MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,588
- Thread starter
- #81
...kiukweli, maisha yamejaa suspicious minds/looks kila mahala unapokwenda. Ni vile weye unavyoweza ya balance maisha yako na kuji adapt haraka haraka na changes.
Challenges huanzia pale;
---mtoto anapowatambua watu wa nyumbani, na kuwa 'mtoro' kwa asiowajua...
---unapopelekwa shule kwa mara ya kwanza, kuanza kujenga urafiki na wanafunzi wenzio, kumzoea mwalimu nk
---unapohamishwa shule/kuingia shule mpya i.e sekondari...unakutana na wanafunzi wapya nk
---unapoingia chuo/vyuoni nk...
---unapoanza kazi/unapobadilisha kazi...kujuana upya na wafanyakazi wapya...nk
Hizo challenges zote ulizopitia na kufaulu ni ishara kwamba ni wewe mwenyewe unashikilia funguo za maelewano,
vipi unataka jamii inayokuzunguka ikuchukulie. Ukiamua kujiweka mwenyewe mwenyewe jamii itakutenga tu.
Ukijifanya too intruisive, jamii nayo itakuchukulia hivyo na kuwa na tahadhari nawe.
La msingi, jiwekee mipaka...nini la kuongea, nini la kutokuongea.
Nini la kufanya, nini la kuliepuka. Tangu mwanzo unajifunza lipi la kujenga,
lipi litabomoa. Hakuna formula ya kuishi na watu kwa jinsi ya mitazamo yao
La msingi, be yourself.
Mke/Mume, ana nafasi kubwa kukusaidia mawazo/maoni ufahamu wa ndugu zake,
Akili kichwani mwako kuhakikisha nawe unatumia busara zako jinsi ya kuishi nao.
Kumradhi, nimepita kuwasabahi tu dada zanguni...hii sredi imekalia ki kitchen party zaidi..lol..
Mbu aksante sana kwa huu ushauri wako. Nimefurahi kuona kumbe ukiwa wewe kama wewe no matter what happens you are yourself inasaidia. I tried that approach sometimes back but nikawa najishuku tu mwenyewe kuwa may be am not doing it right (Kwa watu wengine tu jamiini na si mawifi au wakwe zangu maana hawa hawakuwa na tatizo kabisa)
Ila your last sentence imenigusa. ...... Mbu umesema wote Mke na Mume wana wajibu wa kuyaongoza haya mahusiano....................limenijia wazo ambalo wewe ndio umeliinstigate ..............inapotokea mke wako anakuwa na clashes na Mkwe/wifi yake how do you (kama mume/kaka/mtoto) solve this ili usionekane unapendelea?
Aksante BaK hapa umetuchambulia vizuri kabisa.......hivi Mwanaume anayeishi ndani ya nyumba ambayo mkewe na in-laws wake wanaclashes zisizokwisha huwa anajisikiaje na which- if I may ask- is the best approach kwa yeye kuletewa mashtaka na kuyaelewa? je mume huyu anapaswa kupata mashtaka kutoka kwa mke au inlaws wa mkewe? na inapotokea mmoja wapo anaku'shtakia' ni approach gani ambayo ni nzuri kuichukua ili usi'haribu' pande mojawapo?Unayosema ni kweli kabisa, lakini inakuwa ngumu mno pale mke anavyojitahidi kadri ya uwezo wake kuwa karibu na wifi zake na mama mkwe lakini bado juhudi zake hizo zisizae matunda yoyote ya kuwa na uhusiano mzuri kati yao. Nayasema haya kwa kuwa nimeshayashuhudia mara nyingi sana na inafikia wakati mke inabidi anyooshe mikono juu na kukubali kushindwa kwamba hawezi kuwa uhusiano mzuri na mawifi zake na mama mkwe. Hawa mawifi na mama mkwe mara nyingi humuona huyo binti "anafaidi sana" au "anamuendesha" mumewe.
Mama Wakwe na Mawifi kama hawatataka kuifuatilia ndoa ya mume (mtoto na kaka yao) labda kila siku iendayo kwa Mungu (Wamekula nini, kamnunulia kanga zipi, kamnunulia gauni la namna gani bei gani, viatu vyake mbona ni ghali mno n.k.) labda hii itasaidia kuwepo na uhusiano mzuri vinginevyo ni utata mtupu ambao unaweza kabisa kuivuruga ndoa hiyo na kuitia dosari kubwa sana na si ajabu kuvunjika.
Pia wapo wake wakorofi ambao mara nyingi hawataki mume asaidie upande wake hata kama ana uwezo mkubwa wa kufanya hivyo, hawa pia wakiacha hii tabia mbaya basi labda kuna uwezekano wa kuwa na "uhusiano" mzuri.
Kwa kweli tuongee ukweli akina dada kabla ya kuolewa huwa mnakuwa mna adabu sana na mnanyenyekea sana.
Sijui ile inakuwaga ni nidhamu ya woga wala sijui ili upate dili la kuolewa na bro au dogo.
Mambo yanabadilika mkisha ingia ndani ya nyumba kuwa miongoni mwa familia yetu dahhh hapo vitimbi na misuguano huanza.
Kama wewe dada ni mnoko au jeuri kwa nini usijionyeshe tu toka mwanzo tujue shemeji yetu mnoko mkiwa katika harakati mnajivika ngozi ya kondoo mkisha zama ndani ndo mnakunjua makucha yenu sasa mashemeji na mawifi wanabaki mdomo wazi hivi ndo huyu huyu kweli aliyekuwa anatuheshimu?? Hapo bado biti la kuwekewa kikwazo cha uhuru wa kwenda kusalimia kwa bro. dahhh
Jamani Fide, sio mara zote bana........sometiomes mke anakuwa innocent kama alivyoingia bali unajikuta anabadilishwa na mambo yalivyo (sisemi ni sawa)