Mahari kwa wanyakyusa

Mahari kwa wanyakyusa

tian

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2007
Posts
1,770
Reaction score
538
Habari Zenu Ndugu Zangu Wana MMU.Nilikuwa Sijawahi kuhudhuria tendo la kutoa posa kwa Wanyakyusa ila leo nimekuwa mmoja wapo wa kupeleka barua ya posa.

Swala la kupanga mahari limentoa macho kidogo huenda ni mimi kutokuwa na uzoefu.Kama ilivyo ada tumewasilisha barua vyema wakaipokea vizuri sana na baadaye tukapewa majibu kamaa ifuatavyo.

Mshenga upande wa binti kaanza kwa kusema sisi wanyakyusa huwa tunazo mahari mara mbili.(1).Mahari Ya Unyago ambayo ni non negotiable,ni kama ifuatavyo.

1.Ng'ombe Dume ambaye dhamani yake ni Tshs.500,000.Na hapa lazima utoe hela ng'ombe haitajiki.
2.Tshs.400,000 Za Mama Mzazi.
3.Blanketi 2 za wazazi.
4.Vitenge kulingana na idadi ya mashangazi.
5.Blanketi 2 za Bibi
6.Majembe Mawili.

(2)...Mahari Ya Pili ni negotiable:

1.Ng'ombe Wanne Majike.
2.Vitenge Vya Mashangazi.

Jamani nia yangu ya kuleta hili swala hapa ni kupata mtazamo wenu.
Je,Kwa Kijana wa kiume ambaye ametoka kwenye familia hohehahe ataweza kweli??

KARIBUNI MNIPE MTAZAMO WENU.
 
Ndagha Malafyale !
!
N'deke mwalangani na ilyopa lyake !
 
Mm ninachokielewa ni ng'ombe mmoja dume hyo ni non negotiable na sh. Kama laki1 hvi ila mahari kamaili ambayo ni negotiable ni ng'ombe3 . Hayo mengne sijui vitenge na nn hyo ni unyonyaji tu wa baadhi ya familia
 
Mwe ndagha mwendie!
Ni kweli,dume sio mjadala,dume hatajwi bei kama ilivyo,lakini jamii ya kinyakyusa ni pamoja majigambo, na matambishiano,hivyo mtoto wa kiume lazima aonyeshe kwamba yupo na ataendelea kuwepo.Vipo vituko na michezo mbalimbali wakati wa sherehe hizo.Na kama unaona hiyo gharama basi kaoe uchagani ambako wanachukuliwa bure
 
Mwe ndagha mwendie!
Ni kweli,dume sio mjadala,dume hatajwi bei kama ilivyo,lakini jamii ya kinyakyusa ni pamoja majigambo, na matambishiano,hivyo mtoto wa kiume lazima aonyeshe kwamba yupo na ataendelea kuwepo.Vipo vituko na michezo mbalimbali wakati wa sherehe hizo.Na kama unaona hiyo gharama basi kaoe uchagani ambako wanachukuliwa bure


Usiongee Hivyo Kwa Kuwa Unauwezo Mkubwa Wa Kifedha,Mimi Naongelea Mtanzania Wa Kawaida Kwa Mahari Yote Hiyo Tuliyotajiwa Kwani Binti Anauzwa Au Anafanywa Mradii Wa Ujasiriamali??

Msiwakatishe Tamaa Vijana Wenye Malengo Ya Kuoa.
Makabila Yenye Hizi Tamaduni Waige Mfano Wa Wachaga,Sio Mambo Ya Kurudishana Nyuma Kimaendeleo
 
Mm ninachokielewa ni ng'ombe mmoja dume hyo ni non negotiable na sh. Kama laki1 hvi ila mahari kamaili ambayo ni negotiable ni ng'ombe3 . Hayo mengne sijui vitenge na nn hyo ni unyonyaji tu wa baadhi ya familia

Daaah....Tumebaki Tunakodoa Macho Tu
 
Mahali inaombwa au kutolewa kutokana uwezo wa familia ya kijana.

Ni jukumu la binti kuwaeleza wazazi wake uwezo wa mkwe wao mtarajiwa ili wakati wa kupanga mahari wajue mkwe wao ni mtu wa namna gani.

Sidhani kama kuna familia inaweza kumzuia binti yao kuolewa kwa kutoza mahari kubwa!
 
Hizi mila zishapitwa sana na wakati. Waachieni binti yao mkatafute kwingine. Maisha haya ya fcbk na insta wanafanya km tuko enzi za kupiga cm ttcl
 
Bei ya ngombe dume na mkaja wa mama vinapangwa na kwa kuangalia uwezo wa muoaji.
Binti ndio anajua uwezo wa mwanaume hivyo wanaweza kutaja hata 50,000-milioni kwa bei ya ng'ombe dume. Na mkaja inaweza kua 20,000-500,000 na hata zaidi.
 
ImageUploadedByJamiiForums1399236273.406112.jpg
Karibu mbeya kwa mikono miwili

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Mahali ndogo ivo unalalama,,,, huku watu tunaolewa kwa gharama fuso akiwa tajiri semi au bus
 
Wanyakusya hawafai wana masharti magumu ya kuoa we acha kabisa halafu mabinti wenyewe wabishi na jeuri ukishawaweka ndani! Mke wangu ni mnyakyusa nilipoenda kuoa cha moto nilikiona. Kuna kitu wanaita mkaja wa mama, sijui kikingi, hela ya shangazi, vitenge, mablanketi, mashuka, ng'ombe 3 wawlli majike na dume moja, ukikaribishwa unalipia pale ulipokaa, wakileta msosi usidhani ni bure baada ya kula utaulipia. Mbona niliomba po at once nilijikuta km 2m zinakatika!
 
Kama ni bidhaa vile nikinunua basi hairudi ntaoa kwa hyo hela wanayo itaka
 
Back
Top Bottom