Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Muhongo ni engine kubwa kavunja rekodi ya kuteuliwa mara mbili kwenye wizara ile ile na Marais wawili tofauti.
namkubali kwa utendaji wake uliotukuka tokea mwezi wa kwanza tunalipia umeme sh 5000 mwezi mzima zero tariff na hakuna mambo ya kero za service charge za kila mwezi. isitoshe siku hizi umeme ni masaa ishirini na nne.
mimi sikuelewi ukisema aondolewe bali adumu hapo hapo kwa kutuondolea kero za ukosefu wa umeme wa mara kwa mara na upunguzwaji wa gharama zake
 
Hivi hawa vikatuni wa uongozi wanakaa hata kwenye baraza la mawaziri na kujadiliana cha kufanya na kusema?
Haya sio mapya hata awamu ya 4 yalikuwa hivi hivi! Mwingine alisema hakuna haja ya katib mpya, mkuu wa kaya akaja akasema kuna haja ya katiba mpya! Kama rais kwanini usimwite waziri husika ukamwambia akabatilishe kauli yake kuliko kujitokeza kwa wananchi na kumpinga!
 
Tatizo kubwa ni kukosa sera ya nishati iliyokubalika kwa wananchi.
...Katika nchi hii haijawahi tokea wananchi wakashirikishwa katika kuandaa sera, kufikia hatua ya kuikubali au kuikataa.

...Sera ya nishati iliyopo inatosha kwa sasa, na bado kuna maboresho yake, sijui kama yamepitishwa. Tatizo ni utekelezaji.

...Actually, ukisoma hizo sera, unaelewa mashaka ya Kiranga, The Boss na Nguruvi3.

Ndio maana kila kiongozi anakuwa na mtizamo wake. Ila Muhongo inabidi asome alama za nyakati vinginevyo atawaingiza mkenge madalali wenzake

...Mitazamo kadhaa katika mambo mbalimbali, haijulishwi na sera zilizopo. Ndio maana wengine mnadhani hakuna sera. Zipo! Zinajaa vikapu!

...Prof. Muhongo is right as per existing Energy Policy.

PS. Tusipofuata hizi sera -kama hazifai tuandae nyingine- hutatafanikiwa, tutatafutana ubaya tu.
 
Hili swali najiuliza kila siku
waziri anaongea a,b,c
anakuja Rais anasema x,y,z...
jambo ni hilo hilo.....unabaki mdomo wazi
JPM amejikanganya... na wajanja wameshamjua sasa wanamjaza king, kama aliyemtangulia... soon tutarudi kulekule

JK did put our state into an unorganized chaos on purpose, na hao stewards wa unorganized chaos wamemzunguka JPM, na kwa bahati mbaya sana, yuko busy na "operations" badala ya "strategies"

ticking time bomb!!!
 
Kazungukwa na watu wale wale
na anaamini mikwara ndo ita solve ufisadi....
 
...Katika nchi hii haijawahi tokea wananchi wakashirikishwa katika kuandaa sera, kufikia hatua ya kuikubali au kuikataa.

...Sera ya nishati iliyopo inatosha kwa sasa, na bado kuna maboresho yake, sijui kama yamepitishwa. Tatizo ni utekelezaji.

...Actually, ukisoma hizo sera, unaelewa mashaka ya Kiranga, The Boss na Nguruvi3.

...Mitazamo kadhaa katika mambo mbalimbali, haijulishwi na sera zilizopo. Ndio maana wengine mnadhani hakuna sera. Zipo! Zinajaa vikapu!

...Prof. Muhongo is right as per existing Energy Policy.

PS. Tusipofuata hizi sera -kama hazifai tuandae nyingine- hutatafanikiwa, tutatafutana ubaya tu.
Hivi katika mtizamo wako kuna sera inaweza kufanikiwa bila kushirikisha wananchi? Au tunajidanganya? Unaposema inatosha kwa sasa ina maana hii sera haina maono ya miaka ijayo? Mzee hizi sera za zilizojaa kwenye vikapu ambazo hazipo kwenye mioyo na vichwa vya watendaji wa serikali na wanachi zinatupeleka kuzimu.
 
Hivi katika mtizamo wako kuna sera inaweza kufanikiwa bila kushirikisha wananchi? Au tunajidanganya?

...Kushirikisha wananchi kuna tafsiri nyingi. Kwa ufupi, wanashirikishwa, kupitia wawakilishi mbalimbali, na wao wenyewe katika ngazi tofauti.

...Sera nyingi, ni kwa ajili ya matumizi ya Serikali, kama mwongozo wa kutoa huduma au kutekeleza jambo kwa manufaa ya nchi. Ambayo, ni kazi ya Serikali.

Unaposema inatosha kwa sasa ina maana hii sera haina maono ya miaka ijayo?
...Umeisoma? Au, umezisoma? Maana ziko mbili hapo, na zote zinaongelea future ya nishati na umeme Tanzania.

Mzee hizi sera za zilizojaa kwenye vikapu ambazo hazipo kwenye mioyo na vichwa vya watendaji wa serikali na wanachi zinatupeleka kuzimu.
...Hizo sera hutungwa na kuandaliwa na watendaji wa Serikali. Zinatoka vichwani mwao!

...Hebu soma japo moja kati ya hizo mbili, halafu tuendelee na hoja! Au unasemaje?
 
Alifuta semina elekezi nadhan ulikua ndio muda wa kupeana msimamo na mitazamo
 
Hata mimi nimeona kuna confusion.Ingekuwa vema kama wangekuwa na sera moja.Hata hivyo mimi namuunga mkono Magufuli.Electricity to me is a strategic commodity.Kama uzalishaji wake ukiwa totally in private hands,jamaa ni rahisi kutuyumbisha.No,tuisaidie TANESCO kiutendaji na kifedha uzalishie,isafirishe na idistribute umeme majumbani,wanaweza.Hili suala la TANESCO kuwa middle ni upuuzi.
Wale mliomsikia Rais Magufuli alichosema leo kuhusu sera ya nishati ya umeme
mtakubaliana na mimi alichofanya leo Magufuli ni 'kumpinga waziwazi'
waziri wake wa nishati ndugu Muhongo....

nimewahi kuleta thread humu nikiuliza anayoyasema Muhongo ndo aliyotumwa
na Magufuli?Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Tunaweza kusema sasa kuwa Muhongo alikuwa 'ana sera zake binafsi'
za nishati alizokuwa anazitekeleza na sera za Rais Magufuli ni tofauti
na za Muhongo

Muhongo toka ateuliwe amekuwa anazungumza kuhusu 'wawekezaji binafsi'
kuzalisha umeme na Tanesco kununua tu

akisema ndo solution ya matatizo ya umeme Tanzania

Leo Rais Magufuli kasema hataki kusikia tena biashara za kununua umeme na kukodisha
mitambo na mambo ya mikataba na kampuni binafsi
Tanesco ijiimarishe izalishe yenyewe....

Sasa najiuliza je hii sio confusion now?
why Muhongo aendelee kuwa waziri?
why Magufuli asimteue anaemuona anaelewa sera zake?

Je wawekezaji waliomsikiliza Muhongo waki invest mabilioni wakiwa
na imani kuwa 'muelekeo ni Tanesco kununua tu na si kuzalisha yenyewe si wataingizwa mkenge?

Niseme ingawa binafsi naona Magufuli yuko sahihi kwa hili
lakini hii 'confusion' inaweza leta shida huko mbele....

Kama Muhongo anatofautiana kimtazamo na Rais Magufuli kwenye sera za nishati ni bora
aondoke au aondolewe haraka asije sababisha 'mkanganyiko' huko mbele

Na Rais Magufuli awe very clear na sera ya nishati
tueleweke muelekeo ni upi? ili hata TANESCO nao wajipange huku wakijiamini kuwa
wapo sawa kisera na mkuu wa nchi
Kuliko kuwa na waziri anaewaambia 'wajiandae kuachia uzalishaji'
huku Rais anawaagiza 'wajiimarishe kwenye kuzalisha'
hii confusion ni jipu kubwa
 
Tatizo ni kuwa Magu na Muhongo wote ni wataalamu katika fani zao lakini hawajui chochote kuhusu siasa. Wote wameshika nyundo wakidhani hata ukucha hushughulikiwa kwa nyundo. Iko siku Magu atakuja kutumbua kichwa akidhani ni jipu na Muhongo akaleta wawekezaji wa kuja kuuza hata karanga na sigara katika ungo.

