Mahusiano na Wakwe/Mawifi Nini kifanyike?

Mahusiano na Wakwe/Mawifi Nini kifanyike?

Mambo haya hayana fomula kabisa,unaweza kuwa ww mtu mzuri unaheshimu sana ndugu za mumeo na mama yake na baba pia ula wao wanakuwa wanajihisi sana kwamba maybe unafaidi sana kuwa na ndugu yao

Cha muhimu ww jutahidi kufanya yote mazuri kama vile kwa ndugu yao no matter wao wakoje hiyo itasaidia kujijengea trust kwa mumeo, then ukiona imezidi sana fanya unaloona linakupa amani, ila pia kuna wake wengine wachoyo sana hata kwa mama mkwe wake, hawa nao sijui tuwaweke kundi gani
 
Aksante ninashukuru kwa uwazi huu........... mh lucky she is!!

Just curious Mbu........................inapotokea Mume akijua kuwa Mama yake au dada zake huwa ni watata!! should it be part of the 'pre-marriage/coutiship-go tell- information' package au akae kimya mpaka litokee (kwa kuamini kuwa huwenda huyu wa sasa atabahatika kupata 'kibali' mbele zao?...... the same kwa mwanamke iwapo anajua kabisa kuwa ana dada au mama ambao wana tabia ya kuwascorn wakwe zao aseme mapema kama tahadhari au asubiri likitokea?

...lol, ...kama utabiri wa hali ya hewa...'hali ya bahari itakuwa na mawimbi kiasi, pepo za pwani zitavuma tokea kusini kuelekea kaskazini aka kusi!'...kwakuwa nakupenda, kukupa utabiri ni muhimu.

hahahahha muhanga umenichekesha naona umeamua kulipasua jipu pwaaaaa. Umenikumbusha MTM alishawahikiri hapa kuwa kuna rafiki ambaye alipokuwa akiwa naye mambo yake yalikuwa yanakwenda poa kabisa, yaani yeye maisha yalikuwa ya raha raha tu (kama sikosei ni ile thread ya whether ni kweli kuna wanawake wenye nyota njema au la) sasa sijui ndo hii nyota unayoizungumzia hapa?! Mwe

Mbu utanisaidia hapa au ndo yale ya Radhi ya mke?? ....Mheshimiwa tafadhali nisaidie majibu ya hili swali la nyongeza!

...hapana Mwj1 wangu ee,...hayo mambo ya kutizamia nyota sijui nyota ya mke haing'ari kwetu/kwangu mie huo ni ushirikina!..Mwiko wallah...Love Conquers All!

yoyote tu, muhimu iwe imejaa tu na ukila inarambika. sipendi sahani zilizozeeka na kufanya ufa.

bek to ze topik: kwa ninavyowaelewa dada zake Mbu nadhani unahitaji kujifunza mipasho kabla kuvalishwa pete na Mbu. lol

Lol....huyu solicitor wangu hafai hata kidogo, Lawyer gani ana disclose confidential information hadharani namna hii?
hii ni ku breach my statutory rights bana. Acha Mwj1 aingie mwenyewe apime ipi itamsumbua, ukali wa mng'ato au muwasho!

Anyway, mtoto wa kitanga aminia...huna haja ya Jahazi la Mzee Yussuf wala la Isha Mashauzi.
Ji imbie ule wimbo wa Khadija Kopa - ♪ "TX Mpenzi Dokta wangu jamani....Ananipasua ndani....!" ♪
kila ujipitishapo mbele ya mkweo na wifi zako,...lol...!
 
...lol, ...kama utabiri wa hali ya hewa...'hali ya bahari itakuwa na mawimbi kiasi, pepo za pwani zitavuma tokea kusini kuelekea kaskazini aka kusi!'...kwakuwa nakupenda, kukupa utabiri ni muhimu.

Lol habari muhimu ..........aksante. I take it kuna kuchuja pia hapa, habari muhimu kwangu mie kuzijua maana kwa siwe wenye midomo mipana mara nyingi tunajisahau tunasema habari zote halafu baadae zinabackfire mambo yanapokwenda mrama. So I agree with you na umuhimu wa kutafakari na kujua lipi ni MUHIMU kwa mwenzi wako mtarajiwa kujua juu ya familia yake mpya na lipi la kuacha.

