Mahari ya Single Mom

Mahari ya Single Mom

Vip binti kaolewa ndani ya two years mume kafariki kaacha mtoto huyo hafai?
Vip Kwa binti ambae hana mtoto kuolewa na kijana mwenye mtoto?
binti asiye na mtoto kuolewa na single father ni maamuzi yake.ya kuambiwa atachanganya na akili zake
 
Personally,siwezi kuoa mwanamke mwenye mtoto nitaonekana zoba..

Wanawake wanaopata mimba kiwepesiwepesi hawa ndo tusemezane nao...Njia za kujikinga zipo kibao why uzae bila ya kuwa kwenye ndoa serious??.

Wanaochana/Kufiwa na waume zao hiyo ni case nyingine..

Tusiwazodoe sana,ila pia tusilifanye hili kuwa ni jambo jepesi..Kuoa mke mwenye mtoto wa mwanaume mwingine inahitaji moyo

Wanaume pia tubebe misalaba yetu..ukimpa binti wa watu mimba muoe usijekuwapa watu wengine mizigo isiyowahusu
what if kama mwanamke alitegesha mimba?
 
Maneno makali sana

Typed Using KIDOLE

Ukweli usemwe mkuu tuokoe kizazi chetu hali ikiendelea kama ilivyo sasa miaka wanetu watakapotaka kuowa na kuolewa tutajikuta ktk wakati mgumu sana.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Comments za watoto wadogo na primitives zinajidhihirisha wazi. Hayo mambo ya single mother visababishi ni sisi sisi wanaume. Acheni kuropoka upumbavu nyinyi washenzi.
hamna mzee kuna wanawake wanategeshea mimba?
 
Kuwa single mama siyo kosa hata kidogo, na wengi wapo wanaolewa kwa harusi safi na tunatoa michango na kusherehekea pamoja.

Swala la mahali ni makubaliano ya pande zote mbili.

Tuache kuwakashfu hawa single mamaz maana nao ni binadamu kama sisi wana moyo wa nyama na wanasikia maumivu pale wanapotukanwa ama kukashifiwa.

Nawapenda single mamaz wote hasa wale wapambanaji na wanaolea watt wao katika misingi iliyobora.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa single mama ni kosa usihalalishe dhambi, ukishakuta msichana ana mtoto na hajaolewa huyo ni MZINIFU! Usirembe wala kupepesa macho wambie Dada zetu wenye nia ya kuolewa waache Zinaa la hasha awe amechagua maisha yake mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenzi hayachagui,mwanamke kuwa single mom kuna sababu nyingi sana,tusiwahukumu sana na kuwaona dhambi yao nikubwa kiasi hiki...........tuache hii tabia maana chanzo ni sisi wanaume,mtoto wa watu anakuamini anakuvulia nguo kumbe wewe unataka tu kupunguza shida zako wakati mwenzio yupo serious.Tuwaache kwakweli maana chanzo ni male.......
Shida ipo hapo kwanini aakuvulie chupi? Mama huruma? Atawaamini wangapi sasa hata baada yako? Kikubwa mabinti wajiheshimu usitete Uovu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenichekesha sana
Anyway, si dhambi kutofautiana mitazamo.
Ila tuache kuwasema hawa single mothers si vema.

Nakupa mfano wangu, mimi nilimtia mimba binti wa watu na kusema ukweli ni mimi kisababishi - hakua tayari. Wanaume tuna nguvu kubwa ya ulaghai na ushawishi.
Hakuna mtu anaweza kumlazimisha mtu kufanya kitu asichokitaka kama hataki, wala sio kosa lako mkuu yeye alikua tayari kufanya mlichotaka kufanya ndio mana amefanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenichekesha sana
Anyway, si dhambi kutofautiana mitazamo.
Ila tuache kuwasema hawa single mothers si vema.

Nakupa mfano wangu, mimi nilimtia mimba binti wa watu na kusema ukweli ni mimi kisababishi - hakua tayari. Wanaume tuna nguvu kubwa ya ulaghai na ushawishi.
ashaolewa huyo binti?
 
Back
Top Bottom