Hivi Yesu alipo mwambia Petro kuwa lolote utakalolifunga Duniani litakuwa limefungwa Mbinguni na lolote utakalolifungua Duniani litakuwa limefunguliwa Mbinguni,rejea Mathayo 16:19,Je Petro hakuwa Mwanadamu?Je Petro alikuwa Malaika?,Au basi jiulize mwenyewe badala ya kujivika blanketi la Ujinga ktk Yohane 20:22-23,Kwanini Yesu aliwapa mitume Uwezo wa kuondolea watu dhambi ili hali wao ni Wanadamu na wana mapungufu yao?,Tatizo lenu ninyi ni Uzuzu ndo unawasumbua sasa mimi nikienda kwa Papa au Askofu au Padre wangu nikaungama dhambi zangu wewe inakuuma nini?,Fuata yako bhana!,kila siku Midomo wazi kupiga umbea mambo yasiyowahusu.Mbona sisi habari za Wachungaji wenu kujifanya miungu hatuzisemi?Wapo wachungaji wanajiita Ma-transformer mbona hatuwasemi?,Wapo wanaojiita wazee wa kufufua watu cha ajabu watoto wanafia makanisani mwao,mbona hatuwasemi?,Wengine wamezaa na waumini wao mbona hatusemi?,Hivi bora yupi hapo,Anayefanya mambo kwa kufata Biblia au yule anayejitungia ya kwake?,Mkuu makinika sasa Kanisa Katoliki linaongozwa na Roho Mtakatifu,ndiyo maana halitakuja lianguke hata siku moja.