Yale maneno ya Baba wa Taifa kuwa "Ili tuendelee, tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora," yamepuuzwa. Watu wapo, ardhi bado ipo kidogo baada ya kuifisidi, lakini hatuna siasa safi (sera, hatijui kama tunafuata siasa za kibepari au za kijamaa) na hatuna uongozi bora bali bora uongozi.
 
...Kushirikisha wananchi kuna tafsiri nyingi. Kwa ufupi, wanashirikishwa, kupitia wawakilishi mbalimbali, na wao wenyewe katika ngazi tofauti.

...Sera nyingi, ni kwa ajili ya matumizi ya Serikali, kama mwongozo wa kutoa huduma au kutekeleza jambo kwa manufaa ya nchi. Ambayo, ni kazi ya Serikali.

...Umeisoma? Au, umezisoma? Maana ziko mbili hapo, na zote zinaongelea future ya nishati na umeme Tanzania.

...Hizo sera hutungwa na kuandaliwa na watendaji wa Serikali. Zinatoka vichwani mwao!

...Hebu soma japo moja kati ya hizo mbili, halafu tuendelee na hoja! Au unasemaje?
Kama zipo kwa nini rais anahubiri kulia waziri anatenda yake kushoto. Raisi anapiga ndombolo waziri anacheza ngololo! Hii inadhihirisha Raisi ameona madhifu ya waziri na sera zisizokuwa na maslahi kwa taifa zenye kuwakumbatia madalali na wapiga dili, ndio sababu anakuwa na mtizamo tofauti. Ifike mahala tuwe na uzalendo wa kweli kwa nchi yetu!
 
kama muhongo anakosea watarekebishana huko mbele,,,,walishaambiwa wachukue maamuzi hta kama n mabaya watarekebishana huko mbele ya safari....#tusiwe wepesi kusahau
 
Kile kipengele cha usiri (non-disclosure) wa mikataba kinachodhamiria kuwalinda wawekezaji ndicho kinachotimiwa (uchochoro) na viongozi wetu kutengeneza mikataba mibovu.

Swali, hivi kampuni lililojipambanua linaweza kuweka uwekezaji mkubwa mfano uwekezaji wa mitambo ya umeme (multi-billions tsh.) alafu dhamira iwe ni kutapeli? Napata shaka kukubali majibu ya ndio, hata kwa upande mwingine (otherwise).

Ukitaka kujua kwanini ni hapana kwa mifano, litafute shauri la BIWATER la baraza la usuluhishi wa uwekezaji.

Hivyo naona hakuna hicho kinachoitwa "mparaganyiko" au "confusion" kama mtoa mada anavyoeleza.

Lakini, ile hoja ya hatuna fedha za kutosha kugharamia miradi mikubwa mfano, ujenzi wa mitambo binafsi ya TANESCO ya kufua umeme ndiyo inayombeba waziri wa nishati na madini.

Lakini, zaidi ya hapo, mh. Raisi anahamasishwa na dhamira yake ya dhati mfano kuweza kushurutisha makusanyo ya kodi, tozo na mapato ya serikali kwa ujumla wake, tena ya ndani kwa mamlaka husika na kupata fedha za kugharamia uwekezaji huo mkubwa. Mifano ni dhahiri kwa mfuatiaji wa siasa changa za awamu ya tano. Fedha zilizotolewa kwa mahakama, upanuzi wa barabara, ATCL n.k

Nadhani ile hoja ya waziri wa nishati iliyopata umaarufu awamu ya nne imepitwa na msimu. Mtoa mada anapaswa kulitambua hilo. Sababu ni moja au mbili hivi. Ule mradi wa umeme vijijini REA ulifanikiwa sana. Hapa nina ushahidi wa Alibi kwa vijiji vingi (samahani kwa kukosa neno la kiswahili mbadala wa alibi).

