Mahojiano ya Dr. Mwakyembe juu ya Madai ya Lowassa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahojiano ya Dr. Mwakyembe juu ya Madai ya Lowassa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 20, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Dr. Harrison Mwakyembe Mwenyekiti wa Kamati Teule iliyochunguza sakata la Richmond na ambaye ripoti ya Kamati yake ilisababisha aliyekwua Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa kujiuzuu amesema kuwa jaribio jingine la Lowassa kujisafisha kwa kutumia vyombo vya umma kwa maamuzi yaliyomgharibu Uwaziri Mkuu haliwezi kufanikiwa.

  Katika mahojiano nami kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mauaji ya Prof. Mwaikusa na harakati zake za kurudi Bungeni Dr. Mwakyembe amesema kuwa mtu pekee anayewajibika kwa kujiuzulu kwa Lowassa ni Lowassa mwenyewe!

  SEHEMU YA KWANZA:


  SEHEMU YA PILI  SEHEMU YA TATU  Please do enjoy!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ningefurahi zaidi kama Dr Mwakyembe angesikika ktk main stream media na hasa TV zetu kubwa mbili, ITV au/na TBC.

  Najua ni jambo gumu maana nadhani bado kuna watu wanaamini EL atakuwa Rais na kuwarudi. Hata Tido hana ushujaa huo maana anapowahoji naona ni kama katekwa nyara.

  BTW, kuna tetesi kwamba EL sasa anataka U-spika. What expected encounter is this? Kama ni kweli hapo ndo tutajua unafiki wa wanasiasa wetu.
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa nini kukata mti kwa kisu wakati shoka lipo?

  Hawa wote dawa yao ni Dr. Slaa peke yake.

  Sasa hivi kazi kubwa mbele yetu ni kumfanyia kampeni ya nguvu Dr. Slaa ashinde. Akishashinda, basi ndiyo utakuwa mwisho wa Eddy Murphy ahh Eddy Lowassa. Nilichanganya kwa sababu wote ni WASANII.

  Tuachane na yote na tubaki ni Slaa. Tule nao sambamba hadi kieleweke mwaka huu.
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nasubiri kusikiliza hayo mahojiano ingawaje naweza kusema mapema kabisa kuwa wote hao, Mwakyembe na Lowassa, wanaogelea kwenye bwawa moja. Mwakyembe hawezi kudai mwenzake ni mchafu huku wote wamejifunika shuka moja, huo ni uwongo, unafiki na uzandiki unaofaa kusutwa na kulaaniwa kwa nguvu zote. Watu kama Mwakyembe ndio watu hatari kabisa kwa nchi hii na lazima waambiwe ukweli huu hata kama unauma kiasi gani - tumechoka kuzugwa na wanafiki walafi.
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji Aksante na hongera kwa kazi nzuri. Lakini kwa nini umeleta habari hii leo alafu unaseme utarusha mahojihano hayo JUMATANO. Unafanya EDITING ? au Muhojiwa kakuomba kabla ya kurusha hewani asikilize yeye kwanza asije akaingia kwenye matatizo na CHAMA na serikali yake.?
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Yep.. mara nyingi sifanyi editing.. nafanya mixing kidogo tu.

  hakuna mtu ninayemhoji mwenye ubavu wa kutoa ombi kama hilo kwangu. Its a no no!
   
 7. N

  Ngala Senior Member

  #7
  Jul 20, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwamba mwakyembe naye niniiii?
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Anataka kufunga mlango wakati farasi kesha kimbia? Kama walimuona mchafu kwa nini walimlinda? Nini kimebadilika sasa? Lolote atakalosema sasa itaonekana ni wivu na chuki binafsi. Wakati wake umepita.

  Amandla......
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ninafikiri kuna haja ya kuangalia impact ya hayo mahojiano kati yako na Mwakyembe kabla ya kuyaleta hapa. Ukumbuke kuwa tayari Lowassa anabebwa na Kikwete kwa sasa, kwa hiyo namna yoyote itakayoonyesha kwamba Mwakyembe bado anaendelea kumwandama, inaweza kuhatarisha usalama wake.

  Ningependekeza uangalie kwanza kama ni mhimu sana kuleta hayo mahojiano hapa. Otherwise kama hayana impact kubwa.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Yaani Lowassa aachwe azungumzie suala lile lile ambalo muda wake umepita kwa sababu analindwa na Kikwete?
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Unaogopa nini Mkuu? Unataka kutuambia nchi yetu imefika mahali ambapo mbunge aogope kusema kwa kuhofia maisha yake? Wengine hatupendi kutafuniwa kwanza kabla ya kupewa chakula. Mwakyembe alijua anafanya nini alipokubali kuhojiwa. Hamna kitakachompata.