...hapana Mwj1 wangu ee,...hayo mambo ya kutizamia nyota sijui nyota ya mke haing'ari kwetu/kwangu mie huo ni ushirikina!..Mwiko wallah...Love Conquers All!

................Lol ......haya bana so hakuna cha nyota ya mke wala nini ila kama nimekuelewa vizuri ni kuwa palipo na LOVE na baraka zinakuwepo na kuendelea kumiminika as long as that LOVE inaleta amani ndani ya nyumba.

Lol....huyu solicitor wangu hafai hata kidogo, Lawyer gani ana disclose confidential information hadharani namna hii?
hii ni ku breach my statutory rights bana. Acha Mwj1 aingie mwenyewe apime ipi itamsumbua, ukali wa mng'ato au muwasho!

Anyway, mtoto wa kitanga aminia...huna haja ya Jahazi la Mzee Yussuf wala la Isha Mashauzi.
Ji imbie ule wimbo wa Khadija Kopa - ♪ "TX Mpenzi Dokta wangu jamani....Ananipasua ndani....!" ♪
kila ujipitishapo mbele ya mkweo na wifi zako,...lol...!

Hah kusema ukweli jana Klorokwini alinichekesha sana............lol huyu ndo anafaa kuwa Best Man Mbu what do you say? Maana ni mkweli kupitiliza!
Lol hiyo sasa si utakuwa unanipa bichwa nsijekwea kilele cha mnazi nkajisahau kisa Mume kanithamini! Akhu mipasho mie hapana..... Kama Mama MwanajamiiOne sijawahimuimbia wala kumwekea asikilize, why nimwimbie Mamake Mbu au dada zake? hahaha but nimeelewa hapa ulikuwa unamaanisha nisiwe na shaka au siyo?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mahusiano haya mnayoyazungumzia yanahitaji mambo matatu muhimu:
1. Upendo wa dhati
2. Akili
3. Historia

1. Bila upendo wa dhati kwa mumeo/mkeo na kutambua kwamba ndugu zake ndio amekuwa nao na hata kama hawakupendi au hauelewani nao, maisha ya ndoa yatakushinda. Wengi tunapenda kushindana na ukweli huu.

2. Akili ni jambo la muhimu sana. Akili zinakusaidia kuchanganua na kufahamu mwelekeo wa uhusiano na namna unavyotaka uhusiano uende. Akili zinasaidia kuchuja yale unayopaswa kuyafanya. Usipotumia akili yako katika mahusiano yako, uwe ME au KE, unacheza pata potea. Wengi wanaendesha maisha yao kwa 'emotions' na ndio wanaoumia sana pale inapotokea matatizo.

3. Napenda nizungumzie historia kama sehemu nyingine muhimu. Wengi wanaingia ktk mahusiano na kujifanya ni watu ambao hawajawahi kugombana na watu ktk maisha yao au hawajawahi kupishana na watu. Hulka hii huiangusha ndoa nyingi. Historia yako ya mahusiano yako na watu baki, ndugu zako na marafiki zako ina uzito sana ktk namna unavyoweza kutatua tatizo au ugomvi wowote unaotokea kati yako na shemji/wifi zako. Kama ulikuwa mropokaji tegemea hilo, kama ulikuwa unasusa tegemea hilo, kama ni mlipizaji tegemea hilo. Sasa iweje leo uanze kulialia eti unaonewa? Kwenye ugomvi wowote lazima kuwe na pande mbili na kila mmoja anachangia kulifanya tatizo liwepo.

Nina mawifi na mashemeji kedekede na kila mmoja ana personality yake so it does not bother me na siku zinaenda . Hatujawahi kushikana wala kusemezana. And am happy and they are happy.
 
