Mahubiri ndani ya mabasi

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,364
Wakuu leo nilikuwa katika basi fulani la kutoka mkoani na tulipofika sehemu ya kujipatia chochote kabla yakuendelea na safari, baada ya hapo alipanda mhubiri mmoja aliyejitambulisha katokea Kenya na kuanza kuhubiri na kusema wote wanaoumwa au wenye wagonjwa nyumbani wanyoshe mikono pamoja na kuwaombea na pia ameshuhudia watu mbalimbali wamekwishapona ktk mahubiri yake kwenye mabasi.

Baada ya kuwaombea alidai tangia pale wote walionyoosha mikono wameponywa na baada ya hapo kilichofuata ni kukusanya sadaka.

Je, hizi ndo nyakati za mwisho?
 
Mkuu tatizo ni mahubiri, au kukusanya sadaka au maombi kwa wagonjwa?
 
sasa kutwa afanye mahubili fikiri bila ya sadaka atakula nn mpeni chake bana malipo ya mbinguni ni mengine
 
Wakuu leo nilikua ktk basi flani la kutoka mkoani na tulipofika sehem yakujipatia chochote kabla yakuendelea na safari, baada ya hapo alipanda mhubiri mmoja aliyejitambulisha katokea Kenya na kuanza kuhubiri na kusema wote wanaoumwa au wenye wagonjwa nyumbani wanyoshe mikono pamoja nakuwaombea na pia ameshuhudia watu mbalimbali wamekwishapona ktk mahubiri yake kwenye mabasi, na baada yakuwaombea alidai tangia pale wote walionyoosha mikono wameponywa na baada ya hapo kilichofuata ni kukusanya sadaka. Swali je hizi ndo nyakati za mwisho?

Hii tabia inaongezeka sana sasa hivi, anapanda mtu ktk basi lenu, anachapa injili, kituo cha kushuka anachokijua yy kikikaribia,anaanza kuomba sadaka, nadhani ni vizuri wachape injili na kuombea safari,halafu kama wasafiri wameridhika na huduma yake wampe cho chote kwa hiari yao.
 
huwa wana karaha kuwapigia kelele watu ndani ya bus wengine wana mawazo yao, pia kila msafiri ana imani yake
 
Ukiwa kama mtumishi wa mungu sio lazima utegemee sadaka ili kuendesha maisha yako ya kila siku. Asiyefanya kazi na Asile. Mungu anajua hilo kwamba hata kama utamtumikia basi jishughulishe.
 
Wajinga ndio waliwao,watu wanacheza na kaz ya mungu imeshakuwa mtaji na njia ya kutengeneza pesa
 
Nina maswali kadhaa, hivi hao jamaa huwa wanapanda gari bure?
Tena huwa wanakula nini?
Wanavaa nini?
Na je wanaonekana hawana elimu wala uwezo wa kufanya kazi nyingine isipokuwa hiyo?
La mwisho hivi kuna mtu kalazimishwa kutoa sadaka au ameuliza mtu anayejiskia kutoa na atoae ili aendelee kwenye basi lingine.
 
Wakuu leo nilikua ktk basi flani la kutoka mkoani na tulipofika sehem yakujipatia chochote kabla yakuendelea na safari, baada ya hapo alipanda mhubiri mmoja aliyejitambulisha katokea Kenya na kuanza kuhubiri na kusema wote wanaoumwa au wenye wagonjwa nyumbani wanyoshe mikono pamoja nakuwaombea na pia ameshuhudia watu mbalimbali wamekwishapona ktk mahubiri yake kwenye mabasi, na baada yakuwaombea alidai tangia pale wote walionyoosha mikono wameponywa na baada ya hapo kilichofuata ni kukusanya sadaka. Swali je hizi ndo nyakati za mwisho?
Siku za mwisho wa nini? mtu huyo alitakiwa kuadhibiwa kwa kukirihi abiria na kuingilia utulivu wao.
 
lets be fair jamani, angepanda kwenye basi mtu anafundisha quran (sijui nimepatia spelling?), tungeona sawa pia? huwezi kufanya vitu mahali ambapo watu wako confined na hawana alternative ya kutoka! sio sawa kuhubiri kwenye basi! niliwahi kuwa kwenye basi akapanda jamaa anauza sabuni na bidhaa za kichina.aliongea kwa umbali wa kama 100kms! ilikua kero haswa kwa sababu nilikuwa nimechoka na niliona nahitaji kupumzika. kama kulikua na wasioamini nafikiria walikerwa kiasi gani! na ya sadaka tena, hata nisiiongelee.manake tunapiga vita posho za watumishi wa umma, kwani kila mahubiri lazima sadaka itoke?
 
ckuhizi mahubiri ni biashara mbona msiwashangae kina kakobe na mzee wa upako wanavyokusanya mapato
 
Ni common sana kwa mabasi yaendayo arusha!ukifika mwanga wanapenda sn panda!nahisi ni nyakati za mwisho,inawezekana manabii wa uwongo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom