fimboyaasali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 8,598
- 8,172
Hiyo sio kazi ya serikaliWakuu habari za jioni? Wiki hii Nilikuwa DODOMA kwa shughuli za Kiofisi,nimependa jinsi jiji la Dodoma linavyokua kwa kasi,Lakini hali ya maisha inaonekana ni ngumu Sana kuliko Dar es salaam.
Nilitafuta guest house, bodabo whyda akaniambia kuwa vyumba vya bei ya chini ni 20,000/=, nikashangaa Sana kwasababu niliwahi kwenda DSM na nikafanikiwa kupata gesti ya 10,000/=, nzuri tu. Chakula kwa Dodoma ndo usiseme,kipimo changu cha kwanza ni kwa Mama ntilie, maana watu wengi wa hali ya chini huenda huko kununua chakula;
Aise kina bei hatari , Kuna sehemu niliambiwa wali nyama 3,000/=,Ugali nyama 3000/=,Wali samaki 3500/=, Ugari Maharage 2000/= na wali Maharage 2500/=, Sehemu nyingi za Mama Ntilie bei ni hizo.Nilipolala ni karibu na Holly Cross Center inayomilikiwa b
Na Kanisa Katoliki Jimbo kuu la DODOMA,Aise hapo kitimoto ya kukaanga kilo ni 10,000/=,Ya kubanikwa ni 12,000/=,Ndizi moja 500/=. Ugari kuku robo 6000/=. Na vyakula vingine bei zipo juu pia.Haya nikasema Niulize Vipi kuhusu nyumba za kupanga?; Kheee!, Bei nilizotajiwa nilishangaa Sana.Twende Bodaboda aisee Hivi kweli kutoka Holly Cross Center hadi Mkonze mtu anaanza na 6000/=baada ya kuvutana Sana ndo anaishia kwenye 4000/=.
Sijauliza viwanja.Nastaajabu kwasababu miaka ya Nyuma DODOMA haikuwa ghali kiasi hicho.Nilijiuliza swali moja kuwa DODOMA ni wafugaji wazuri wa mifugo sasa Kwanini bei ya Nyama ya ng'ombe ipo juu hivi?? Mnazidiwa na Morogoro ambao hawafugi km ninyi kweli?
Serikali ichunguze Hali hii, kwasababu inachangia kwa kiasi kikubwa sana Watumishi wa wizara waliokuwa wamehamishiwa DODOMA kutoka Dar kutamani kurudi Dar kuliko kuishi DODOMA.Tafadhari Serikali inusuru Hali hii.
Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app