Magufuli: Saddam alikuwa rais wa Kuwait!!

Pia ameishasema yeye sio mwanasiasa ni mtendaji

Hiyo ni disqualification moja kubwa sana tayari. rais lazima pia awe mwanansiasa! Utaongozaje nchi kama wewe sio mwanasiasa? Hii ina maana atakuwa anaendeshwa tu na wale wanasiasa, si ndio? Tunataka rais ambaye ni mwanasiasa na ni mtendaji pia. Hizi sifa anazo Lowasa? Kikwete alikuwa mwanansiasa sio mtendaji. Lowasa ni mwanasiasa na ni mtendaji ndio maana kwa muda mfupi aliokuwa waziri mkuu alimfunika kabisa kikwete, na hii ndio ilikuwa chanzo cha kikwete kumchukia.
 
Barabara zenyewe usikute takwimu za uongo! Kwani nikisema barabara ya kutoka nzega hadi mwanza ni kilomita laki nne elfu ishirini na tatu mia mbili sabini na tatu nani atabisha! Provided watu wenyewe sio wafuatiliaji

Kwa ile confidence ahaaa ni wa kuwait nimeamini tulikuwa tunadanganywa sana na hizo data ziliOkuwa zinatolewa .
 
Tatizo lake ni kupenda mijisifa ya kijinga.
Anajikuta anaropoka tu ili watu wacheke. Mi namuona kama Political Comedian kama Mtikila.
Ameshazoea kuwavunnga watu na mitakwimu yake isiyo na kichwa wala miguu ya idadi ya samaki ,ngombe,barabara nk vitu ambavyo si mwananchi wa kawaida wala mtaalam wa takwimu anaweza kuvithibitisha kuwa ni sahihi!
Nadhani aishie kuhesabu idadi ya wanafamilia yake na idadi ya vyumba na vitanda nyumbani kwake!
 
naomba Mzee Lowasa aongeze vipaombele iwe ni Elimu,Elimu,Elimu,Elimu,Elimu manake kama hali halisi ndiyo hii tunakazi kwenye Elimu
 
Huyu jamaa ukichanganya na uwezo wake mdogo wa lugha ukilinganisha na ngazi ya eleimu aliyofikia basi lazima tuseme hapa tunauziwa mbuzi kwenye gunia!
 
Karibu hadi ndani mgeni. Jisikie upo nchini kwenu. Huku kwetu mgombea mmoja wa kiti cha uraisi ambae pia ni waziri anasema sadam husein alikua raisi wa Kuwait, raisi aliepo madarakani ndie baba wa taifa na ashafariki, na pumba nyingine kibao. Waziri wa mambo ya nje anasema Balali ameugua July 2008 akafa May 2008. Naogopa kumsema JK..... Hii ni trela
 
Huku ndio utakutana na malofa wenye akili fupi kuliko nyumbu na wakinunuliwa viroba tu utaona mikono yao hewani na wanaamriwa kugeuzwageuzwa huku wakiita jina la anayewageuza
 
Kina cha maji cha bwawa la Mtera kimepungua kwa megawatt kadhaa-Simbachawene
 
Saddam alikwisha wahi kuiteka Kuwait na ndiyo mwanzo wa kilichompelekea kushambuliwa na mataifa makubwa yote duniani mpaka kuuliwa.

Hivi mleta mada hiyo shule ulienda kusomea ujinga?

Haàhaaaaa sio chuki ya uislamu tena maana ww ni iislamu na ccm tu kichwani mwako.pole so unataka kutuaminisha kuwa alichosema magufuli ni sahihi wala hakukosea? Duuh kweli kichwa kimeishiwa ubongo.
 
Huku ndio utakutana na malofa wenye akili fupi kuliko nyumbu na wakinunuliwa viroba tu utaona mikono yao hewani na wanaamriwa kugeuzwageuzwa huku wakiita jina la anayewageuza
Na wewe unaamini sadam alikua rais wa kuwait/libya?
 
Back
Top Bottom