Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
JokaKuu... ni lazima tukumbuke kuwa Lowassa alijiuzulu kuzuia huko unakotaka kwenda. Asingeweza kupinga Bungeni na kusema yote yaliyosema hayakuwa kweli kwani hapo ushahidi zaidi ungetakiwa kutolewa. Lakini kwa vile wahusika wakubwa walikubali kuwajibishwa utoana ile haja ya kwenda huko mbele zaidi ilipotea. Ndio maana bado anashauriwa kuwa kama hakutendewa haki aende mahakamani au kufungua kesi ya madai au wherever other discourse ambayo anafikiri anayo.
Mkuu nadhani Katiba inapinga kufikishwa mahakamani kwa mambo yoyote ayanayotamkwa na mbunge anapokuwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano. Hakuna uwezekano wowote wa Lowassa kufikisha shutuma au shitaka lolote mahakamani kama lilijadiliwa Bungeni. Maana hakuna hukumu yoyote ambayo mahakamani inaweza kutoa kutokana na shitaka hilo.
Mahali pekee ambapo Lowassa angeweza kujitetea ni ndani ya Bunge. Alishindwa kwa kuwa hakuwa na utetezi wowote wa kufanya aidha kwa kuhofia kuumbuliwa zaidi au vinginevyo, lakini pale ndipo haki zake zote zingeweza kupatikana.