Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Magufuli kama mtu mpenda haki hebu atende haki ya urais zanzbr na meya dar
 
suala la ku deal na malaya limewapa polisi ulaji,wanavamia hadi ma lodge sasa hivi na hili la pool table ni deal nyingine...hehehehehehe...ptuuuuu

Hahahah tulieni ..... Mlimsifu kuwa ana kasi sana.... Sasa anakimbia mpaka anapiliza kwao.....

Najiuliza wanaosema nidhamu imerudi na rushwa hakuna serikalini wanaongea kwa facts zipi?
 
Mimi nasema wafanye wanavyojua lakini watanzania wanataka umeme wa uhakika
 
Kuanza tu kufikiria kuwa kuna kipya ambachop hii serikali inaweza kuleta ni kama kusubiri meli airport.......

Hakuna mwenye lengo zuri hapo nakuambia,watu ni wale wale na ofisi ni zile zile.......

Kama huniamini subiri muda ukuambie.....

Anatumia mbinu za miaka ya 1970 kutatua matatizo ya 2016!
Dunia na mifumo yake inabadilika kila siku.China, Venuzuela, Zimbabwe,Bolivia,Russia, Cuba zote zimelekea upande wa kibepari yeye bado anawazo huko kisa kafananishwa na Nyerer

Sijui katiba mpya atasimamia chama au nchi??
 
Mramba eti keshakuwa mshauri wa hospitali cjui ana elimu ya utabibu yule au kuogopana kuwekana mbaroni?
 
Anatumia mbinu za miaka ya 1970 kutatua matatizo ya 2016!
Dunia na mifumo yake inabadilika kila siku.China, Venuzuela, Zimbabwe,Bolivia,Russia, Cuba zote zimelekea upande wa kibepari yeye bado anawazo huko kisa kafananishwa na Nyerer

Sijui katiba mpya atasimamia chama au nchi??

Kwa style yake hii usishangae watu wakaanza kuulizwa vitambulisho
na kesi za uzururaji zikaanza tena
 
Shida ya nchi hii iko hapo
mtu hana team ya wataalam na kama anayo haisikilizi

Sasa Magufuli hotuba tu ya kuandikiwa haisomi
anazungumza yake...jiulize team ya washauri ya uchumi ataisikiliza?

nimewahi toa mfano humu
Makamu wa Rais wa Marekani sio mtendaji..hafanyi maamuzi
lakini still ana washauri wa kila sekta
unakuta Makamu wa Rais ana mshauri wa uchumi...
Rais ana mshauri wa uchumi na kuna mawaziri husika nao wana washauri...

Sisi Rais anaibuka tu na kusema kitu hata washauri hawana taarifa nacho
Umenikumbusha enzi ya kampeni washauri wake kutwa kulalamika jamaa hasikii ushauri,
Ni kiazi by default
 
Kwa mawazo yangu Rais kamweka Muhongo kiporo aendelee kuropoka nafhani wizara hiyo Rais kisha anza kutafuta mtu ila bado anaandika jina kisha anafuta anaandika jingine tena anamfuta hajampata waziri wa kufiti wizara hiyo.

Muhongo ni mtaalamu mzuri aliyebobea kwenye fani ya madini, anajua michorongo, aina na mambo kama hayo lakini hajui lolote juu ya utawala, sera na uongozi wa nishati na madini. Walivyomwona ni mtaalamu wa madini wakafikiri atakuwa kiongozi mzuri wa wizara ya madini. Mpelekeni Geita Gold mine mwone atakavyokuchoreeni njia na mikondo ya dhahabu si kuongoza.
 
Kuanza tu kufikiria kuwa kuna kipya ambachop hii serikali inaweza kuleta ni kama kusubiri meli airport.......

Hakuna mwenye lengo zuri hapo nakuambia,watu ni wale wale na ofisi ni zile zile.......

Kama huniamini subiri muda ukuambie.....


Mkuu naona huamini wala hutaki kuamini kabisa. Dah hata Tomaso hakufikii
 
Kwa style yake hii usishangae watu wakaanza kuulizwa vitambulisho
na kesi za uzururaji zikaanza tena
Traffic wamesonga mbele kwenye kupiga tochi kuliko Rais, sa hivi wanapiga tochi kwa nyuma unakuta fine inakusubiria mbele
Rais should think different and come up with long term solution
 
Kwa taratibu za utandaji, waziri ndie mdomo wa rais kwenye sekta inayohusika. Ndie anazungumza aliloamua rais na baraza lake kuhusu sekta hiyo. Tofauti kidogo tu lazima waziri aondoke. Nyerere alitofautiana na Mtei kwenye suala la IMF wakati, ingawa walitofautiana kwa siri ilibidi Mtei aondoke. Ndivyo serikali inavyoendeshwa kinyume chake ni vurugu tu.

