Magufuli hatakiwi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli hatakiwi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mvaa Tai, Nov 26, 2010.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kuna jamaa mmoja anayehisiwa anafanya kazi miundombinu jana akiwa maeneo ya Mbezi tangi bovu akipata kinywaji, baada ya kuwa amelewa kidogo alikasirika sana kuwasikia watu wa meza ya pili wakisifia uteuzi wa Magufuli na Mwakyembe kwenda miundombinu anadai tokea Jk alipomteua Magufuli na Mwakyembe kuwa mabosi wao wapya, hali ya hewa siyo nzuri sana pale Wizara ya miundo mbinu kila mtumishi anataka ikiwezekana ahamishiwe wizara ya uchukuzi kuepukana na huyu mtu, wenye uwezo wa ku-robe wameanza kufanya hivyo, wafanyakazi wengi hawajafurahishwa maana walisha wahi kufanya kazi chini ya magufuli hali ilikuwa ngumu sana kimaslahi, wanadai ni mtu anayependa sana sifa kwa kuendekeza zaidi maslahi ya Taifa huku akiwaacha watumishi wakihaha kwa kuwabania mianya ya kujipatia pesa za ziada. Huku akijua fika mishahara ya serikali haiendi na wakati.

  Jamaa anasisitiza "Usije ukashangaa ukiona wakandarasi wa barabara wanafunga sana makampuni yao kipindi hiki maana hili eneo litakuwa halilipi kama awali, ukitaka kuamini haya nenda ile wizara ya mifugo na uvuvi uone jinsi wanavyofurahia huyu jamaa kuondoka, mi binafsi simtaki kabisa"


  Jamani tujifunze kutokuyazungumzia masuala ya ofisini tukiwa bar, nina uhakika huyu jamaa hatima yake siyo nzuri. maana waliokuwa wanamsikiliza walikuwa wengi.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Msalimie Bruno Shirima, mkaguzi wa ndani
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu mleta mada... tayari umeonyesha jinsi watu wasivyopenda kuwajibika.

  Wacha waondoke wote watakuja walio serious, tena Magufuli hii ni zamu yake kwenda kwa Odinga kujifunza kwani Odinga anayofanya yote kenya mengine aliyatoa kwa Magufuli

  I am glad wakimbie wenyewe kama hawawezi kazi
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa naona kama umeandika kama sisi wote mafisadi na ya kuwa tuanze kujadili sifa na ubaya wa magufuli

  Titile yako ungebadili kuweka angalau inayomsifia kwa content yako hii! LOL!!
   
 5. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Ahh kumbe ni mawazo ya mlevi..! neways ni mawazo yake.. ila nivyojuwa walevi hawajui wanaongea pumba gani wakiwa nzutu!
   
 6. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi ninavyowafahamu watanzania, Kwangu hii sio HABARI hata kidogo!!!!! Ingekuwa HABARI endapo ningeambiuwa kwamba waliopo wizara hiyo wamefurahi ile mbaya kuletwa kwa Magufuri na Mwakyembe!!
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!mkuu saa mbovu wakati mwingine huonyesha majira sahihi!naomba tusipuuze mawazo ya mlevi kiasi hicho!
   
 8. M

  Msharika JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hao ndio vobaraka wa mafisadi, wanapewa fungu la kumi , wanaingiza nchi hasara ya matrillion. Watimue wote kabisa. Magufuli gooooooooo, gooo please, anza na MREMA wa TANROADS kwanza, kisheria Dkt wa ukweli, lowyer, mwaki=yembe atakujuza, chapeni kazi, hiyo ndiyo njia yako kuelekea 2015
   
 9. N

  Newvision JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ningemkubali anayosema kama angesema jamaa naye ni mwizi lakini kumbe kweli huyo ni mlevi na kama wako wengine kama yeye wahame wizara au waache kazi. Ni kwamba wamezoea kuiibia serkali halafu jioni wanakaa kwenye viti virefu bar wakijisifia wanapesa kumbe wizi mtupu!!!!!!!!!!!
   
 10. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Nimefurahia hapo nilipo-bold Red, Fungu la kumi. Terminology hiyo inatumika sana mahali fulani nahisi ndipo unapofanyia kazi. Big up hahahhaaa
   
 11. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  hao ni wezi wamezoea ten percent bila kufikiria kazi watakiona cha mtema kuni.

  mhusika badilisha hii title maana ni mawazo ya mlevi wa pombe na pia mlevi wa madaraka
   
 12. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kiongozi mzuri hana asilimia nyingi za kupendwa na wa tz anaofanya nao kazi......kwahiyo hii ni habari nzuri kwa magufuli
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  jamani mijadala mingine!
   
 14. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Analoongea mlevi ndilo lililo moyoni mwake, pombe inampa tu ujasiri wa kuongea mbele ya hadhara bila kujali ila wanajua wanachokiongea!
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Heading ya thread yako ina-mislead, mimi nilifikiri hatakiwi kwa sababu taifa litaangamia kumbe mijizi na mijitu inayolewa pesa za barabara ndio itaangamia. Hivi kwanza watu wanaolewa kila siku jioni pesa wanapata wapi?
   
 16. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwa nini hatima yake sio nzuri/ kisa kujali masrahi ya wananchi? wanaomchukia ni waroho na wachafu tu kama mtu si mpenda rushwa huwezi kumchukia Mgufuli,wanajua kuwa jamaa atabana mianya yote ya rushwa na wizi mpaka wakome kabisa, kwenye ujenzi nako yuko Tibaijuka najua kutakuwa na moto chini...
   
 17. muya

  muya Member

  #17
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sasa mleta maada sisi tutajifunzaje kutoka kwa mlevi
  mwalimu akiingia darasani na kata k wanafunzi tutajifunza nini kutoka kwake, huyo alisema alichotumwa na pombe
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Magufuri ni mwiba huwa hataki ujinga, unakumbuka wakt mkwere anaingia madarakani awamu ya kwanza jamaa walimvalia njuga ili akate tamaa but he survived. Jamaa anafanyakazi kwa data na uwajibikaji. Nina ndugu yangu anafanya kazi tanroads kakasirika kweli kusikia dr pombe ni bosi wake. Anasema kwa huyu bwana hakuna kulala!
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Wewe ndo ulikuwa BAR maangezi ya bar hayana TIJA JF


  Nyie ndo mnapenda mianya ya Rushwa kiboko yenu huyooooooo
   
 20. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hadithi umeitoa kwenye ulevi. Aliyezungumza ni mlevi halafu unamuonya. Mlevi? Ni mtu wa TANROAD?

  Haya waambie hao walevi Magufuli John Pombe yuko wizarani.
   
Loading...