Mahojiano ya Dr. Mwakyembe juu ya Madai ya Lowassa...

JokaKuu... ni lazima tukumbuke kuwa Lowassa alijiuzulu kuzuia huko unakotaka kwenda. Asingeweza kupinga Bungeni na kusema yote yaliyosema hayakuwa kweli kwani hapo ushahidi zaidi ungetakiwa kutolewa. Lakini kwa vile wahusika wakubwa walikubali kuwajibishwa utoana ile haja ya kwenda huko mbele zaidi ilipotea. Ndio maana bado anashauriwa kuwa kama hakutendewa haki aende mahakamani au kufungua kesi ya madai au wherever other discourse ambayo anafikiri anayo.

Mkuu nadhani Katiba inapinga kufikishwa mahakamani kwa mambo yoyote ayanayotamkwa na mbunge anapokuwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano. Hakuna uwezekano wowote wa Lowassa kufikisha shutuma au shitaka lolote mahakamani kama lilijadiliwa Bungeni. Maana hakuna hukumu yoyote ambayo mahakamani inaweza kutoa kutokana na shitaka hilo.

Mahali pekee ambapo Lowassa angeweza kujitetea ni ndani ya Bunge. Alishindwa kwa kuwa hakuwa na utetezi wowote wa kufanya aidha kwa kuhofia kuumbuliwa zaidi au vinginevyo, lakini pale ndipo haki zake zote zingeweza kupatikana.
 
..Dr.Mwakyembe aliwahi kusema kwamba kuna mambo ambayo hawakuyaandika ktk ripoti yao ili kukwepa kuiabisha serikali.

..kwa msingi huo naamini kwamba kuna ufisadi mkubwa zaidi ambao Mwakyembe na timu yake waliamua kwa makusudi kabisa kuyaficha.

..sasa ni ufisadi upi ambao Mwakyembe aliamua kuuficha? je ni mafisadi gani ambao Mwakyembe aliamua kuwasitiri?

Hapa ndipo ninapopata matatizo. Huyu bwana na kamati yake waliona responsibility yao ni kwa serikali na sio wananchi waliowatuma itakuwaje sasa wabadilike? Leo hii wakati uchaguzi umekaribia ndio atambue kuwa walikosea? Pengine badala ya kutumia lugha ya kificho, angetuambie tu hayo waliyoyamezea ni yapi. Au anaiweka kama trufu ili iwapo atakaposhindwa uchaguzi ageuka kuwa shujaa wa wanaoonewa?

Amandla.......
 
Mkuu nadhani Katiba inapinga kufikishwa mahakamani kwa mambo yoyote ayanayotamkwa na mbunge anapokuwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano. Hakuna uwezekano wowote wa Lowassa kufikisha shutuma au shitaka lolote mahakamani kama lilijadiliwa Bungeni. Maana hakuna hukumu yoyote ambayo mahakamani inaweza kutoa kutokana na shitaka hilo.

Mahali pekee ambapo Lowassa angeweza kujitetea ni ndani ya Bunge. Alishindwa kwa kuwa hakuwa na utetezi wowote wa kufanya aidha kwa kuhofia kuumbuliwa zaidi au vinginevyo, lakini pale ndipo haki zake zote zingeweza kupatikana.

NI kweli lakini sasa Lowassa anazungumza nje ya Bunge.. anachotaka kusema akisema au aende nacho mahakamani.. anaweza hata kufungua kesi ya kikatiba kama kuna utata na kwa vile tumeshajua kuwa Mahakama ndiyo iko hivyo ilivyo anaweza akapata chance ya kuchallenge kilichotokea bungeni.
 
Hivi mbona Watanzania wamekuwa waoga waoga kiasi hiki ?

Sielewi na inasikitisha,inatia hasira sana.Leo watu ooh EL na Richmond,ooh RA na EL wanakula nchi maisha magumu,kesho ooh tusimzungumzie EL kwa sababu nchi itaingia matatizoni - KWA NINI TUWE WAOGA KIASI HIKI?Sasa kweli unategemea hayo maisha yatabadilika kama hakutakuwa na change.Mtu akikuibia leo na kesho akaja na nyimbo na chakula,utamkubali tu na kusahau ya jana??Tuache upuuzi na upumbavu wa aina hii.Utakuta mijitu mingine ni watu wazima kabisa na wamesoma sana tu.Inasikitisha sana.Inakatisha tamaa kuwa tulianzisha moto pamoja halafu watu wengine wanakatiza safari katikati kisa uoga.Kama mtu hataki kusikiliza mahojiano,sio lazima,kaa na maisha yako ya kuwa fisi.
 
Mkuu, nadhani Kamati ile ilipewa scope ya kazi. Inategemea na ukubwa wa scope... Naamini kuwa
Aah, kumbe we mwenyewe huna hakika. Sasa kwa nini unampa yeye faida ya shaka?