Upo sahihi japo umesahau kuwa Rais ana Mamlaka hata ya kuzungumza jambo ambalo halijajadiliwa kwny Cabinet au na Waziri husika Then ndio anampa Maelekezo Waziri au Chief Secetary aandae kama hoja kwny Cabinet Meeting.
Ishu ya Mtei na Nyerere kulitokea Mabishano kabisa kuhusu Kufuata Masharti ya IMF nyerere alikataa ushauri wa Mtei alietaka Mwl akubali kushusha thamani ya fedha yetu (Devaluation of Currency) kama walivolazimishwa na Mabepari wakiwa Msasani, ndipo wakatofautiana Walipotoka pale Mtei akaandika Barua ya kujiuzulu huku Mwl Nyerere akiandika barua ya kufukuza kazi. Dereva alieleta barua ya kufukuzwa alipishana na Dereva aliepeleka barua ya kujiuzulu Ikulu na hili kalisema Mwenyewe Mtei siku ya uzinduzi wa kitabu chake akielezea Kutoka Uchungaji mpaka Govenor wa Bank kuu hivyo sio sahihi sana kufananisha na kilichotokea leo.
 
Muhongo hana kosa kwani Mh Rais anauwezo wa kumuita na kumueleza sera zake kuhusu nishati ..ama baraza la mawaziri siku hizi halikai
 
Lakini hii inaashiria nini? Inatoa picha gani kwa Magufuli? Sio Rais alipaswa tangu awali kabla ya kumpa hiyo kazi angempa Sera....mwelekeo na imani yake ktk sekta hiyo? Hii haituoneshi Mzee Magu Mzee wa ghafla na kuripuka?
Mkuu inawezekana Rais ana vision
Inakuaje Boss hukai na timu yako na kuwaambia unataka Ku achieve nini?

Hii inaonesha dhahiri Mr. President hana vision!
Mkuu inawezekana Rais ana vision but haijawa clearly translated kwa wasaidizi wake ili wajue what is expected and how will be achieved. Leo nimeona Mawaziri walitoa mwelekezo kwa new RCs ambayo ni ya jumla sana, sasa unless kuna dossier ambayo imeandaliwa in advance na watakabidhiwa itakuwa vigumu sana kwao ku translate vision ya ya boss wao.
 
Wale mliomsikia Rais Magufuli alichosema leo kuhusu sera ya nishati ya umeme
mtakubaliana na mimi alichofanya leo Magufuli ni 'kumpinga waziwazi'
waziri wake wa nishati ndugu Muhongo....

nimewahi kuleta thread humu nikiuliza anayoyasema Muhongo ndo aliyotumwa
na Magufuli?Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Tunaweza kusema sasa kuwa Muhongo alikuwa 'ana sera zake binafsi'
za nishati alizokuwa anazitekeleza na sera za Rais Magufuli ni tofauti
na za Muhongo

Muhongo toka ateuliwe amekuwa anazungumza kuhusu 'wawekezaji binafsi'
kuzalisha umeme na Tanesco kununua tu

akisema ndo solution ya matatizo ya umeme Tanzania

Leo Rais Magufuli kasema hataki kusikia tena biashara za kununua umeme na kukodisha
mitambo na mambo ya mikataba na kampuni binafsi
Tanesco ijiimarishe izalishe yenyewe....

Sasa najiuliza je hii sio confusion now?
why Muhongo aendelee kuwa waziri?
why Magufuli asimteue anaemuona anaelewa sera zake?

Je wawekezaji waliomsikiliza Muhongo waki invest mabilioni wakiwa
na imani kuwa 'muelekeo ni Tanesco kununua tu na si kuzalisha yenyewe si wataingizwa mkenge?

Niseme ingawa binafsi naona Magufuli yuko sahihi kwa hili
lakini hii 'confusion' inaweza leta shida huko mbele....

Kama Muhongo anatofautiana kimtazamo na Rais Magufuli kwenye sera za nishati ni bora
aondoke au aondolewe haraka asije sababisha 'mkanganyiko' huko mbele

Na Rais Magufuli awe very clear na sera ya nishati
tueleweke muelekeo ni upi? ili hata TANESCO nao wajipange huku wakijiamini kuwa
wapo sawa kisera na mkuu wa nchi
Kuliko kuwa na waziri anaewaambia 'wajiandae kuachia uzalishaji'
huku Rais anawaagiza 'wajiimarishe kwenye kuzalisha'
hii confusion ni jipu kubwa

Najaribu kuuchukulia katika postive uteuzi wa muongo baada sioni tija kwakweli, anaishia kupoteza imani ya watu kuamini ufanisi wake katika wizara hii.

uongozi inatakiwa upendwe na majority, hizi confusion anazotengeneza zinamuongezea wasio muamina na kutokuwa na imani na yeye. hazimpi umaarufu bali anaonekana ndo waziri mzigo kuliko wote yani kilaza

kutokana na hizi confusion hata kama aalikuwa ni mzuri kikazi automatic ataishia kufanya madudu tu.

najua amewekwa kisiasa kurinda heshima ya serikari iliyopita, na scandal zake. this guy is huge political burden, and anamuaibisha magufuli na kuonekana utawala usio na vision
 
Back
Top Bottom