Maige aichana serikali ya JK

Maige aichana serikali ya JK

Uswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,204
Reaction score
627
Aliyekuwa waziri wa JK ambae alitoswa kwenye reshuffle, akichangia bajeti ya wizara ya nishati na madini amesema


  1. mawaziri wanaofanya maamuzi wako hatarini sana kwa sababu kama maamuzi yataenda kinyume na maslahi ya mafisadi basi inaweza ikala kwa waziri

  2. akimpa ushauri naibu waziri masele, amemwambia aende kahama kurekebisha mambo maana huko vitalu wamepewa mabwenyenye ila awe makini maana maauzi ya kutetea wanyonge yana gharama zake, na ushahidi upo na akamaliza kwa kusema 'najua wewe ni mtu mzima, nafikiri utakua umenielewa!'
 
Maige kama vile Karai la magamba lililotupwa baada ya nyumba kukamilika.
 
Huyu nae ni majeruhi wa siasa chafu....aende zake huko!!
 
Mbona alikuwa hasemi akiwa ndani?......huo ni utoto tu...wana ccm waache unafiki.

Hata anne kilango akikosa ubunge utamsikia atakavyoanza kubwabwaja kuhusu serikali huku kipindi hiki anatetea madudu.....
Ccm chama cha kinafiki sana
 
Maige huna aibu, na wewe unakemea wala rushwa. Mpaka leo hujawaeleza watanzania dola 700,000 US$ za kujenga hekalu Mbezi beach ulizipata wapi!!! Twiga wetu walipita KIA. UMEPATA WAPI MORAL AUTHORITY ! SHAME UPON YOU!!!
 
Kweli hii nchi ya vipofu yan hata wezi wanatoa wasia
 
Mwacheni aweweseke na kwa kuwa ushahidi wa madudu yake upo asubiri pingu tu.
 
Kwa mujibu wa taratibu zetu yeye sio fisadi tena kwani alishatoka kwenye uwaziri.na amesamehewa kama el,chenge na wengine
 
hata mimi nimemshangaa EM kwa kukemea ufisadi. Maige tafadhali unatupa majaribu, ni afadhali ungekaa kimya maaana wewe ni fisadi No. 1
 
kusaidia mwizi kuiba au kutokuzuia wizi unakuwa mwizi automatically.
 
Kwa mujibu wa taratibu zetu yeye sio fisadi tena kwani alishatoka kwenye uwaziri.na amesamehewa kama el,chenge na wengine

na kwa mujibu wa kanuni zetu, waziri akikwakupua lakini ule mkwapuo ukawa haujazidi mikwapuo ya mtoto wa kigogo, huwezi kumuita huyo waziri fisadi, kwa waheshimiwa naomba tuelewane hapa. . . hahahaaa!
 
Maige huna aibu, na wewe unakemea wala rushwa. Mpaka leo hujawaeleza watanzania dola 700,000 US$ za kujenga hekalu Mbezi beach ulizipata wapi!!! Twiga wetu walipita KIA. UMEPATA WAPI MORAL AUTHORITY ! SHAME UPON YOU!!!

Mkuu nikurekebishe kidogo, sio kujenga ilikuwa cash za kununua hekalu!
 
Jamani muacheni atoe la moyoni, atakuja kusema tu kwamba hata yeye pale wizarani waliomponza ni akina fulani ambao walikuwa na wakubwa huko mbele, lakini ukweli ni kwamba hakufanya mazuri sana hususan ikizingatiwa na kiwango cha dolla kilichojenga nyumba yake mbezi beach.
Maige ni bora uendelee kunukuu vifungu vya bible ili kujionesha kuwa ukikosa ubunge utafungua kanisa lako na kuingiza fedha za sadaka.mu
ngu ibariki tanzania.
 
Back
Top Bottom