwa, unanusa kwanza nguo ili ujue kama unaweza kuipa round ya pili au hapana.


Ubachelor mtamu sana, Ngoja niendelee kuufaidi hadi 2025.
 
Hahahha Mara unapika wali unatoa kitu bokoooo.au ugali unapika Mara unga unaisha .inakua haielewek ni uji au ugali
 
NOMA SANA nami nitafika huko tu.. ila nikitaka kufua silogwi kuiliweka maana hua inatoa hadi vidudu mwishoni inaenda jalalani..

Kiss daniel namkubali sana salam zake zimefika..
hahaaaa nimepitia huko...
by the way msalimie Huyo kiss daniel
 
Kuanza kupika saa 4 ya usiku
Hahahahah umenikumbusha mkuu enzi hizo hostel, watu wameshalala saa sita ndo naanza kuwasha jiko. Kama ni maharage nayatenga saa mbili/tatu night. Muda wangu wa kula ni menu litakapokuwa tayari. Sasa nimeshazoea kulala mida mibovu, hata kama sina company, sichat, na sina kazi yoyote nalala mida ya wanga tu.
 
Back
Top Bottom