Recta, baadhi ya wananchi, kama mimi, huwa hatudhanidhani na kuaminiamini vitu tu ovyo. Nimekosoa ripoti kutokamilika wewe unasema "nadhani ilipewa scope...inategemea na scope," scope gani? Ungeitaja, sema kamati iliambiwa ifanye hiki na kile, hayo mengine hawakutumwa, ningekuelewa. Lakini huwezi kutegemea nidhani dhani tu kwamba wigo wa kazi waliotumwa ndio ulikuwa ule, mimi siupi uongozi faida ya shaka.

Tena hata yeye hakujitetea hivyo. Kadai alishindwa kumwapisha Lowassa kwa sababu yule dada anaeapisha mashahidi ni "mtoto mdogo sana," kama kawaida yake Mwakyembe na dharau. Hivi mwanasheria unaesemwa umebobea utashindwaje kuelewa kwamba Lowassa angekuja mbele ya Tume angeapishwa na mamlaka ya Tume ya Bunge, sio "karani.. dada... mtoto mdogo sana" ? Huyo mtoto mdogo kwa mamlaka ya Tume anauwezo wa kumwapisha shahidi yeyote atakaekuja mbele ya Tume, hata Rais.

Eti Mwakyembe na weledi wako wote unaosemekana, hayajui haya. Tumepungukiwa wataalam Tanzania.
 
MSAUZI hivi unamfahamu Mwakyembe vilivyo. Umesikiliza mahojiano yake? Umesikiliza majibu aliyotoa? Nina uhakika hukumsikiliza kwa makini na hivyo hukuelewa. Kama ungeelewa alichosema wala usingeandika hiki ulichoandika hapa.

Kwa taarifa yako Mwakyembe ni mwalimu wa Chuo Kikuu Mlimani. Amesema amefundisha na marehemu aliyeuawa kwa miaka 30. Unatarajia kwa uzoefu wake wa kufundisha miaka 30 ashindwe kujibu maswali madogo hayo?. Kwanza nampa pole kwa kumpoteza mwenzake waliyesoma naye Mirambo na kufanya naye kazi Dar na pia ni wa nyumbani kwao.

MSAUZI unatakiwa uelewe pia kuwa Mwakyembe alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge iliyochunguza Richmond. Yeye na wanakamati wenzake wameshiriki katika kuchunguza na kutoa ripoti ya Richmond. Na kwa kukukumbusha, yeye ndiye aliyewasilisha ripoti ile kwa lugha tamu sana na kwa kujiamini. Dr. Mwakyembe anajua kila kitu kuhusu uchunguzi wa Richmond. Hahitaji kuambiwa majibu. Ukisikiliza mahojiano unaelewa kuwa hawakumhoji Lowasa kwa sababu kadhaa. Hizi sababu walikuwa wanazijua tangu awali.

Ni ajabu kusema kuwa eti ameandaliwa majibu.

Halafu kumbuka kuwa Mwakyembe ni Daktati wa shule. Mwakeymbe siyo Dr. Majimarefu au Dr. Kikwete cheo cha kupachikwa, kuvishwa kilemba cha ukoka. Dr. Mwekyembe siyo Dr. Kikwete wa kutaka sifa asizositahili, aliyeulizwa swali ughaibuni kwa nini nchi yako ni maskini japo ina maliasili nyingi, yeye kaseme sijui. Dr. Mwekyembe anajiamini, ni kati ya watu wachache wa CCM anayejali uhuru wake katika kuishi. Hafungwi na minyoro ya CCM, ameweza kupinga ufisadi bila kutetereka. Dr. Mwakyembe anaamua kuhojiwa na Mwanakijiji, ni wangapi wa CCM wanaoweza kudiriki kuhojiwa JF?.

MSAUZI unatakiwa ufanye tafakuri ya kina kabla ya kuandika. Mwakyembe anauwezo wa hali ya juu wa kupambanua mambo, ni msomi wa kweli, shule imetulia pale. Hongera Mwakyembe kwa kumrudishia Lowasa maji taka yake aendelee kujichafua.

Apparently Dr Kikwete was awarded a honorary degree by an online university which has no physical address. follow this link.....

.... plus please let me know His Excellency's personal advisor or advisors.... I find them quite incompetent. the reason for His Excellency Mr President to have no answers in an international forum can be closely blamed on them.... Au sio watanzania.. tell me what you think?
 
Last edited by a moderator:

Nime follow his link kwenye youtube ,haipendezi viongozi kuwa awarded honorary degree kwenye chuo chenye utata namna hiyo.

Halafu duh kuna marais kama 8 hivi makamu rais wa kenya,TANZANIA JK,burundi,uganda Museveni........................
 
Last edited by a moderator:
Kuelekea uchaguzi mkuu haya mahojiano yameonyesha na yanazidi ku prove kweli wapinzani wa kweli hawepewi nafasi ya kusikikilzwa na vyombo vya umma ambavyo ni mali ya walipa kodi.

Binafsi sipendi kuwaita hawa watu wapinzani wa kweli, bali Wapiganaji wa kweli...
 
