Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Wale mliomsikia Rais Magufuli alichosema leo kuhusu sera ya nishati ya umeme
mtakubaliana na mimi alichofanya leo Magufuli ni 'kumpinga waziwazi'
waziri wake wa nishati ndugu Muhongo....

nimewahi kuleta thread humu nikiuliza anayoyasema Muhongo ndo aliyotumwa
na Magufuli?Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Tunaweza kusema sasa kuwa Muhongo alikuwa 'ana sera zake binafsi'
za nishati alizokuwa anazitekeleza na sera za Rais Magufuli ni tofauti
na za Muhongo

Muhongo toka ateuliwe amekuwa anazungumza kuhusu 'wawekezaji binafsi'
kuzalisha umeme na Tanesco kununua tu

akisema ndo solution ya matatizo ya umeme Tanzania

Leo Rais Magufuli kasema hataki kusikia tena biashara za kununua umeme na kukodisha
mitambo na mambo ya mikataba na kampuni binafsi
Tanesco ijiimarishe izalishe yenyewe....

Sasa najiuliza je hii sio confusion now?
why Muhongo aendelee kuwa waziri?
why Magufuli asimteue anaemuona anaelewa sera zake?

Je wawekezaji waliomsikiliza Muhongo waki invest mabilioni wakiwa
na imani kuwa 'muelekeo ni Tanesco kununua tu na si kuzalisha yenyewe si wataingizwa mkenge?

Niseme ingawa binafsi naona Magufuli yuko sahihi kwa hili
lakini hii 'confusion' inaweza leta shida huko mbele....

Kama Muhongo anatofautiana kimtazamo na Rais Magufuli kwenye sera za nishati ni bora
aondoke au aondolewe haraka asije sababisha 'mkanganyiko' huko mbele

Na Rais Magufuli awe very clear na sera ya nishati
tueleweke muelekeo ni upi? ili hata TANESCO nao wajipange huku wakijiamini kuwa
wapo sawa kisera na mkuu wa nchi
Kuliko kuwa na waziri anaewaambia 'wajiandae kuachia uzalishaji'
huku Rais anawaagiza 'wajiimarishe kwenye kuzalisha'
hii confusion ni jipu kubwa
kamanda nadhani hujaelewa mustakabali mzima wa Magufuli na Mhongo. embu take time na review the whole issu
 
Najaribu kuuchukulia katika postive uteuzi wa muongo baada sioni tija kwakweli, anaishia kupoteza imani ya watu kuamini ufanisi wake katika wizara hii.

uongozi inatakiwa upendwe na majority, hizi confusion anazotengeneza zinamuongezea wasio muamina na kutokuwa na imani na yeye. hazimpi umaarufu bali anaonekana ndo waziri mzigo kuliko wote yani kilaza

kutokana na hizi confusion hata kama aalikuwa ni mzuri kikazi automatic ataishia kufanya madudu tu.

najua amewekwa kisiasa kurinda heshima ya serikari iliyopita, na scandal zake. this guy is huge political burden, and anamuaibisha magufuli na kuonekana utawala usio na vision
Huyu ndio katika wale watakaoachwa kwa aibu.
 
Unajua siku Magufuli atakapo badilisha katiba ajiongeze mda kuna watu
watastuka kama vile hawaoni huu mwanzo...
hao mawaziri kina Makamba wanaomsifia kinafiki now huku
wakimsubiri amalize miaka 10 wagombanie kumrithi watabaki mdomo wazi
wakati hili lipo waazi kabisa ukilitazama
Tatizo la kushangilia udikteta ni kwamba udikteta hauna mipaka. Utasema rais kufanya udikteta ni sawa katika jambo unalotaka, yeye atatumia nafasi hiyo kufanya udikteta mpaka katika jambo usilotaka.

Utafurahia rais kufukuza vijana wasio na kazi mjini leo, kesho watalalamika hawana pa kulima, rais huyo huyo atakunyang'anya shamba lako ili awape wao walime. Unatakiwa uendelee kushangilia tu, maadam ushakubali kushangilia udikteta.

La sivyo utawala wa sharia uchukue mkondo.
 
Tatizo la kushangilia udikteta ni kwamba udikteta hauna mipaka. Utasema rais kufanya udikteta ni sawa katika jambo unalotaka, yeye atatumia nafasi hiyo kufanya udikteta mpaka katika jambo usilotaka.

Utafurahia rais kufukuza vijana wasio na kazi mjini leo, kesho watalalamika hawana pa kulima, rais huyo huyo atakunyang'anya shamba lako ili awape wao walime. Unatakiwa uendelee kushangilia tu, maadam ushakubali kushangilia udikteta.

La sivyo utawala wa sharia uchukue mkondo.

Unakumbuka kabla Tony Blair hajawa waziri mkuu
kuna mtu alitoa kitabu akimuonesha Tony Blair akiwa na macho ya kishetani hivi
title ilikuwa 'The New Danger' ....kipindi hiko Blair anakuja na 'The New Labor'..
huwa namuona Magufuli kwenye picha ya aina ile....
watu hawajui 'hatari' ambayo anaileta bado...
 
