hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,683
- 27,605
Kardinali Müller anasema
“Inapaswa kusemwa wazi kwamba hakuna mtu aliye na haki ya kumkosoa Papa pale anapofuata kwa uaminifu utume alioupokea kutoka kwa Kristo wa kushuhudia Injili ya amani.”
Hayo ni maneno ya kardinali Muller
Mimi nasema ,kama Mungu anatukanwa, na Bwana Yesu mwenyewe alipingwa na kutendewa jeuri, Papa Leo XIV ni nani hadi asihojiwe?
Hapa ndipo hatari ya kumpandisha mwanadamu mahali pa Mungu inaanzia. Je, Müller anataka kurudisha zama za giza—nyakati ambazo kumkosoa Papa ilikuwa sawa na hukumu ya kifo? Jambo ambalo Waprotestanti hawajasahau madhira hayo. Au tuseme Muller ana jaribu kutetea fundisho la infallibility (kwamba Papa hakosei)?. Fundisho ambalo lilijaza damu Ulaya na kupelekea mpasuko mkubwa wa kanisa la Katoliki?
Kwa kauli kama hizi, angekaa kimya kuliko kuongeza mafuta kwenye moto. Tayari nchini Marekani baadhi ya Waprotestanti wameanza kuamka, wakimpinga Papa huku wakimtetea Trump kwa kurejea historia. Hata bunge la Seneti limepiga kura kumpa Trump mamlaka ya kuendelea na vita dhidi ya Iran.
Ikumbukwe pia, Papa si tu Askofu wa Roma bali ni kiongozi wa nchi ya Vatican. Hivyo anashika pia mamlaka ya kisiasa. Na pale siasa zinapohusika, kukosolewa si chaguo—ni haki ya msingi kwa yeyote asiyekubaliana naye.
Makasisi wasijisahau. Kabla ya mwaka 1981, Vatican na Marekani hazikuwa na mahusiano ya kibalozi bali uhasama.
Mahusiano hayo ya kibalozi yalirejea kupitia rais Ronald Reagan na Pope John Paul II, si kwa sababu ya umoja wa kiroho, bali kwa kuwa walikuwa na adui mmoja—USSR.
Izingatiwe kwamba Papa Leo IVX kumkosoa Trump sio tatizo maana anayo haki ya kutoa maoni ila shida ni hao wasio taka Leo ajibiwe ama asikosolewe.
Pia soma > Trump: Papa Leo XIV ni dhaifu, simshabikii
Muller ni nani?
Ni Kadinali wa Kanisa Katoliki kutoka nchini Ujerumani (alizaliwa mwaka 1947).
Alikuwa Mkuu wa Baraza la Mafundisho ya Imani (Congregation for the Doctrine of the Faith) kuanzia mwaka 2012 hadi 2017. Huu ni moja ya nyadhifa zenye nguvu zaidi Vatican baada ya Papa, kwani kazi yake ni kulinda usahihi wa mafundisho ya kanisa.
Anachukuliwa kama mmoja wa wanatheolojia (wasomi wa mambo ya Mungu) bingwa duniani, akiwa mwanafunzi wa karibu na mfuasi wa fikra za marehemu Papa Benedikto XVI.