Mahusiano haya mnayoyazungumzia yanahitaji mambo matatu muhimu:
1. Upendo wa dhati
2. Akili
3. Historia

Sawa kabisa BiMkubwa akisante kwa kuileta hii perspective. Wengi tumekuwa tukiisahau na kuichukulia negative. Yaani kukiwa na clashes ile chuki, hacra inaziba hata uwezo wetu wa kuchanganua mambo na kuangalia hapa uishi vipi, pale ukae vipi, lipi uliseme, lipi ulichukulie maanani na lipi la kulipotezea. Unajua sometimes hizi clashes hutokana na vitu vidogo sana ambavyo tunavikuza kwa sababu tu tayari kuna ile tension ya 'Mama-mkwe/wifi mkorofi'

Nakumbuka kuna wakati mzazi wangu alikwaruzana na bibi (Bibi yangu alikuwa mtata hasa, yaani utafikiri alikuwa mke mwenza kwa mama yangu) siku hiyo alimrushia mamangu maneno kiasi kwamba hata mie ikaniuma sana. Mama akashindwa kuvumilia naye akawaka - ile scene siweziisahau hata leo........... maana mama alijibu kidogo kisha akaamua kuondoka sebuleni, bibi si akawa anamfuata nyuma kwa maneno chungu mbovu. Mpaka ikanibidi nimwambie Mama we nyamaza tu kaa kimya.kisha nikamgeukia bibi, basi bibi yameisha, tusamehe........ ofcoz aliendelea kusema na hata aliponyamaza si kwamba alinyamaza kwa sababu mie nilimwomba la hasha ........yule aliamua tu kunyamaza, pengine mate yalimkauka. Hakuwa akiogopa mtu Bibi yangu yule; Mwenyezi Mungu amrehemu.
Lakini cha ajabu kuja kuuliza chanzo kilikuwa ni nini, nlicheka, eti kosa lilikuwa Mama kumwomba Bibi aache kufua kwanza aje anywe chai! bibi akasema asiingiliwe taratibu zake kwani siku nyingine Mama anavyokwenda kazini nani anamkaribisha chai.......ugomvi ukaanzia hapo maana mama aliichukulia kama kajibiwa vibaya. Sasa hapa unaona kabisa ingekuwa salama kama jibu hili lingepuuzwa!

2. Akili ni jambo la muhimu sana. Akili zinakusaidia kuchanganua na kufahamu mwelekeo wa uhusiano na namna unavyotaka uhusiano uende. Akili zinasaidia kuchuja yale unayopaswa kuyafanya. Usipotumia akili yako katika mahusiano yako, uwe ME au KE, unacheza pata potea. Wengi wanaendesha maisha yao kwa 'emotions' na ndio wanaoumia sana pale inapotokea matatizo.

Akili, sawa kabisa. Na hili linahusu wote wawili ambao ni wahusika wakuu- mke na mume. Utakuta mke mwingine kwa vile tu ashajua kuna tatizo upande wa wakwe na wifi zake basi naye anayakuza. Kitu kidogo tu (hata clashes za kika) ambazo anaweza either kuziignore au kuzisolve mwenyewe atamfikishia mumewe! Tena kishari basi utadhani mumewe ndo alomtenda...........utashangaa tu kanuna, hata pole ya kazi hakuna....ukiuliza unapigwa nalo usoni.kamwulize mamako/dadako!! au mie hapa nimeolewa na wewe na si Mamako wala dada zako!........... sasa maneno haya yakizoeleka kila mara ukifanyiwa kijikitu hata huyo mume naye atashindwa kuvumilia na slowly atadrift-away from wewe na kuanza kuside na ndugu zake. Mke mwema ni yule anayejua kuitumia akili yake vema kuhakikisha amani ndani ya nyumba yake na upendo.

Kwa upande wa mume pia, akili katika kutuliza rabsha hizi ni muhimu sana. Sio mke chumbani kakushtakia basi we unatoka na kushika tambi lako unabwata kwa sauti kugomba au kama ndo mama/wifi kakushtakia basi nawe wamwita mkeo mbele ya wote na kuanza kumfokea hadharani. Hapo husolve tatizo bali unazidi mwagia petrol kwenye moto ulioanza kuwaka. Maana mke atadharauliwa zaidi kwani kaka umetoa ruhsa hiyo na mama/wifi watapandwa kichwani kwa kuwa umetoa go ahead kwa mkeo.