Common guys!!nyie ndio mnajua kila kitu? nchi ya wato jamani!!! mnahukumu tuuu...au mkumbo
 
Hakuna mtu mwingine wa kumsafisha Lowasa kwa kashfa ya Richmond bali ni yeye mwenyewe ndio mwenye jukumu la kujisafisha. Asitumie vyombo vya habari kama redio,magazeti nk ili kujisafisha. Yeye sio mtoto mdogo kwamba akijinyea asafishwe na mtu kubwa nooo! Alioshirikiana nao kwenye Richmond walishamkana hadharani.
Lowasa,ukitaka ukubalike japo Utafiti wa kupika wa Twaweza unakupa kiburi,jitokeze hadharani umwage mboga kuwa Engineer wa Richmond alikuwa ni fulani ili mambo yakae sawa.
Lowasa,mwl Nyerere alikukataa. Richmond ili kufanya ujiuzulu ili kumlinda nyangumi au papa,sasa ni wakati wako kujisafisha,liwalo na liwe,otherwise we wont build trust to you. Kama unategemea watu kukusafisha,imekula kwako,wanakulia pesa yako bure. Ni ushauri tu,hutaki unaacha.
 
YUPO WA kUMSAFISHA LOWASSA PAMOJA NA WEWE!!
NI YESU TU NA SIO TB JOSHUA!!
LOWASSA ANAKOSEA!!! ANAWAENDEA WANADAMU AMBAO NAO WANAMAKOSA!!!
ANATUMIA NGUVU YA RUSHWA ASIJUE NI CHUKIZO KWA MUNGU!!
LOWASSA ANAPASWA KUTUBU KWA YOTE ALIYOFANYA NA KUDHAMILIA KUISHI SAWA SAWA NA TOBA YAKE!!!
HATA WEWE PIA HUFAI MBELE ZA MUNGU KAMA HUJAFANYA TOBA HII
 
Mungu anasamehe watu waliokiri makosa yao hadharani. Huwezi kwenda kwa jirani na kumwambia nenda kanisani ukaseme nina dhambi sana hivyo naomba toba. Huku ni kumkufuru Mungu. Toba ni wewe mwenyewe uliyetenda dhambi sio kuagiza mtu akatubu dhambi zako,huku ni kumdharau Mungu. Tunataka ajitokeze hadharani na aseme kuwa mimi ni mwizi au nilikuwa mwizi na sakata la Richmond fulani ndio alikuwa Engineer,taabu iko wapi?
 
Hapa ndipo ninapopata matatizo. Huyu bwana na kamati yake waliona responsibility yao ni kwa serikali na sio wananchi waliowatuma itakuwaje sasa wabadilike? Leo hii wakati uchaguzi umekaribia ndio atambue kuwa walikosea? Pengine badala ya kutumia lugha ya kificho, angetuambie tu hayo waliyoyamezea ni yapi. Au anaiweka kama trufu ili iwapo atakaposhindwa uchaguzi ageuka kuwa shujaa wa wanaoonewa?

Amandla.......

Bila shaka baada ya kushuhudia yaliyo endelea toka post yako ya mwisho ktk Uzi huu mpaka leo utakua na mtazamo na mawazo tofauti. Hakuna tofauti yoyote kati ya Lowassa,Mwakyembe,Sitta,nk. Wote ni wana CCM wenye kupigania maslahi yao na makundi yao. Anaye bisha atafakari upuuzi ulio endelea ktk BMK kama kuna mmoja wao alisimama kutetea maoni ya wananchi!
 
hakuna mtu mwingine wa kumsafisha lowasa kwa kashfa ya richmond bali ni yeye mwenyewe ndio mwenye jukumu la kujisafisha. Asitumie vyombo vya habari kama redio,magazeti nk ili kujisafisha. Yeye sio mtoto mdogo kwamba akijinyea asafishwe na mtu kubwa nooo! Alioshirikiana nao kwenye richmond walishamkana hadharani.
Lowasa,ukitaka ukubalike japo utafiti wa kupika wa twaweza unakupa kiburi,jitokeze hadharani umwage mboga kuwa engineer wa richmond alikuwa ni fulani ili mambo yakae sawa.
Lowasa,mwl nyerere alikukataa. Richmond ili kufanya ujiuzulu ili kumlinda nyangumi au papa,sasa ni wakati wako kujisafisha,liwalo na liwe,otherwise we wont build trust to you. Kama unategemea watu kukusafisha,imekula kwako,wanakulia pesa yako bure. Ni ushauri tu,hutaki unaacha.

umemaliza kila kitu !
 
Mwakyembe mwenyewe tayari kajipeleka kwa Lowassa kuomba msamaha amsamehe ili asimwache kwenye baraza lake la mawaziri 2015. Jina la Lowassa likipita mtaona atakavyojikanyaga na kukataa maneno yote aliyokuwa anatumia kumtukana Lowassa huko nyuma.
 
Bila shaka baada ya kushuhudia yaliyo endelea toka post yako ya mwisho ktk Uzi huu mpaka leo utakua na mtazamo na mawazo tofauti. Hakuna tofauti yoyote kati ya Lowassa,Mwakyembe,Sitta,nk. Wote ni wana CCM wenye kupigania maslahi yao na makundi yao. Anaye bisha atafakari upuuzi ulio endelea ktk BMK kama kuna mmoja wao alisimama kutetea maoni ya wananchi!

Like....
 
Back
Top Bottom