Tena kuhusu upatikanaji wa umeme. Kwa kipindi kifupi shirika lilinyooka na umeme "angalau" ukawa wa uhakika tofauti na baada yake. Rudi nyuma kidogo kipindi kifupi na utazame tatizo la umeme wakati tunaelekea kwenye uchaguzi na kwenye uchaguzi wenyewe. Baadae akarejea na tumerudi kule kwenye "angalau" umeme hausumbui. Kwa matumaini "angalau" itajitenga. Time will tell

Kwa kipindi hiki sasa. Siasa mbeleko za awamu ya nne zizikwe na tuangalie utendaji. Hali ya kutafuta "kiki" katika awamu ya tano kupitia skendo ya escrow hazina tena nafasi. "If you want to find pleasure in others' miafortunes, go to hell and ask the devil to crown you " nyapara"

Ni hayo tu.

Fake ID. Likemikelove

PS. Radhi kwa matumizi ya kimombo. Nimezaliwa tz, Nimekulia tz na nimesoma tz, tena S. Kayumba from ground zero mpaka elimu ya juu. Na nimekuwa nikizungumza kiswahili tangu awali. Ajabu ni kuwa siwezi kujieleza kwa kiswahili kama unavyoona hapo juu. Badala yake, lugha ninayoweza kujieleza vizuri,100℅ ni kiingereza.

Nilichofanya hapo juu ni kutafsiri moja kwa moja kutoka kiingereza kwenda kiswahili.

Kama umeshindwa kuona hapo juj ubovu kwangu wa kujieleza kwa kiswahili, pengine tunashiriki tatizo moja.

USHAURI
 
Kile kipengele cha usiri (non-disclosure) wa mikataba kinachodhamiria kuwalinda wawekezaji ndicho kinachotumiwa (uchochoro) na viongozi wetu kutengeneza mikataba mibovu.

Swali, hivi kampuni lililojipambanua linaweza kuweka uwekezaji mkubwa mfano uwekezaji wa mitambo ya umeme (multi-billions tsh. investment) alafu dhamira iwe ni kutapeli? Napata shaka kukubali majibu ya ndio, hata kwa upande mwingine (otherwise).

Ukitaka kujua kwanini ni hapana kwa mifano, litafute shauri la BIWATER la baraza la usuluhishi wa migogoro ya kimataifa ya uwekezaji.

Hivyo naona hakuna hicho kinachoitwa "mparaganyiko" au "confusion" kama mtoa mada anavyoeleza.

Lakini, ile hoja ya hatuna fedha za kutosha kugharamia miradi mikubwa mfano, ujenzi wa mitambo binafsi ya TANESCO ya kufua umeme ndiyo inayombeba waziri wa nishati na madini.

Lakini, zaidi ya hapo, mh. Raisi anahamasishwa na dhamira yake ya dhati mfano kuweza kushurutisha makusanyo ya kodi, tozo na mapato ya serikali kwa ujumla wake, tena ya ndani kwa mamlaka husika na kupata fedha za kugharamia uwekezaji huo mkubwa. Mifano ni dhahiri kwa mfuatiaji wa siasa changa za awamu ya tano. Fedha zilizotolewa kwa mahakama, upanuzi wa barabara, ATCL n.k

Nadhani ile hoja ya waziri wa nishati iliyopata umaarufu awamu ya nne imepitwa na msimu. Mtoa mada anapaswa kulitambua hilo. Sababu ni moja au mbili hivi. Ule mradi wa umeme vijijini REA ulifanikiwa sana. Hapa nina ushahidi wa Alibi kwa vijiji vingi (samahani kwa kukosa neno la kiswahili mbadala wa alibi).

Tena kuhusu upatikanaji wa umeme. Kwa kipindi kifupi shirika lilinyooka na umeme "angalau" ukawa wa uhakika tofauti na baada yake. Rudi nyuma kidogo kipindi kifupi na utazame tatizo la umeme wakati tunaelekea kwenye uchaguzi na kwenye uchaguzi wenyewe. Baadae akarejea na tumerudi kule kwenye "angalau" umeme hausumbui. Kwa matumaini "angalau" itajitenga. Time will tell

Kwa kipindi hiki sasa. Siasa mbeleko za awamu ya nne zizikwe na tuangalie utendaji. Hali ya kutafuta "kiki" katika awamu ya tano kupitia skendo ya escrow hazina tena nafasi. "If you want to find pleasure in others' misfortunes, go to hell and ask the devil to crown you " nyapara"

Ni hayo tu.