Jaribu kuongea nao kila pande peke yao kama hali haijawa mbaya but kama ndo imeshakuwa bomu lililo karibu kulipuka basi kaa nao meza moja na waeleze kiupole bila kupoint fingers jinsi hali ya maisha hayo inavyokutesa kifikra, na kisha weka rules zako. Jitahidi kuwafanya kila mmoja ajione amekosea/amemkosea mwenzie.

3. Napenda nizungumzie historia kama sehemu nyingine muhimu. Wengi wanaingia ktk mahusiano na kujifanya ni watu ambao hawajawahi kugombana na watu ktk maisha yao au hawajawahi kupishana na watu. Hulka hii huiangusha ndoa nyingi. Historia yako ya mahusiano yako na watu baki, ndugu zako na marafiki zako ina uzito sana ktk namna unavyoweza kutatua tatizo au ugomvi wowote unaotokea kati yako na shemji/wifi zako. Kama ulikuwa mropokaji tegemea hilo, kama ulikuwa unasusa tegemea hilo, kama ni mlipizaji tegemea hilo. Sasa iweje leo uanze kulialia eti unaonewa? Kwenye ugomvi wowote lazima kuwe na pande mbili na kila mmoja anachangia kulifanya tatizo liwepo.

Nina mawifi na mashemeji kedekede na kila mmoja ana personality yake so it does not bother me na siku zinaenda . Hatujawahi kushikana wala kusemezana. And am happy and they are happy.

.........Hii ya historia Bmkubwa imenishika.its very interesting ningependa kuifahamu zaidi BiMkubwa ...........naelewa kuwa kama mke/mama/wifi allikuwa ni mtu wa kidomodomo hatowezajizuia kuchezesha kidomo chake kwenye ndoa ya mtoto/kaka au mumewe....ndio unachomaanisha hapa?? So kama mume anajua kuwa dada zake/mama yake wana historia ya ugomvi (labda aliona/anaona kwenye ndoa za ndugu zake wengine) aitegemee hiyo kwenye ndoa yake??
 
Mwanajamii, natumia simu kuandika kwa hiyo inanichukua muda kidogo kujibu. Ngoja nikae kwenye computer ndio nitajibu swali lako. Historia ina maana pana kidogo. Wala usiwe na shaka I will respond.
 
...nilipata kusikia nasaha kwamba mke/mume akiwa na dukuduku, au malalamiko ni mwiko kwenda kusema kwao (i.e wazazi, dada zake, nk) kwani hilo litamjengea mwenza wake uadui.

Anapaswa huyo mke/mume kwenda kuyaelezea malalamiko yake Ukweni (Wazazi wa Mke/Mume/ wifi/Shemeji zake nk) ili hata ikibidi, wakae na ndugu yao wamueleze/wamkanye.

Sasa ukiwa na mahusiano mabaya na wakwe zako, utaanzaje anzaje yarabi?
 
Hapo sasa..........lol ila sidhani kama hii huwa inawork siku hizi naona kama kukiwa na ulazima wa kwenda kushtaki basi wanafuatwa walel wasimamizi wa arusi (kama ni ndoa ya kikristo- waislamu sijui kama wana wasimamizi). But am telling you sie kina dada tuna udhaifu wa kushtakia kwa mama zetu!! hata tukikatazwa vipi huwa tunawauma sikio mama zetu sema tu wanakuwaga wastaarabu sana not to show kuwa wanajua lolote........but ukimkuta mkwe-nuksi loh hakawii kukurushia kijembe Mbu ukashaa!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
MJ1 ni mada nzuri, na ningependa nichangie ingawa kwa kujazia kidogo kwani mengi mazuri yameshasemwa.

Binafsi naona uhusiano kati ya wake zetu na wakwe/mawifi wakati mwingine unakuwa mgumu kutokana na vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu. Kuna vyanzo vingi lakini tukiangalia inawezekana sisi wanaume tunatengeneza mazingira hayo hata kabla ya ndoa. Unakuta mimi nina mpenzi wangu nampenda kwa dhati na pia nataka awe ndiyo dira yangu ya maisha. Sasa kabla sijaoa nawaita mama na dada zangu eti wampitishe..yaani naleta demkrasia kwenye maisha yangu, nadhani ili ni kosa kubwa na ndiyo chanzo cha matatizo ya baadaye kwani ndugu zangu wataona wana share kwenye ndoa yangu. Nadhani kinachotakiwa ni kuwapa tu taarifa kwa busara kuwa huyu ndiye ndugu yenu niliyependezwa nae..wapende au wasipende. Full stop! Hii inawezekana nami nilifanya hivyo!

