Maisha ya ubachela ni vituko

Maisha ya ubachela ni vituko

Kuna vile vidawa vinauzwa 200 wengine huwa wanachoma kwenye moto,,lakin kuna vifaa vyake vinauzwa 10000 vingine 5000,,,unachukua hiyo dawa unaiweka kwenye hiyo kifaa kisha unachomeka kwenye soket ,,dawa inatoka taratibu inaua mbuu,,na hakuna harufu
Okay hicho kifaa ungejua kinaitwaje ndio ingekuwa poa zaidi ili uweze kukitafuta kwa urahisi huko madukani bila kujieleza saana
 
Daaaaah huyu jamaaa kaniweza asee huyu ni Mimi kabisa daaah
 
Hahaaaaa mkuu umenikumbusha mbali sana
 
Okay hicho kifaa ungejua kinaitwaje ndio ingekuwa poa zaidi ili uweze kukitafuta kwa urahisi huko madukani bila kujieleza saana
IMG-20171208-WA0006.jpg
 
Aisee mboga yangu ni samaki tu ata mwezi mzima, ndio mboga rahis kwa wali,ugali, na tambi
 
Bachila kula suti kawaida sana anapika wali hana mboga anawahi maziwa ya Tanga Fresh kwa mangi au ugali maziwa mtindi hahahaaa ubachila kiboko mboga ya majani inakatiwa kwa Mama muuza
 
1. Niliwahi kuloweka nguo kwa siku 4 hadi wapangaji wenzangu wakajua naumwa siwezi kufua.
Nilizitoa hapo nikazisuuza bila kufua tena nikazianika juani.

2. Niliwahipika ugali mara paaah mbichi, nikaenda mgahawani kutafuta chakula.

Ila kwa sasa naweza kupikapika kiasi changu.
 
Kuna tofauti kati ya kuwa MCHAFU na kuwa bachelor. Mambo yote uliyoyasema hapo juu ni dalili ya mtu mchafu sana na asiyejielewa na kama hayo ndio maisha yako my brother sio sifa nzuri hata kidogo.
Naona povu kwa mbaaaaaali linakuja kuja anyway ngoja nivute stuli na karanga nisubiri nione nini kitatokea.
 
Burudani zaidi ni pale unapoamua kuanza maisha ya ubachelor halafu ukafanikiwa kununua kila kitu unachokihitaji kwa siku ya kwanza lakini ukasahau kununua mwiko au kisu
 
Back
Top Bottom