Muendelezo wa siasa za fisi....kufuatilia mambo yasiyo na mantiki.
Hivi waziri kutofautiana rais bado tu huoni ni tatizo?.kuna maana gani ya kua na waziri asiye elewa matakwa ya rais juu ya wizara husika?.

Wakati mwingine ni vizuri kuto shabikia tuu kila jambo.
 
Nilishaacha kupost na Kujadili siasa za nchi hii kule Facebook na very soon hapa napo nitaacha kujadili siasa za katika hili jukwaa
 
Mawaziri wetu sio watu wa principles.Hawasimamii wanachokisema.
Muhongo angetakiwa ajiuzulu mwenyewe.
 
The Boss

Kuna tofauti kubwa kati ya wawekezaji binafsi katika sekta ya umeme na Tanesco kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme.

Fikiria japo kiduchu utaelewa tu.

Hint: PPP
 
The Boss

Kuna tofauti kubwa kati ya wawekezaji binafsi katika sekta ya umeme na Tanesco kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme.

Fikiria japo kiduchu utaelewa tu.

Hint: PPP

Magufuli leo alikuwa very clear Tanesco ijiimarishe izalishe umeme yenyewe
tofauti na Muhongo alisema na tulileta threads hapa mara kadhaa
alisema namnukuu 'solution ni umeme uzalishwe na sekta binafsi kwa asilimia 90'

Na Tanesco alitaka kuigawa isizalishe kabisa
upande wa generation hatimae uwe privatized..

Tofauti ipo wazi kabisa na kauli ya Magufuli leo
 
kamanda nadhani hujaelewa mustakabali mzima wa Magufuli na Mhongo. embu take time na review the whole issu
Mkuu hebu tumwagie hapa jamvini jinsi ambavyo wewe umewaelewa maana wote hapa lengo kuu ni kujenga nyumba moja.
 
Mawaziri wameshindwa muelewe Magu ni mfuasi wa ujamaa, mawaziri wao wanawaza kibepari,
By the way Magu anahitaji msaada mkubwa wa kisera na fikra,
Hajitambui anataka nini tofauti na majipu
Hivi kati ya Magu na wew yupi ambae hajitambui?

Wakati mwingine kukaa kimya kuna maana sana
 
Si ndo maana anaanza kusema watu wakamatwe wapelekwe kwenye makambi
kisa wanacheza pool...huku anatoa amri za kupunguza wafanya kazi kwenye mashirika..

yaani akiachwa kila kitu kiende ubongo wake unavyo mtuma...the worst is yet to come...
Una kazi kubwa sana....
 
Muhongo huwa haongei kwa fact from the ground , yeye huongea kutokana na theory anazo soma. Mgufuli anaongea kile anacho kiamini kinatekelezeka na ndio maana anafuatilia sana kila mradi na anaona uwezekano wa tanesco kujiendesha upo.
Binafsi simwamini kabisa Muhongo kwani anategemea vyeti vyake na cv yake ndivyo vitatuletea umeme. Kumbuka kuna wakati alisema wawekezaji wa tz hawaweI kuwekeza kwenye gas kwa kuangalia figures za fedha kumbe kwenye biashara hakuna figure kubwa .

Magufuli yupo.sahihi na kama kuna uwezekano muhongo awekwe pembeni maana inaonekana sio msikivu.
Ndugu zangu, ukiondoa doa la Escrow, pamoja na mapungufu ya kibinadam aliyonayo ambalo ni jambo la kawaida kwa kila binadam, Prof S Muhongo ni kati ya Viongozi ninaowaanini na kuwakubali. Kwanza siasa yeye hajui anakupa za uso(zikiwa ni FACTS TUPU).
Katika awamu ya tano, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ujenzi, na Waziri wa Kilimo na Uvuvi, so far ndiyo ninaowakubali hadi leo hii. Kwanza wameonyesha ukomavu kiutendaji, media hajatumia sana kujipa kick.
 
Ni dhahiri kuna mgongano wa mawazo.
Jambo amabalo kwangu binafsi naona ni sahihi. Wote ni wasomi wa level ya PhD na kuendelea, lazima kimtizamo kuna sehemu kila mmoja atakua na fikra yake. Lakini mwishowe fikra zao waziharmonize na kuja na kitu kimoja
 
Ninyi endeleeni kumzungushia mikono lowassa

Tatizo la watu wengi wa nchi yetu ni kwamba wamekwama katika one track mind ya UKAWA/CCM Lowassa/Magufuli.

Umejuaje mimi namuunga mkono Lowassa?

Au kwako wewe mtu yeyote anayeisema serikali ya Magufuli basi lazima ni mshabiki wa Lowassa?

Unaweza kunipa hata post moja niliyomshabikia Lowassa hapa kama ushahidi wa kwamba fikra zako si kwa sababu ya tongotongo za ujinga wa msingi tu?
 
Back
Top Bottom