  Amandla....
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji, kama utakuwa una kumbukumbu nzuri, ni kwamba mara tu baada ya lile sakata Tido alimwandalia kipindi Lowassa TBC ili ajitetee, lakini kile kipindi hakikudumu hata dk tano kikakatizwa.

  Bila shaka kuna order ilitoka kwenye mamlaka za juu kumtaka Tido akizuie, sasa leo TBC hukohuko kapewa nafasi ileile iliyozuiwa 2008 huwezi kuona kwamba kuna kitu hapo? Kuna sababu sasa ya Mwakyembe kutumia njia zilizo sahihi kulijibu hilo ikiwa ni pamoja na kupitishia kwenye mamlaka za bunge kuliko kuonekana na yeye ameingia kwenye vyombo vya habari kupinga kilichosemwa na Lowassa. Mwakyembe didn't work as an individual, he worked on behalf of the parliament.

  Kwa nini leo asimame yeye independently kutoa majibu juu ya mambo ya bunge. hizi ropoka ropoka hizi kwenye vyombo vya habari ndiyo zinasababishaga uvunjifu wa amani mahali pengi. So napendekeza uziangalie kwa umakini hoja za Mwakyembe kama hazina impact zitoe, otherwise, zinaweza kumgharimu. Take it from me.
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Hakuna kitu cha kuangalia katika hayo mahojiano mahojiano yarushwe bila kuchujwa. jF ni mahali wanapothubutu watu kuongea openly. Tena nasema kundi lililojipambanua kama wapambanaji wa ufisadi sasa ndio wakati wao wa kukaza buti kuliko mwanzo wa vile vita vyao japokua havikua na matokeo mazuri. Na hii ni kwa sababu wako boti moja(ccm). Tunataka sasa wakati wa kampeni wananchi wajulishwe kwamba ile richmond ilikua sii Lowasa tu bali na Kikwete ni mmoja wao. Alijitahidi kuikwepa lakini sasa ananaswa maana ni kipindi chake kigumu cha kutafuta ulaji. Hivyo JK utaungama usaliti wake wote kwa kina EL na kina ROS waliofanikisha kumuingiza ikulu 2005 kwa gharama kubwa ya kujitoa mhanga kuvunja Bank mchana kweupe(EPA).
   
 14. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160

  Hivi mbona Watanzania wamekuwa waoga waoga kiasi hiki ?
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitakachomgharimu Mwakyembe, ingawa alikuwa mwenyekiti lakini kwa sasa yuko huru kuzungumzia matokeo ya tume hafungwi na kitu chochote, kama tume ingekuwa bado haijatoa matokeo hapo ndipo angekuwa hayuko huru kuzungumzia.

  Lowassa ni mhalifu kama wahalifu wengine alistahili leo awe Segerea na atakayejaribu kumsafisha na yeye atachafuka awe Tido Kikwete au yeyote yule, kinachotakiwa ni yeye na magazeti yake ajisafishe kama anaweza. Mwana mkiwa.
   
 16. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  as far as both mwakyembe and lowasa are ccm kadas hawana jipya la kutuambia cha muhimu october wazalendo wote wa ukweli tupange foleni ya kupiga kura ili tuing'oe ccm
   
 17. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wakati mjadala wa richmond unazikwa bungeni Mwakyembe alikuwa wapi? Mbona hakuinuka na kusema hiki hakiwezekani? Je mapendekezo ya kamati yalitekelezwa? Yeye mwenyewe Mwakyembe anajua wazi jinsi suala hilo lilivyo hatari kwake. Si lazima wampige risasi. Lakini wanaweza kumneglect na kumsahau. Cha msingi tuchange karata zetu vizuri, watu wote waelewe ni mabadiliko gani yanahitajika nchini, wampe kura Dr Slaa, basi. Ukiwa ndani ya system ya CCM usije ukadhani kuna uhuru kihivyo my friend.
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #18
  Jul 21, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Vangi, Dr Mwakyembe ameshaliangalia hili jambo upside down,ndiyo maana akakubali mahojiano na MM.
  MM, well done ! lazima tupate both side of the story,sio tulishwe mahojiano ya kupanga ya TBC.
  EL anataka madarka kwa cost yoyote, hata hili la uspika si ajabu ni kweli. Huyu bwana kama hatadhibitiwa kwa majibu, atatembelea FM radio zote akijitahidi kuoga! Kumbuka uongo ukirudiwa mara nyingi hugeuka kuwa ukweli, kwahiyo asipewe mwanya.
   
 19. M

  Mutu JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  so u teach leaders to be cowards!!!???
  aogope nn ? that is what he sign in for.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mahojiano yapo kwenye posti ya kwanza!! Enjoy!
   
Loading...