Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,502
- 16,712
Siku nikisikia jumba fulani la Mbezi limepigwa na drone ya US kutoka Sychelles basi nitalia na Lole.Nitamuona kama askari wa miguu wa Marekani anayetafuta targets.Wakuu tupeane habari mabayo imekuwa minong'ono ya chini chini kwa muda mrefu hapa Dar.
Pamekuwapo na "uwekezaji" usio wa kawaida kutoka ndugu zetu wa Kisomali katika jiji la Dar es salaam kwa muda sasa.
Sehemu za Mbezi kuna nyumba, zenye nakshi ambazo kimsingi ni za kiarabu, ambazo zimekuwa zinaota kama uyoga.
Miradi kama Ununio development,TANSOMA na hata jengo moja refu hapo Mbezi ni za raia wa Kisomali.
Tusisahau hata Paradise chain.
Ni vyema kukaribisha uwekezaji , lakini je kuna uhusiano wowote na pesa haramu za maharamia wateka meli?
Nauliza tu.
Dalili zinaonesha jeshi letu limeshaingiliwa na CIA na muda si mrefu jumba lolote la Mbezi likipigwa itaelezwa kulikuwa na gaidi fulani wa mtandao wa Alqaeda alikuwa amejificha hapo.