Pili tukumbuke kuunganisha familia mbili zilizoishi katika mazingira tofauti si kazi ndogo..yaani ukiweza asilimia 60% mshukuru Mungu. Sasa ni jinsi gani sisi wana ndoa tutakubali kubeba kwa pamoja yale mapungufu ya asilimia 40% ambayo tupende au tusipende haiwezekani ku balance hiyo equation..ni mitihani na yataka ujasiri na kuaminiana? Je.. kina mama wakimsema mke wangu nikae kimya? au niwafokee ili wanitenge na kuniambia nimelishwa dawa? au niwaeleweshe kuwa kutompenda wifi au mkwe ni sawa kwa asilimia 110% kutonipenda mimi.. kama watamtenga basi waanze kunitenga mimi?

Kwa haraka haraka .. Mimi binafsi nadhani wanaume tunachangia bila kujua mahusiano haya. Tuna nguvu ya kuyaboresha na pia tuna uwezo wa kuyakoleza moto. Ila tusisahau.. ili kusawazisha mambo inabidi mke na mume kuwa kitu kimoja kwenye lawama na busara. Inabidi mke na mume kuwa wakweli na uwazi utawale kwani ..baada ya ndoa ..familia zetu na wazazi wetu ..wanarudi kupunzika seat ya pili na kutuacha sisi wenyewe kwenye usukani..hawatakiwi tena kutuingilia wakati tunaendesha jahazi letu..Nawasilisha..

To me, you are very right, ningeweza ningekupa thanks mara mia.
Wanaume wengine wanachangia matatizo ndani ya ndoa zao wenyewe, kama tujuavyo jamii za kiafrika, mwanamke anaonekana ndio amehamia kwenye ukoo wa mwanamme na anapoteza Identity kwenye ukoo wake, Hivyo ni jukumu la mwanamme kujua kua mke hana mtu anayemfahamu na kumlinda zaidi ya yeye, mme anapoonekana kutomlinda mkewe, na mke hana mtu mwingine mwenye uchungu naye kwenye hiyo jamii hapo ni maumivu makubwa sana kwa mwanamke.
Mara nyingi ndugu wa mwanamme wanajiona wana haki zaidi kwenye familia ya wanandoa kuliko ndugu wa mke, ndugu yako akija kusalimia tu, hata kama mama mkwe na mawifi wapo mbali, utapigiwa simu na kuulizwa..
Tatizo lingine kubwa ni pale mwanamme hataki kua muwazi, akiwa anaongea na ndugu zake ni kama anaongea na nyumba ndogo, Namaanisha mwanamme anashirikiana na ndugu zake kukusema, nilishambana Mume wangu baada ya kusikia maneno flan, akaniambia ni kweli wazazi na ndugu zangu wanakusema vibaya ila sitakuambia...nae anashirikiana nao katika huo upuuzi, kwa hali ya kawaida mwanamke huwezi kua na Amani wala kujiamini kwenye hiyo nyumba.
Unakuta mipango ambayo mtaitekeleza mda flan ujao, unaanza kusikia Kwa wakwe/Mawifi kabla mumeo hajakuambia, ina maana anapanga na ndugu zake, wakishakubaliana wewe utaambiwa tu kama mtekelezaji.

nk, nk...
 
Mwanajamii one yaani kusema cha ukweli hii mada huwa inanibariki saaanaaaa, ingawa niliiona toka hapo awali ulipoiweka lakini nimejikuta nikiitafuta tena. Duh! Big up sana kwako na kwa wadau kwa michango yao mizuri.
 
Phweeeeeh aksante neggirl maana ungeniona nlivyokimbilia huku baada ya wewe kupost maana nlihisi ushaharibu huko kwa mkweo na mawifi. Ubarikiwe sana mpendwa
 
Phweeeeeh aksante neggirl maana ungeniona nlivyokimbilia huku baada ya wewe kupost maana nlihisi ushaharibu huko kwa mkweo na mawifi. Ubarikiwe sana mpendwa

Lol... wakati unaiweka nilifurahi saana maana niliipitia kwa nguvu zote ili nihakikishe mbeleko hainishindi. Mara ghafla nkaona kibebeo kinaanza kunizidi uzito nkasema nije tena kujikumbushia mambo ya msingi ..hahaaaa haha.
 
Wanawake sometimes tuna matatizo, ndio sisi sisi madada na ndio sisi mama na ndo sisi wake. yani kama sio dada wa mtu utakuwa mke au mama. cha muhimu ni kila mtu kujua role yake na limits zake. ukiwa wifi au mama kuwa na principle zako ambazo hazilgongani na maslahi ya mke kwa kaka yako au mwanao. the same kwa muolewaji yako yawe na limit yasiaffect mahusiano ya mama na mwanae au adada na kaka yake. kila mtu akicheza kwa nafasi yake na kujua limits zake sioni kwa nini kuwepo na shida.
 
akubaliana nawe humble finest! it doesnt bother me mwenza kuwa karibu na ndugu zake, ni ndugu zake anyways! umemkuta mwenzio na ndugu zake, they have been thru rain and sunshine huko walipotoka koote hadi umemuona handsome at 25 say! muhimu ni kuongea pale privacy yako inapokuwa intruded.lakini ukiwachukulia wakwe na mawifi kama ndugu zako tu, and not fussing over small stuff maisha yanaenda tu. huwezi kukwepa lawama kwa asilimia mia,lakini just play ur part. iliyo haki yao wape,ya kwako hakikisha u stand by it. confrontations kwenye kila kitu nayo inakufanya unakuwa a ajabu,vingine unapotezea tu. japokuwa nadhani mara nyingi mwanaume anakuwa na sehemu kubwa ya kuweka familia ya kwao na ya kwake vizuri kama atasimama kama mwanaume. kuna aliyewekewa paja humu, akarudi na mkewe sebuleni akamuambia mamake usijali,huyu mwanamke anajua kunitunza ile mbaya! siku hizi nimezeeka sili kama wakati ule nakua! approaches tu! akifanya kitu mama mkwe ama wifi,jiulize kama angekuwa mama/dada yangu ningewasha moto hivi? ama ningepotezea?
kweli hili ni neno kubwa sana nilishawaambia watu huku nikiwa kama nivea wakati ule hapo kwenye red panamata sana hii kitu huwa hainichoropoki kichwani kuhusu yeye kuwasaidia nduguzake hata kama how hard the situation about the family is i alwaz surrender,mwache awasaidie hujui alipotoka nao na sio yote unayajua hii maneno its so logical aisee.alwas remember your past life alwas haunt you!!!!!!!!!!!!!!!its not all about love same applied
 
Last edited by a moderator:
To me, you are very right, ningeweza ningekupa thanks mara mia.
Wanaume wengine wanachangia matatizo ndani ya ndoa zao wenyewe, kama tujuavyo jamii za kiafrika, mwanamke anaonekana ndio amehamia kwenye ukoo wa mwanamme na anapoteza Identity kwenye ukoo wake, Hivyo ni jukumu la mwanamme kujua kua mke hana mtu anayemfahamu na kumlinda zaidi ya yeye, mme anapoonekana kutomlinda mkewe, na mke hana mtu mwingine mwenye uchungu naye kwenye hiyo jamii hapo ni maumivu makubwa sana kwa mwanamke.
Mara nyingi ndugu wa mwanamme wanajiona wana haki zaidi kwenye familia ya wanandoa kuliko ndugu wa mke, ndugu yako akija kusalimia tu, hata kama mama mkwe na mawifi wapo mbali, utapigiwa simu na kuulizwa..
Tatizo lingine kubwa ni pale mwanamme hataki kua muwazi, akiwa anaongea na ndugu zake ni kama anaongea na nyumba ndogo, Namaanisha mwanamme anashirikiana na ndugu zake kukusema, nilishambana Mume wangu baada ya kusikia maneno flan, akaniambia ni kweli wazazi na ndugu zangu wanakusema vibaya ila sitakuambia...nae anashirikiana nao katika huo upuuzi, kwa hali ya kawaida mwanamke huwezi kua na Amani wala kujiamini kwenye hiyo nyumba.
Unakuta mipango ambayo mtaitekeleza mda flan ujao, unaanza kusikia Kwa wakwe/Mawifi kabla mumeo hajakuambia, ina maana anapanga na ndugu zake, wakishakubaliana wewe utaambiwa tu kama mtekelezaji.

nk, nk...
hii kitu ilimwachanisha dada yangu na mumewe waliezaa naye watoto wawili,kweli jamii za kiafrika bado kabisa wapo usingizini mume hakuweza mtetea mkewe yani ilifika mahali yule dada kama yuko ugenini tena msituni kabisa mume amefikia hata kuhamia kwao kumtete na nduguze,mama yule kumpangia hata mwanae sehemu za kuishi bia kumshirikisha yule mke mtu du mwisho wifi mtu akamtukana matusi na mumewe hakuzungumza lolote basi yule dada aliondoka na watoto wake mpaka leo ameolewa na mme mwingine!!!!!!!!!
 
mkwe hasa mama na mawifi hata uwabebe bado hawabebeki wanawivu ni balaa! MAMA MKWE ni kama mchanga kwenye mchele unajitahidi kuupembua wee lakini ukikosea tu ukabaki ukitafuna unaumiza meno ni balaa. MAWIFI nao ni kama chuya katika mchele unajitahidi kupembua lakini ikibaki inasumbua kwenye kula si mchezo. afadhali MASHEMEJI ni kama pumba ktk mchele ukipembua vizuri aah hazinaga shida hizoo zinakwenda. hivyo shemeji ukimtendea vizuri huwa hana time nawewe sanasana atakusifia sana kazi ni hao wawili!
 
1. Tatizo kubwa hapa ni wivu, wanawake wote wana wivu sio wivu mbaya ila ni wivu ambao hutokana na natura yao. Kwa hiyo mwanaume anatakiwa kujua jinsi ya kuwa referee wa wote hawa. ukipatia wataishi vizuri sana. Mimi nina dada zangu, kila mmoja anataka aonekane bora, sometimes hata wanagombana, ukiwauliza nini wanagombania hata hakieleweki. cha msingi inabidi nitafute njia ya kuwa fanya wawe wamoja na wala huwa haichukui muda.
2. Pili mke asimbane sana mume na kuona kana kwamba anakua amepoteza kitu kama mume wake anauhusiano mzuri na familia yake. ajiingie vizuri kwenye familia ya mume wake na awe mtoto wa familia kabisa japo yeye ni mke wa mtoto wa familia.
3. Wadada wajifunze kuheshimu ndoa za kaka zao na wajue wapo kuwasaidia kaka zao kutimiza ndoto zao za kuwapenda wake zao. wanatakiwa wawe mstari wa mbele kuwaelekeza jinsi ya kuwapenda wake zao badala ya kuwaonea wivu kwani ni haki ya mke wa kaka yako kupendwa kimapenzi tena 100%

nawakilisha.
 
mkwe hasa mama na mawifi hata uwabebe bado hawabebeki wanawivu ni balaa! MAMA MKWE ni kama mchanga kwenye mchele unajitahidi kuupembua wee lakini ukikosea tu ukabaki ukitafuna unaumiza meno ni balaa. MAWIFI nao ni kama chuya katika mchele unajitahidi kupembua lakini ikibaki inasumbua kwenye kula si mchezo. afadhali MASHEMEJI ni kama pumba ktk mchele ukipembua vizuri aah hazinaga shida hizoo zinakwenda. hivyo shemeji ukimtendea vizuri huwa hana time nawewe sanasana atakusifia sana kazi ni hao wawili!

Nimetamanije kugonga like mara mbili???? Kifupi ndugu za mume ni kama gunia la misumari, hata ulibebe vipi litakuchoma tu, yani kikubwa hapa ni mume kuwa na msimamo na kumuweka kila mmoja katika nafasi yake na kuzingatia mipaka yake.
 
Nakubaliana kabisa na hoja zako. ni vizuri wenye wake, mawifi wakwe wakazingatia haya ili kuepusha migogoro kwenye ndoa.
 
Back
Top Bottom