Magufuli hatakiwi?

Magufuli hatakiwi?

kwanza heading ya thread na content vinatofautiana, cha msingi ni kuwa wale wala rushwa na wazembe wanamuogopa Dr (wa ukweli) Magufuri, lakini pia magufuri ni mchapa kazi
 
Watanzania ndivyo tulivyo, hatutaki kufanya kazi tunataka kupata maslahi kwa njia haramu! Magufuli hawachekei watu wa namna hiyo....
 
Sio la kushangaza hata kidogo, tunajua watanzania wengi ni wavivu.
 
Kuna jamaa mmoja anayehisiwa anafanya kazi miundombinu jana akiwa maeneo ya Mbezi tangi bovu akipata kinywaji, baada ya kuwa amelewa kidogo alikasirika sana kuwasikia watu wa meza ya pili wakisifia uteuzi wa Magufuli na Mwakyembe kwenda miundombinu anadai tokea Jk alipomteua Magufuli na Mwakyembe kuwa mabosi wao wapya, hali ya hewa siyo nzuri sana pale Wizara ya miundo mbinu kila mtumishi anataka ikiwezekana ahamishiwe wizara ya uchukuzi kuepukana na huyu mtu, wenye uwezo wa ku-robe wameanza kufanya hivyo, wafanyakazi wengi hawajafurahishwa maana walisha wahi kufanya kazi chini ya magufuli hali ilikuwa ngumu sana kimaslahi, wanadai ni mtu anayependa sana sifa kwa kuendekeza zaidi maslahi ya Taifa huku akiwaacha watumishi wakihaha kwa kuwabania mianya ya kujipatia pesa za ziada. Huku akijua fika mishahara ya serikali haiendi na wakati.

Jamaa anasisitiza "Usije ukashangaa ukiona wakandarasi wa barabara wanafunga sana makampuni yao kipindi hiki maana hili eneo litakuwa halilipi kama awali, ukitaka kuamini haya nenda ile wizara ya mifugo na uvuvi uone jinsi wanavyofurahia huyu jamaa kuondoka, mi binafsi simtaki kabisa"


Jamani tujifunze kutokuyazungumzia masuala ya ofisini tukiwa bar, nina uhakika huyu jamaa hatima yake siyo nzuri. maana waliokuwa wanamsikiliza walikuwa wengi.

Magufuli haendi kokote na atawafagia hawa mafisadi uchwara, Tanzania sio shamba la bibi Mwizi mwenyewe japo hamkubali ameogopa joto ya jiwe.

 



Tataizo kubwa ni kuwa nyie watu wa DAR mnapenda sana starehe na kura raha tuu nadhani kuna haja ya kuhamishia wizara zote Dar (to Dodoma) na ndio maana mwisha jisaha na kudhania DAR ndio TZ na mtabakia hivyo na ngojeni KATIBA ibadilike na mtaukimbia huo mji na mtakuja huku kwenye dhahabu nawambieni.

Kweli mko wizarani bado mwataka mlelewe kama mayai mliandika wenyewe wako mtiifu sasa mwataka kuikana tumikieni Taifa msilete ya ubinafsi hapo si mlitaka kazi wizarani mfanye sasa na kukimbilia Dar teh teh teh, Kumbe warudisha maendeleo mko wengi huko wizarani no wonder kuna kuwa na MAFISADI na majumba ya ajabu huko Dar Ati Kiwanja Billion Moja jamani hiyo Pesa mwaitowa wapi nchii hii imefika mahali pa kuuza kiwanja Bil 1???????

Kwa rushwa,10%,wizi na ubadhirifu wa kila aina mbona inawezekana?

Tatizo la watz wengi huwa hatujui tunachokitaka,unalalamika viongozi mafisadi,mkipata kiongozi mzuri napo mnalalamika watu gani nyie?
Wanaokula rushwa si ndio sisi?wezi na kwasaidia hao viongozi si ni sisi?wanaosaidia wafanyabiashara kukwepa kodi si ndio sisi?ni vizuri tukaacha ushabiki na kuropoka ropoka,tufikirie kwa makini tunachokitaka na tuishi hivyo kwa vitendo.
 
Mwambie amsalimie Kipande mtoa vibali vya wide load, maana naye ana kiburi cha aina yake.
 
Back
Top Bottom