Fake ID. Likemikelove

PS. Radhi kwa matumizi ya kimombo. Nimezaliwa tz, nimekulia tz na nimesoma tz, tena S. Kayumba from ground zero mpaka elimu ya juu. Na nimekuwa nikizungumza kiswahili tangu awali. Ajabu ni kuwa siwezi kujieleza kwa kiswahili kama unavyoona hapo juu. Badala yake, lugha ninayoweza kujieleza vizuri,100℅, ni kiingereza.

Nilichofanya hapo juu ni kutafsiri moja kwa moja kutoka kiingereza kwenda kiswahili.

Kama umeshindwa kuona hapo juu ubovu kwangu wa kujieleza kwa kiswahili, pengine tunashiriki tatizo moja.

USHAURI
 
Wale mliomsikia Rais Magufuli alichosema leo kuhusu sera ya nishati ya umeme
mtakubaliana na mimi alichofanya leo Magufuli ni 'kumpinga waziwazi'
waziri wake wa nishati ndugu Muhongo....

nimewahi kuleta thread humu nikiuliza anayoyasema Muhongo ndo aliyotumwa
na Magufuli?Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Tunaweza kusema sasa kuwa Muhongo alikuwa 'ana sera zake binafsi'
za nishati alizokuwa anazitekeleza na sera za Rais Magufuli ni tofauti
na za Muhongo

Muhongo toka ateuliwe amekuwa anazungumza kuhusu 'wawekezaji binafsi'
kuzalisha umeme na Tanesco kununua tu

akisema ndo solution ya matatizo ya umeme Tanzania

Leo Rais Magufuli kasema hataki kusikia tena biashara za kununua umeme na kukodisha
mitambo na mambo ya mikataba na kampuni binafsi
Tanesco ijiimarishe izalishe yenyewe....

Sasa najiuliza je hii sio confusion now?
why Muhongo aendelee kuwa waziri?
why Magufuli asimteue anaemuona anaelewa sera zake?

Je wawekezaji waliomsikiliza Muhongo waki invest mabilioni wakiwa
na imani kuwa 'muelekeo ni Tanesco kununua tu na si kuzalisha yenyewe si wataingizwa mkenge?

Niseme ingawa binafsi naona Magufuli yuko sahihi kwa hili
lakini hii 'confusion' inaweza leta shida huko mbele....

Kama Muhongo anatofautiana kimtazamo na Rais Magufuli kwenye sera za nishati ni bora
aondoke au aondolewe haraka asije sababisha 'mkanganyiko' huko mbele

Na Rais Magufuli awe very clear na sera ya nishati
tueleweke muelekeo ni upi? ili hata TANESCO nao wajipange huku wakijiamini kuwa
wapo sawa kisera na mkuu wa nchi
Kuliko kuwa na waziri anaewaambia 'wajiandae kuachia uzalishaji'
huku Rais anawaagiza 'wajiimarishe kwenye kuzalisha'
hii confusion ni jipu kubwa
Ukiangalia kwa haraka haraka utaona Muhongo hayupo sahihi, ila ukaanza kuchimba ndani zaidi utagundua tatizo lipo kwa Mh Rais. Ki vipi? Mimi naamini hakuna waziri hata mkuu wa mkoa au makatibu wanaoelewa nini hasa Raisi anataka. Kuna sera za Chama, kuna slogan ya hapa kazi tu, na kuna mtazamo wa Rais then kuna facts! Tatizo hiko hapa kuna wanaofanya kutokana na sera, wengine kutokana na facts na wengine kutokana na Slogan na wengine kwa mtazamo wa Rais. Kwa namna hii lazma watapishana tu, ndio maana wanaofanya kwa mtazamo wa rais wanafukuza kila mtendaji aliyekosea. Hivyo Mkuu sio Muhongo tu utakuja ona na wengine wanavyopishana na rais ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom